Tuesday, May 2, 2017

TABIA 7 ZA KUACHA KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO


Tokeo la picha la HABIT TO LEAVE

Sponsered by NGUZO 3 ZA MAISHA.

Habari msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel, najua wewe ni mtu wa pekee sana na unajua thamani yako mpaka umeamua kuchukua muda huu kusoma makala hii kwa muda huu. Leo hii salamu zangu nitazielekeza kwako katika kuangalia mambo muhimu ambayo unatakiwa kuacha ili uweze kuishi maisha ya ndoto zako au ili uweze kufanikiwa, nitasalimu haswa Watanzania wenzangu na itakuwa vizuri nikisema mambo ambayo watanzania wanatakiwa kuacha ili waweze kufanikiwa.

Naomba kuanza kama ifuatavyo.

1. Ni Lazima Uache Tabia ya Kusema Uongo katika jambo Lolote.

Najua itakuwa ni mshangao wa hali ya juu kuhusu kusema uwongo na mafanikio mana unaweza kuona mbona wengine wanakuwa matajiri kwa kudanganya wengine? Lakini huo sio utajiri wa kweli ambao tunausemea, kuwa tajiri inamaana ni kuwa na amani, upendo na ushirikiano kwa kile ambacho unacho. Wengi wanakuwa matajiri lakini kwa kudanganya kwao wanakuwa hawana amani ya moyo na mara nyingi huishia kufa mapema na kutokufaidika na hizo mali zao.

2. Acha Tabia Ya kuwa na Roho ya kutokupongeza mwenzako kwa kizuri alichokifanya.

Hapa wengi ndipo tunapoangukia mana kuna watu wao kazi kubwa katika mambo ambayo wanafanya wengine ni kutokuwatia moyo wenzao lakini ni kutafuta makosa tuu na kuwakatisha tamaa, ukiwa na hii tabia acha kabisa mapema jitahidi kuwapongeza wenzako ambao wamefanya vizuri nawe kwa madogo iliyokuwa nayo yatakuzwa na Mungu. Mungu hapendi mtu mwenye Roho mbaya na hawezi kukusaidia ufanikiwe zaidi mana anajua wewe kwa roho ya namna hiyo ukifanikiwa utawatesa wengi sana na utawakatisha tamaa mana hautataka watu wakupite.

3. Acha Tabia ya Kujitamkia maneno mabaya.

Kumbuka ukitaka kufanikiwa na kuishi maisha ya ndoto zako lazima ujitamkie maneno mazuri hata kama uko katika wakati mbaya namna gani unavyojitamkia ndivyo unavojenga hari ya kuweza kufanikiwa mana itakuwa tabia na tabia itaelekeza katika kweli kutimiza ile ndoto yako. Lakini ukiwa mtu wa "mimi siwezi" ndugu yangu hili neno dogo sana lakini linaweza funga milango mingi sana ya mafanikio katika maisha yako, liache kabisa hili neno na anza kutumia neno NAWEZA kila siku unapolala hata unapoamka hebu jitahidi na hakikisha kwamba unajinenea maneno ya ushindi mara TATU (3) mfano NAYAWEZA YOTE KWA YEYE ANITIAE NGUVU au HAKUNA JAMBO LINASHINDIKANA JUU CHINI YA JUA. Maneno yako ni ufungua kwa mambo mengi sana kama hujui.

4. Acha Tabia ya kudharau watu.

Dharau kwa watu ni kujenga ukuta au kujiweka mbali na njia nzuri ya mafanikio katika maisha yako. Ukiwa na dharau ni kama kupunguza baraka ambazo ulikuwa unatakiwa kupata, ukiwa na dharau umemdharau Mungu na umbaji wake kwahiyo yeye hataona haja ya kuweza kukufanya ukafanikiwa mana utadharau wengi.Achana na hii Tabia na heshimu kila mmoja utaona mambo yako yanavoenda.


5. Acha Tabia ya kukataa kujifunza.

Hapa watanzania wengi tupo pia mana mtanzania yupo radhi/tayari kutumia nguvu kupata hela lakini asitake kupata maarifa ya jinsi anavyoweza kubadilisha maisha yake  kwa kutumia akili. Kwa sasahivi vitabu viko vingi sana na ambavyo watu wanaweza badilisha maisha yao lakini wamekuwa wavivu kusoma, hapohapo wanasema uchumi mbovu ila pia najiuliza wanapata wapi hizi hela za disco 10,000/= na mpira 5000/= mpaka 20,000/= uwanja wa taifa alafu wanalalamika maisha magumu? Maisha sio magumu na wala uchumi haubani kiasi hicho ila sisi akili zetu tumezibana, uchumi wetu tumeubana wenyewe. Kwanini usinunue kitabu kwa 5000/= au 10,000/= nakuendelea kikakusaidia katika maisha yako? Huu ni uzembe na watu hawajaamua.Kunadada mmoja aliniambia Lazaro mimi sio mtu wa kusoma vitabu ila nataka kuanza kusoma vitabu kwa kuanza na kitabu chako, nilifurahi sana kwamba kuona dada anamoyo kama huo nikasema tukipata watu kama hawa Tanzania tutakuwa mbali sana haswa kwenye kubadilisha maisha yetu.

6. Acha Tabia Ya Kudhani Kwamba Mafanikio Hayaji kwa Kusali au kumwomba Mungu.

Hii sentesi naona imejitosheleza na naimani umeielewa vizuri. Jua tuu sala ni mawasiliano baina yako na Mungu wetu kwahiyo tukitaka kufanikiwa vizuri zaidi ni lazima tuweke mawasiliano mazuri baina yetu na Mungu na ukitaka kuweka mafanikio yako mbali weka mawasiliano yako na Mungu.

7. Acha Tabia Ya kuwa Mwoga.

Uwoga ni mjumuiko wa tafsiri hasi ya maneno ambayo unayasikia na kuambiwa na kuyaweka katika akili yako mfano Unaambiwa Jaribu kuimba unasema siwezi, yani hapo ndipo unapotoa tafsiri hasi mana hata haujajaribu kuimba unasema huwezi, hata haujafanya mazoezi ya kutosha umeshaona mpira mgumu, hata haujawahi kuendesha gari lakini unasema gari gumu kuendesha, unapewa kazi kuifanya unasema ngumu na siwezi kuifanya ingali hata haujawai kuifanya. Haya ni mambo ya kukimbia.

Naomba kuishia hapo japo kunamengi mengine ambayo unajua unatakiwa kuacha kama uvivu, wizi, n.k

LAZARO SAMWEL  .
Contacts ;0753616584 / 0653386586
Email     ; lazarosamweli41@gmail.com

KARIBU UPATE COPY YA KITABU CHA NGUZO 3 ZA MAISHA KAMA KWELI UNATAKA KIBADILI MAISHA YAKO.
.
.

0 comments:

Post a Comment