Friday, May 5, 2017

JIANDAE NA IFANYE KAMPUNI YAKO IWE NA MATOKEO MAZURI


Tokeo la picha la quotes about a leader in an organization

Habari mpenzi msomaji wa makala za Lazaro Samwel naimani tuko pamoja na unafuatilia ipasavyo maarifa haya na kila siku zinakufanya kuwa mpya.Naomba tuendelee kuwa pamoja  mana nazidi kukuona mbali zaidi ya jana na zaidi ya changamoto ambazo unapitia kila siku.

Katika kazi ambayo huwa  nikifanya nilishakutana na vijana wenzangu ambao wao waliamua kuchukua hatua ya kuweza kuungana pamoja na kufungua kampuni lakini baada ya muda flani kampuni yao ilikufa na wote wakasambaratika.Lakini nikawa najiuliza kwamba ni kitu gani ambacho kinafanya hawa vijana ambao ni fresh from school kutokusonga mbele na kufanikiwa kupitia hizo kampuni zao? Lakini kunakitu kimoja ambacho nilijifunza baada ya mazungumzo ambayo nilikuwa nikisikiliza kwa hao vijana,haswa ni kwamba Hawa marafiki zangu walikuwa na kiu ya kuwa na kampuni na sio kuwa na kiu ya kuona matokeo mazuri kutokana na kampuni ambayo walikuwa nayo. Hapa namaanisha nini katika msemo huu ambao nimesema hapo juu? Kiu ya kuwa na kampuni haiwezi kumfanya mtu kuweza kufanikiwa lakini maandalizi ya kuwa na kampuni ambayo itakuwa na matokeo mazuri ndicho chanzo cha mafinikio.Ni lazima kufanya maandalizi katika kampuni ambayo unataka kuwa nayo hata kama bado hauna hiyo kampuni na sio unasema kwamba nasubiri kuwa na kampuni ndipo nianze kufanya maandalizi,jenga picha ya kampuni akilini mwako na jione kama kiongozi wa kuwafanya wafanyakazi wako kufanya kazi,jioni katika picha ya akili mwako unasaidia wafanyakazi wako kufanya kazi kwa ufasaha.

Kama utakuwa unanifuatilia vizuri ni sisi wenyewe ambao huwa na makosa pindi tunapokuwa na kampuni hata kwa watu ambao tayari wanakampuni pia wanafanya kosa kubwa kama hili la wao wenyewe kuwa wakosaji.Kwanini nasema hivi? Ukiwa na kampuni sio kufanya wenzako kuwa watumwa,lakini sisi huwa tunataka wafanyakazi wetu kuwa watumwa kwetuu kwa kudhani kwamba ndipo matokeo mazuri yanapopatikana,hii haitakufanya kuwa na matokeo mazuri na wala hauwezi kujenga picha nzuri ya biashara njee na maeneo mengine.Mfanyakazi ambaye yupo katika kampuni yako anahitaji wewe umwoneshe kwamba na yeye ni moja ya sehemu ya kampuni yako,yani kiongozi jitahidi kuhamasisha wafanyakazi wako,kuwa na lugha nzuri kwao,jitahidi muda mwingine kuwatembelea majumbani kwao,kwa makampuni ambayo yanawatu wengi hauwezi kufanya vile lakini kwa jinsi unavoishi na mmojammoja ndivyo wengine watakavyokujua,wape zawadi kwa kazi nzuri ambazo wanafanya, muda mwingine unaweza kutoka nao na ukajumuika nao kwenda kutembea kiofisi kama mbuga za wanyama.

Tokeo la picha la quotes about a leader in an organization
Kama una kampuni tayari au unajiandaa kuwa na kampuni wewe kama kiongozi unatakiwa kuelewa kitu kimoja kwamba chochote kile ambacho unakihitaji kutoka kwa wafanyakazi wako itategemeana na wewe mwenyewe jinsi unavyoyafanya,kama unataka wafanyakazi wawahi kazini unatakiwa kuwahi wewe kiongozi,kama unataka wafanye kazi kwa bidii waoneshe jinsi ya kufanya kazi kwa ufasaha na sio kwa maneno tuu. 

Chukua Hizi "KUWA 3'Ms" Za Kuwa Kiongozi bora katika kampuni yako:

1. KUWA MFANO.

2.KUWA MFANO.

3.KUWA MFANO.

Tokeo la picha la quotes about a leader in an organization

Nikimaanisha kwamba kiongozi bora kwenye kampuni hakai tuu kwenye kiti na kupiga simu shughuli flani ifanyike au akae ofisini azunguke kupata upepo wa AIR CONDITION lakini anatoka na kuwa mfano kwa kila jambo na huyu ndiye kiongozi bora ambaye anaangalia kampuni kuwa na matokeo mazuri.

Asante Sana kwa Muda Wako,ulikuwa nami;

LAZARO SAMWEL 
Contacts; 0753616584 / 0653386586
Email     ; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment