Karibu
Mpenzi msomaji wa makala Hizi za Lazaro Samwel
nikiamini mwanzo wako wa kusoma sentensi hii ni kutaka kujua zaidi kwamba
wewe kama kijana kunamambo gani ambayo huyajui na unatakiwa kuyajua ili uweze
pia kuelimisha wengine baada yaw ewe mwenyewe kuweza kuelimika.Naimani mwisho
wa makala hii utakuwa mtu wa tofauti na fikra tofauti pia katika maisha yako
haswa kama kijana. Kwa kuanza kabisa“Kijana
ni kama mbegu ambayo iko aridhini ili iweze kustawi ni lazima kila siku iweze
kumwagiliwa maji,kuwekewa mbolea vizuri na kupaliliwa ili itoe mazao bora”
–Lazaro Samwel
Kijana
wa kitanzania kukutana na changamoto za hapa na pale katika maisha yake ni kutokana na maandalizi ambayo amepewa
kuanzia kwenye familia yake,shuleni na yeye mwenyewe jinsi alivyojiongeza
katika maisha yake ya ujana.Changamoto nyingi ambazo huwa zinawakumbuka vijana
wa kitanzania kwa asilimia kubwa cha kwanza hatakiwi kulaumiwa kwa upande,mana
mafanikio ya kijana huyu kuondokana na changamoto yanaanza toka alipokuwa mdogo
na ukiangalia malezi mengi ya kitanzania ni kumtoa mtoto katika kusudi lake na
kumweka katika kusudi la serikali kwamba huyu motto anatakiwa akue,aende
shule,afaulu aajiriwe na aitumikie serikali.Kwanini mzazi asifanye kwamba mtoto
wake anatakiwa aende shule agundue kipaji chake na ajiajiri? Utajiri wa kijana
unaanza kuutenegeneza kwa kutunza muda wake toka akiwa mtoto na utaharibu
maisha ya kijana kwa kuuchezea muda wake toka akiwa mdogo.Tusije na siasa
kwamba ni uzembe kijana kupata ajira ila ni uzembe kwa serikali kupoteza muda
wa kijana toka akiwa shuleni na imani ya kuajiriwa akaacha kuwaza kuhusu
kujiajiri.Mana tukumbuke kila jambo linachukua muda na hata kujiajieri sio
jambo la kuamka leo na kesho kujiajiri hapo bado tutakuwa tunatengeneza taifa
bovu,kijana lazima achukue muda kujijua na kujitafakari na kujua achukue muda
kujifunza nini na sio anamaliza mwaka wa 3 chuo na kiongozi anasema kwamba
anashangaa kuona kijana mwenye stashahada anakosa ajira,kwanini kiongozi
ushangae wakati wewe ulimwambia kwamba asome utampatia ajira na sio kwamba
atajiajiri? Licha ya hivyo lakini pia hata elimu anayopewa darasani ni ya
kuambiwa kwamba ukienda kufanya kazi unatakiwa kufanya hivi na sio ukienda
kufungua Kampuni yako unatakiwa kufanya kitu flani namna flani.
Hii ndo
Tanzania ya elimu bure na sio elimu bora, na tusipoangalia tunapoelekea kwa
kubadilika kwa nyakati hizi tusishangae vijana wa Tanzania wakawa watumwa
katika inchi yao kwa kutumikia watu wengine kutoka inchi zingine pia.Serikali
ya Tanzania ikitaka kupunguza pia hili swala la vijana kukosa ajira isianza kwa
kungangania kutengeneza viwanda ila ihakikishe kwa kizazi hichi ambacho kinakuja
na hata ambacho bado kipo kwenye huu mfumo wa elimu wanajikita katika
kutengeneza elimu bora ya vitendo ili vijana wawe na uhakika na maisha sio
kijana anaenda shule hana vidonda vya tumbo anaondoka navyo kwasababu ya msongo
wa mawazo ya nini hatma ya maisha yake mana hata alipotoka na elimu yote
anajiona bado ni mtupu.Tatizo sio mbegu
ila ni mpanzi.
Kama
nilivyosema kwamba kijana ni kama mbegu na inatakiwa kumwagiliwa,kuwekewa
mbolea lakini na kupaliliwa haya yote yakikosekana mwanzo mwisho wa siku hii
mbegu haiwezi kutoka mazao ambayo tuliyatarajiwa lakini sasa tusilaumu mbegu
kwanini haijatoa mazao ambayo yanatakiwa tulaumu aliyepanda mbegu lakini
akashindwa kumwagilia,kuwekewa mbolea na kupalilia
Nakushukuru
kwa muda wako ambao umeutumia kusoma makala lakini kunawengi ambao hawajapata
chansi ya kusoma makala hii jaribu kushare nao nao wafunguke.Ulikuwa nami ;
Lazaro Samwel mtunzi na mwandishi wa kitabu
cha NGUZO 3 ZA MAISHA,kwa
mawasiliano zaidi tunaweza wasiliana kwa namba hizi 0753616584 au 0653386586
Ujumbe mzuri, na jambo ambalo tunalotakiwa kufanya sisi kama vijana ni kuachana na fikra zote ambazo zitatuondoa katika kutekeleza yaleyote ambayo tumeplan kufanya.
ReplyDeleteNi kwelii kabisaa Mr Athumani Unachosema vijana inabidi tufunguke zaidi ya sasahivi tulivyo kwamaana mambo yanapoelekea inabidi sisi wenyewe ndo tuwe mabadiliko katika inchi hii.
Delete