Friday, July 19, 2019

POLENI WAFUGAJI, CHUKUENI HATUA HIZI KUWEZA KUTHIBITI CHANGAMOTO

*KONA YA UFUGAJI*

SEHEMU YA PILI

Habari rafiki yangu, nimatumaini yangu kuwa umeamka salama na kufanikiwa kuianza siku hii ya leo kwa ubora wa hali ya juu sana, kama ni hivyo nakupa hongera sana lakini pia natambua siyo wote tumepata fasi ya kuioa siku ya leo tukiwa na afya bora bali kuna wengine  niwagonjwa au wemeamka na changoto nyingi ambazo zimewafanya waianze siku hii kwa unyonge sana hawa nawapa pole sana kama kuna changamoto yeyote ya kiafya inakusumbua basi chukua hatua mala moja kuweza kuitatua changamoto hiyo na wewe ambaye umeianza siku yako kinyonge kwasababu mbalimbali basi chukua hatua kutatua changamoto hiyo mapema ili uweze kuishi maisha yenye maana. Kabla ya kuendelea mbele kwa heshima ya kipekee sana tumshukuru Mungu kwa neema yake yakipekee sana kwetu kuweza kutufanikisha mimi nawewe tuweze kuiona siku ya leo, siyo kwamba sisi ni wema sana au tunastahili sana kuliko wengine bali ni kwaneema yake pekee tumepata kibari kuiona siku hii ya leo,  hivyo tunalo jukumu kubwa kuhakikisha tunaishi maisha yenye maana kwa kwenda kuchukua hatua sahihi ili kuhakikisha tunafikia viwango vya juu vya maisha yetu, kwakuchukua hatua sahihi kwakila jambo basi maisha yetu yatakuwa bora sana.

POLENI WAFUGAJI, CHUKUENI HATUA HIZI KUWEZA KUTHIBITI CHANGAMOTO

napenda nichukue nafasi hii yakipekee sana katika mwendelezo wa somo la leo, katika somo lilopita tuliona jinsi changamoto ya magonjwa ilivyo tatizo kwa ufugaji wa kuku lakini hatukuishia hapo tu bali tulenda mbele kidogo kuona hatua za magonjwa ya kuku na hatua za kuchukua kwa kila hatua na leo twende tukaone hatua ya pili muhimu kuchukua ili kuweza kutatua changamoto ya magonjwa kabla hayajaingia.

2)THIBITI MAGONJWA KABLA HAYAJAINGIA

Katika ufugaji wa kuku kwa upande wa magonjwa kuna njia/vyazo mbalimbali vya magonjwa ambayo yamekuwa yakituletea hasara kubwa pale tunaposhindwa kuwapa tiba sahihi. Hivyo ili kupunguza au kumaliza kabisa changamoto hizo za magonjwa nimuhimu sana kufahamu vyanzo mbalimbali vya magonjwa ili tuweze kudhibiti magonjwa hayo yasiweze kuwaathiri mifigo yetu.

>chanzo cha kwanza.~mfugaji kutokuzingatia chanjo sahihi.
Ndio kumekuwa na changamoto kubwa kwa wafugaji kuto kuzingatia chanjo sahihi kwa kuku hai inayopelekea kuku kukosa kinga mwili kiasi ambacho ugonjwa kuwa rahisi kuingia. Changamoto hii inatokana na wafugaji wengi kufanya ufugaji kwa mazoe bila kuzingatia chanjo muhimu. Rafiki nimuhimu sana kuwa na maara ya chanjo sahihi kwa kuku wako kuanzi wakiwa na umri wa siku moja na kuendelea, chanjo hizo zinasaidia sana kuwakinga kuku na magonjwa, mfano wa chanjo hizo nikama vile kideri, mdondo, ndui na magonjwa ya matumbo. Kwenye kitabu nimeeleza hili kwa kina katika sura ile ya kumi na saba na ukurasa wa 250.

>chanzo cha pili~ mazingira machafu ya kuishi mifugo.

Hii ni moja ya sababu kubwa ya kuku kuugua magonjwa mala kwa mala, kuku wanapokuwa kwenye mazingira machafu inawasababishia wale sehemu ya kinyesi chao na uchafu mwingine uliopo kwenye banda kiasi ambacho inakuwa rahisi kuku kupata magonjwa. Njia sahihi ya kudhibiti tatizo hili nikuhakikisha banda lako linakuwa safi nakavu mda wate hii itakusaidia sana kuwakinga kuku wako na magonjwa ya mala kwa mala, lakini pia unaweza kuwatengenezea cage ambayo itawafanya kuku wako wale kwa juu na uchafu wowote uweze kushuka chini hii itawasaidia sana kuku wako washindwe kula uchafu ulio bandani kwasababu uchafu wote unakuwa upo chini, hii ni moja kati ya njia bora sana kuhakikisha unapungua kwa sehemu kubwa ya magonjwa kwa kuku wako.

3)chanzo cha tatu~kuku kukosa kinga katika mwili wake.

Hii ni sababu muhimu sana ya kuku kupata magonjwa ya mala kwa mala. Ipo hivi rafiki, chanzo cha kuku kuugua nikutokana na kuku kukosa/kupungua kwa kinga ambazo zinahusika katika kudhibiti ugonjwa huo na hii inasababishwa na aina ya chakula ambacho kuku wetu wanakula, hivyo ili kuongeza ufanisi mkunwa kwa kuku wako nimuhimu ukawapa chakula ambacho kinaenda kuogeza kinga kwa wingi katika miili yalo hali itakayopelekea kuku wako kuishi bila kuugua, hapo ndipo utakapo kutana na mimea ambayo inakiwango kikubwa cha kinga ambacho kinasaidia kuwafanya kuku wako wawe na kinga nyingi mwilini zakuweza kukabiliana na magonjwa mbalimbali. Hapo ndipo unapokutana na mimea yenye viwango vikubwa vya kuwaongezea kinga kwa kuku, uzuri wa mimea hii ni sehemu ya lishe kwa kuku na baadhi ya mimea hiyo nikama vile azolla, hydroponic fodder (mimea hii nimeieleza kwa undani kwenye kitabu katika sura ile ya kumi na sita na ukurasa wa 229) ukiachana na mimea hiyo ipo mimea mingine kama vile alovera, majani ya mpapai, majani ya mpera, mronge, mwarobaini, pilipili kichaa, na mrose (mimea hii yote nimeieleze kwa undani kwenye kitabu katika sura ile ya kumi na tisa ambayo inapatikana kwenye ukurasa wa 303) kwa kufanya mambo haya utapunguza kwa kiasi kikubwa cha magonjwa kwa kuku wako hali itakayopelekea uweze kupata faida kwa kuku wako.

Rafiki kama umekuwa mmoja ya wafugaji ambao unapitia changamo kubwa katika ufugaji huu wa kuku basi naomba tuwasiliane ili nikushauri njia sahihi zakuweza kuondoka katika changamoto hizo.

Ni mimi rafiki yako
Mwandishi na mwalimu wa ujasiriamali
Frank mapunda
Unaweza kunipata kwa mawasiliao namba
0758918243
0656918243
0786115129

PIA UNAWEZA KUJIFUNZA ZAIDI KUTOKA KWANGU KUPITIA VITABU HIVI

*TAJIRIKA KWA UFUGAJI WA KUKU*

HARDCOPY 15000/=
SOFTCOPY 7000/=

*NGUVU YA MAARIFA KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA*

HARDCOPY 15000/=

SOFTCOPY 10000/=

ASANTE SANA KWA KUWA PAMOJA NAMI ENDELEA KUNIFATILIA KWA MAARIFA BORA YATAKUYO INUA MAFANIKIO YAKO, MDA SI MREFU UTAWEZA KUNIPATA KWA NJIA YA BLOG HII *www.nguvuyamaarifa.blogspot.com*

Tuesday, May 8, 2018

UNATAKIWA KUFANYA NINI KWA WALE WANAOTUMIA MAPUNGUFU YAKO KUKUSEMA VIBAYA ?



" Hapa duniani kuna makundi 2 ya watu ;

1. Kundi la Albert Einstein - Hawa ni watu ambao wana maono na mawazo ya mbali lakini watu wengi hawawaelewi na inawezekana wanaonekana kama hawana akili na wamechanganyikiwa kwa sasa. Inawezekama kuna watu wanawaelewa lakini hawaamini kwasababu wengi wanasema hawapo sahihi lakini naimani kuna siku wataeleweka na watu watasema walikuwa sahihi.

2. Kundi la Charlie Chaplin ;  Hawa ni watu ambao wanafanya mambo kwa ukimya hawana maneno sana na ni wachache sana wenye akili ya kufikiri pia huwaelewa wanafanya nini lakini kuna wengine wanaona kwa ukimya wao kitu wanachokifanya hakieleweki na hakina maana yoyote kwa wakati huu.  Naimani watakaposonga mbele na kuamini wanachokifanya kuna wakati watu watawaelewa." - Lazaro Samwel

Usiache hata siku moja mtu kutumia mapungufu yako kuwa kama gia ya kupata kuongea kwa wengine na wewe kufanya makosa yasiyokuhusu. Wala usiruhusu mtu kutumia kushindwa kwako iwe sababu ya kupata mada ya kuongea katika makundi ya watu na kuonesha kwamba wewe sio kitu na yeye ni kitu.

 Kivipi sasa unaweza kufanya hivi ?

1. Usibadilike kwa maneno yake ya kujaribu kukushusha kama mwendo ulikuwa wa mbele basi amka na songa mbele.

2. Usitumie na wewe muda wako kwenda kuongea na watu kuhusu ubaya wa huyu anayekusoma , wewe piga kazi na kazi yako ndiyo iongee kwa wale walioambiwa kuhusu kuanguka kwako au mapungufu yako.

3. Usiwachukie wale walioambiwa wala yule aliyewaambia, show love and be real kwasababu ukweli haujifichi na haufichi kweli yake na uwongo haujifichi kuonesha uwongo wake.  Mwisho wa siku itajulikana kipi ni kipi na nai alikuwa mbaya.

4. Usipoteze muda wako kuwaza kwanini amewaambia wengine kuhusu kuanguka kwako au mapungufu yako kwasababu kilichoongewa hakiwezi kurudishwa tena mdomoni na maneno ya uwongo hupingwa kwa matendo. Wekeza muda wako katika kujifunza kwenye kuanguka kwako, wekeza muda wako kwenye kujifunza jinsi ya kwenda sawa na mapungufu yako yani ujue wapi uongeze uimara na sio kuwa mkamilifu.

Enjoy Your Day.

Kocha Lazaro Samwel
0753616584 or lazarosamweli41@gmail.com
#akiliyaushindi

KWANINI UNATAKIWA KUSONGA MBELE KWA KILE UNACHOKIFANYA ?


" Mdomo wako unaweza kutamka kutaka mafanikio lakini maisha yako yakakana uliachozungumza na kukinena kwa watu. Ulipewa mdomo mmoja, miguu miwili,  masikio mawili,  mikono miwili  na akili ili utende kwanza kuupa mdomo wako uhakika wa kuongea kitu sahihi, hakikisha unavitumie ipasavyo kabla ya mdomo wako." - Lazaro Samwel


1.  Songa mbele kwasababu kitu chako hakijakubeba wewe tuu tambua katika shughuli yako kuna ndoto za watu wengine pia umezibeba kuweza kutimia.

2. Songa mbele kwasababu sio kila mmoja ambaye anapenda kusaidia wengine kama wewe unavyofanya unachokifanya.

3. Songa mbele kwasababu inawezekana ile historia mbaya katika uzao wenu wewe ndiye unatakiwa kuibadilisha mfano inawezekana watu wanasema katika familia yenu hakuna mtu ambaye anaweza kufanikiwa,  inawezekana pia toka zamani mlinenewa kwamba maisha yenu hayawezi kubadilika. Wewe unaweza kuwa mkombozi.

4. Songa mbele kwasababu kuna alama unatakiwa kuiacha katika uso wa dunia hii na katika uzao wako na alama hiyo sio ya kusahaulika.

5. Songa mbele kwasababu hata yule anayekwambia kwamba huwezi anahitaji msaada wako kupitia mafanikio yako. Kuna watu wameshakata tamaa na maisha na wewe wanakukatisha tamaa kwasababu wao walishashindwa sasa mafanikio yako yanaweza kuwa chanzo cha wao kubadilika na kuona kumbe inawezekana.

6. Songa mbele kwasababu suluhisho la changamoto au matatizo yako sio kuacha unachokifanya au kukata tamaa, suluhisho ni kusonga mbele na kushinda au kufanikisha malengo yako bila kutazama maumivu yako.

Kocha Lazaro Samwel
0753616584
#akiliyaushindi

Thursday, April 19, 2018

NINI HASWA TUNAJIFUNZA KUTOKA KWA KAZIMOTO NA MANASE KATIKA KITABU CHA KICHWAMAJI ?


Wakati nasoma kitabu cha KICHWAMAJI kilichoandikwa na Mr. Euphrase Kazilahabi nilijiuliza maswali mengi sana wakati naendelea kusonga mbele katika kurasa za kitabu hiko, moja wapo ya swali lilikuwa ni ukichwamaji katika kitabu hili upo kwa nani au wapi?  Je ni Mr Manase kwa tabia yake kutembea na wanawake bila mpangilio au ni kazimoto kwa tabia yake ya kutaka kulipiza kisasi kwa rafiki yake Manase baada ya kufanya kitendo kibaya kwa mdogo wake aliyeitwa Rukia ?

Sikupenda kwenda mbali snaa kwasababu niliona kama wote ni vichwamaji  ikabidi sasa nirudi katika kamusi ya Kiswahili- Kiingerezaya TUKI iliyochapishwa mwaka 2001 kuangalia nini maana ya neno kichwamaji ili nisimuonee Kazimoto wala Manase, nikaona wamesema kwa lugha ya kigeni kwamba KICHWAMAJI- Silly and stubborn person, tukitafsiri kwa lugha yetu  inamaana ya "MTU MJINGA NA MKAIDI."

Niliendelea kusoma kitabu lakini mwisho wake nikagundua ujinga ulikuwa wapi na ukaidi ulikuwa wapi.

Ujinga ulionekana kwa Kazimoto kwamba baada ya mke wake kupata mimba lakini kwa bahati mbaya mke alipokuwa akijifungua mtoto alikufa kwa uchelewaji wa daktari katika kutoa huduma kwa Sabina ambaye alikuwa mke wa Kazimoto na kwasababu Kazimoto alikuwa na shauku ya kupata mtoto basi alikata tamaa kabisa ya maisha na kuona kama mtoto amekufa sasa ya nini kuendelea kuishi, sababu ingine ni kwamba alipata habari ya ugonjwa ambao rafiki yake Manase alikuwa nao na hapo hapo unakuta Kazimoto alishatembea na wasichana ambao pia Manase alishatembea nao kwahiyo akadhani kwamba na yeye atakuwa na ugonjwa huo ambao haukujulikana ni wa aina gani zaidi inasemekana kama mtu alikuwa na ugonjwa huo hata watoto ambao atawazaa watakuwa  na kicha kikubwa ikiwa ni athari ya ugonjwa huo.Hiki pia kilimchanganya na kasahau kwamba bado wananafasi ingine ya kuweza kusonga mbele na mke wake kuweza kupata mtoto mwingine au kwenda kufanya uchunguzi zaidi kujua tatizo ni lipi haswa na wanawezaje kukumbana nalo kulishinda.

Tunaona ujinga kwa Kazimoto kutokuamini katika uwepo wa Mungu licha ya mke wake kumwelewesha juu ya uwepo wa Mungu na hii ndicho kitu amnacho nadhani hata kilimsababisha kuendelea kuteseka kinafsi na kuona kesho yake sio nzuri. Ndio maana mwishoni kabisa mwa kitabu kurasa ya 194 Kazimoto alipokuwa bado ana maneno yake hasi juu ya kwanini anaishi tunaona Sabina baada ya kuchoka tabia yake ya kuongea maneno hayo kila muda alimwambia  " Hakika sikufahamu kwamba wewe ni kichwamaji namna hii !!  Sikufahamu !! "

Na mwishoni kabisa tunaona Kazimoto akijiua kwasababu ya kuhofia ugonjwa huo na changamoto ambazo alikutana nazo.

Upande wa pili ambao tunaona ujinga na ukaidi ni kwa Manase ambaye alikuwa rafiki yake na Kazimoto, huyu akionesha ujinga na ukaidi vyoye kwapamoja kwa kutembea na wanawake bila utaratibu wowote lakini pia kwa kum'baka mdogo wake na Kazimoto na mwisho wa siku kusababisha kupata mimba ya kutokutegemea mpaka kusababisha kifo chake alipokuwa akijifungua.

Licha ya Manase kutokutokea sana kuelezewa katika kitabu cha KICHWAMAJI lakini matukio yake yalikuwa makubwa sana tofauti na Kazimoto na yalikuwa na mafunzo makubwa sana.

Manase alikuwa msomi mwenye cheo cha ukuu wa wilaya serikalini lakini kwa jinsi alivyokuwa kwa tabia yake alionesha picha ya wasomi ambao wamesoma lakini hawajaelimika, kwasababu elimu yake inaonekana haikumsaidia kutambua nafasi yake katika jamii na kujua wajibu wake kama kiongozi pia.  Alitumia cheo chake kutembea na wanawake wengi bila nidhamu yoyote,  alitumia elimu yake kupotosha watu ili tuu apate hongo, alitumia elimu yake kushusha thamani ya watu ambao hawana  maisha ya juu kama yeye.

Nataka tujifunze kitu kimoja katika maisha ya watu hawa wawili.

1. Elimu yako isiwe ni chanzo cha kuongeza matatizo katika maisha ya watu wengine kama Manase jitahidi sana elimu yako iwe ni suluhisho katika maisha ya watu wengine.

2. Cheo chako kisiwe chanzo cha kunyanyasa walioko chini yako wala usiigize kuwa na heshima kwa wale tuu ambao wanaweza kukupatia kitu.

3. Jitahidi sana kupenda majirani zako wala usijenge uadui nao kama familia ya Manase ilivyokuwa na uadui na familia ya Kazimoto kisa ardhi.

4. Ukifanya kosa jana na ukatambua kwamba ulifanya kosa basi usiifanye kesho kuwa jana kwa kujuta tena kwanini jana ulifanya ulichokifanya.

5. Chunga sana tabia yako kwasabahu huwezi kujua ni wangapi wanajifunza kwa matendo yako, Kazimoto pia kitu kingine kilichomfanya ajiue kwa Bunduki ilikuwa ni kujuta tabia yake kumharibu mdogo wake na mwisho wa siku kusababisha kifo n.k

Nimekuweka tu hawa watu wawili kwa leo ujifunze kitu licha ya kwamba kuna watu wengi sana katika kitabu hiki cha Kichwa maji wenye mafunzo makubwa sana siku ingine nitaweka wahusika wengine ili tuendelee kujifunza zaidi katika kazi hizi za fasihi.

Kocha Lazaro Samwel
0753616584
#akiliyaushindi

Monday, April 16, 2018

JE NI KWELI KILA UNACHOHAMASISHWA UNATAKIWA KUKIFANYA ?


Sio kila unachomasishwa unatakiwa kukifanya, unatakiwa kuwa makini sana katika hili kwasababu unaweza shangaa unapoteza muda na kuja kumlaumu yule aliyekuhamasisha  au kukuelimisha.
Ni jambo la busara sana kuwa makini sana na kujichunguza ndani kwa kujiuliza je nilichohamasishwa au ninachohamasishwa kukifanya jee ni jambo ambalo liko ndani ya wangu ?  yani unalipenda kwelii au ni kwasababu tuu umepata hamasa muda ule kulifanya ?

Hii inanikumbusha wakati nafanya Network Marketing Business watu waliokuwa wakihudhuria katika semina yaani Business Opportunity Meeting  wengi walikuwa wanaingia au kuchukua maamuzi ya kufanya biashara kwa hamasa tuu ya kuona mtu flani kapata kitu flani na sio wao wenyewe kutoka ndani yao kuwa na nia ya dhati kufanya hiyo biashara. Mwisho wa siku unakuta kuna malalamiko mengi sana kwa watu ambao unakuta waliwaingiza watu hao.

Utasikia, "Wewe uliniambia hivi ndio maana nikaingia kuifanya biashara hii." hapo unakuta kwasababu ya biashara kuwa na changamoto flani licha ya mara ya kwanza kuambiwa biashara hii iko vipi.
Nachotaka kukwambia ni kwamba hisia zinaweza kukufanya kufanya maamuzi ambayo sio sahihi pale unapokuwa na hamasa kwahiyo jitahidi akili yako isifungwe na hisia za hamasa yako na kuwa na nafasi ya kufikiri kabla ya kutenda katika kile unachohamasishwa.

Sio kila anayekuhamasiaha yupo sahihi na wala sio kila unalolisikia ni kwaajili yako kuwa makini na pembua mambo kwa umakini.

Kocha Lazaro Samwel
0753616584

MIFANO HII ITAKUFUNGUA KATIKA MAISHA YAKO


Utasikia ooo wewe hiyo biashara haikufai,  ooo wewe huna lolote unaigiza tuu,  ooo wewe bado mdogo kula kwanza bata achana na mambo ya kiutu uzima, ooo hiyo biashara inakudhalilisha, ooo huwezi kuwa mwanamitindo,  ooo wewe huwezi kuwa mwandishi,  a lot of blaaah blaaah utazisikia sana tena hata kwa watu wako wa karibu sana ambao ulikuwa unadhani wangekupa ushauri mzuri.

Wakati Shakira akiwa anajifunza mziki mwalimu wake alimwambia "Shakira unasauti kama ya mbuzi." lakini Shakira hakukata tamaa na naimani kwa sasahivi ukiambiwa kuhusu Shakira na sauti yake unaelewa nachokwambia,  sio tena sauti ya mbuzi kama mwalimu wake alivyokuwa anasema, sio hivyo kama ulitazama kobe la dunia mwaka 2006 lililofanyika Afrika Kusini utakuwa unakumbuka mwimbo wake wa "WAKA WAKA".  Robert Goddard moja ya watu ambao leo hii mawazo yake yamechangia katika urukaji wa roketi kwa mara ya kwanza marafiki zake walimcheka sana kwa mawazo aliyokuwa anawaambia na muda mwingine hata kumzomea, Thomas Edison mvumbuzi wa balbu ya umeme aliambiwa na mwalimu wake kwamba " Ni mjinga kuweza kujifunza chochote." lakini leo hii tunaongea mengine na inawezekana hata uzao wa mwalimu huyo wake wanatumia Balbu zake, mchoraji Vincent Van Gogh wakati wa uhai wake michoro yake iilikuwa inadharauliwa sana na katika uhai wake ni mchoro mkoja tuu ambao akiuza kwa rafiki yake tena kwa bei ya chini sana lakini leo hii mchoro wake unauzwa zaidi ya dola milioni 100 ($100million's)

Nachotaka kukumbusha ni kwamba umeua ndoto zako ngapi kwa maneno ya watu ?  je unajua leo ungekuwa wapi kama ungesonga mbele katika ndoto uliyokuwa nayo ?  Kuna umuhimu gani kumsikiliza mtu anavyokukatisha tamaa ikiwa unajua hajui unachokijua hata kama ukimweleza ?
Nikukumbushe tuu kwamba kuna maneno mengi sana ambayo ukiwa kwenye safari yako ya mafanikio utayasikia na lengo unakuta ni kutaka kukutoa kwenye lengo lako husika haswa kisa wanaokwambia wako pembeni na hawaoni wewe unachokiona kule unapotazamia kwa kile unachokifanya.Unachotakiwa kukifanya ni usikilize tuu ile sauti inayokuita kule unapoangalia na kutaka kufika na hizi za pembeni waambie mpaka nifike ninapopaona lakini nyie hampaoni.

πŸ†• Utakuwa umefanya la maana sasa kubonyeza link hii kwa chini kudownload Application yako pendwa ya LAZAROSAMWEL kupata masomo mengine mengi ambayo inawezekana kipindi cha nyuma ulikuaa unafuatilia , bonyeza πŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎπŸ‘‡πŸΎ
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.lazarosamwel.app

Kocha Lazaro Samwel
0753616584
#akiliyaushindi

Friday, February 23, 2018

MTU AMBAYE HUTAKIWI KUMTILIA MAANANI

"Imani ni kama mbegu. Inakuhitaji kukumbuka kwamba mbegu hainenepi wala haikondi bali inakua, licha ya hivyo vyote mbegu lazima uipande, uiwekee mbolea, uipalilie na kuwa na uangalizi mzuri kutokushanbuliwa a wadudu n.k ili iweze kuzaa matunda bora zaidi. Hata wewe lazima uwe na imani ya mafanikio, ni lazima uhakikishe unaipanda mbegu ya imani na kuifanyia kila kitu ili baadae ikupe matokeo mazuri zaidi.Cha msingi zaidi kumbuka Imani bila matendo si kitu."

Mtu ambaye hutakiwi kumtilia maanani sana katika maisha yako;

1. Mtu ambaye anapenda  kazi au shughuli yako zaidi ya wewe. Huyu ni mtu ambaye atakupenda au atakuona wa maana ukiwa na kitu lakini ukikikosa kwake thamani huna tena, sio vyema kujitoa kwake sana wala kumpatia muda wako.

2. Mtu ambaye anashindana nawe kwa nia ya kutaka kuwa juu yako kwa kitu unachokifanya. Mashindano hayakatazwi kwasababu  huwa yanaonesha ubora wa mtu lakini mashindano bora yenye kuonesha ubora bora ni ule unaomfanya mtu kushindana na yeye mwenyewe kuwa bora.

3. Mtu anayetaka kuchuma vyako tuu badala ya kujifunza katika uchumaji wako na yeye ajue jinsi ya kuchuma vyake. Mtegemea cha nduguye hafi mwenyewe masikini lakini hata yule anayembweteza hufa masikini pia.

4. Mtu ambaye anajiona anajua kila kitu.Huyu ni hatari kwasababu hauwezi kushauriana naye wala kubadilishana nae mawazo, kila kitu atakuwa anajiona sahihi na wewe hata kama utakuwa sahihi mawazo yako yatashushwa chini na kuonekana sio kitu. Muda mwingi  hawa huwa ni wakatisha tamaa na wabinafsi kimawazo muda mwingine kimatendo kabisaaπŸ˜€.

5. Mtu anayependa kufanya wenzake wafuasi wake bila hata kuwafundisha chochote ambacho kutawasaidia na wao kuweza kupandikiza mbegu bora kwa watu wengine.

6. Mtu asiyependa kuwa kichocheo cha mabadiliko yoyote. Hawa utakuta kila unachotaka kubadilisha wenyewe hupinga tu hata kwa sababu ambazo zinaonekana wazi wazi hazina uzito wowote.

n.k

Kocha Lazaro Samwel
0753616584
#akiliyaushindi
#MwongozoKatikaMafanikio