Imedhaminiwa na kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA
Watu wengi sana huaribu siki zao asubuhi pindi wanapoamka bila wao kujua kwa kuzipa akili zao jumbe ambazo sio za afya kwa akili,yani kupatia akili asubihi habari ambazo sio za kujenga mfano kusikiliza miziki ambayo haina fundisho lolote au kusikiliza miziki yenye ujumbe mbaya na ambao haumnufaishi msikilizaji zaidi ya kuifanya akili yake kuwaza mambo mengine mabovu na ambayo hayatamsaidia katika maisha yake. Haujawahi kusikia kwamba kunawatu wwanasema kwamba siku yangu iliharibika toka asubuhi mana nilipata habari ambayo sio nzuri,au rafiki yako kangomana na mwenzake asubuhi tu alivyoamka na kila dakika analalamika siku yake sio nzuri? Hii yote ni kwasababu ya kujaza akili yako mambo ambayo ni hasi wakati akili inafanya kazi vizuri asubuhi,kwasababu akili huwa inaanza kufanya kazi vizuri au huwa active pale tuu unapoamka,kitu chochote ambacho utakiweka cha kwanza ndicho ambacho kwa siku nzima kinaweza kuzalisha mengine Sawa na chenyewe kilivyo yani ukianza na mambo ambayo ni hasi jua kwamba matokeo yake ni kwamba unaweza ukajikuta kwamba kwa siku unafanya mambo kwa hasi na matokeo hasi pia.Kuna vitu ambavyo vinaweza kukusaidia katika kuhakikisha kwamba unajenga siku yako na kuifanya iwe na mwonekano mzuri katika kila saa ambalo litakuwa linapita baada ya asubuhi. Yafuatayo ni mambo ya kufanya pindi unapoamka tuu.
1. Anza na sala kwanza kabla ya kukanyaga ardhi ya chumba chako,hii ni kuweka siku yako kwanza mikononi mwa Mungu na kumwambia kwamba ailinde na kukuongoza kwamba chochote kile ambacho utaanza kukifanya ukuu wake udhihirike.Sala ni muhimu sana asubuhi haijalishi kwamba wewe ni dini gani au kabila gani wote asubuhi lazima tumshukuru Mungu na tumuombe aibariki siku hiyo.Wengi husahau sana hili swala kama vile ilikuwa ni lazima yeye kuamka salama asubuhi hiyo au anaona kama majaribu yote ya siku ataweza kupambana nayo bila usaidizi wa Mungu kwake. Jitahidi kubariki siku yako kwa sala kila uamkapo.
2. Jijengee Tabia ya kusikiliza audios za kuhamasisha,au kusoma vitabu vya kukujenga akili kwa DAK 10 au 15 wakati wa asubuhi baada ya kusali na kumaliza au kwa wengine wanaweza kufanya meditation (Tafakari) au kusikiliza muziki ambao utafanya wao kuwaza mambo chanya katika maisha yao,unaweza sikiliza audio za Lazaro Samwel za POSITIVE MIND VIBE unaweza sikiliza audio za Les Brown,Zingo The Great, Unaweza sikiliza audio za Mchungaji Mitimingi,Mr Eric Shigongo,Mr Habel Samida,Coach Bassanga na wengine wengi ambao unawafahau na unajua kwamba watakufanya asubuhi yako kuanza vyema.Hii itakufanya kwanza akili yako ikae sawa na kuweka focus katika kufafanya mambo yenye mtizamo chanya.
3. Baada ya hatua ya 2 sasa unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba Unanyoosha viungo vyako vya mwili hii itakusaidia katika kuruhusu mzunguko wa damu kufanyika vizuri katika miili yetu na kujisikia vizuri zaidi.
4. Pia jitahidi kutafuta msemo mmoja ambao utakuwa unautumia ambao ukiamka tuu unausema kwa saut hii cha kwanza kunahali flani ya kujiamini utajijengea ndani yako kama kweli utaweza kutamka kwa kumaanisha na kujiamini mfano mimi huwa napenda sana kutumia sentens hii NAYAWEZA MAMBO YOTE KWA YEYE ANITIAE NGUVU.Unaambiwa kwamba kwanza kabisa maneno yananguvu sana katika akili zetu kumbuka hata Mungu mwenyewe aliumba kwa NENO tuu hata sisi akili zetu kwa neno tuu tunaweza ziamrisha kufanya mambo makubwa sana ndai ya masaa 24 kwa kutumia misemo ambayo tutakuwa tumechagua.
5. Cha Mwisho kabisa ambacho ni muhimu pia ni kuhakikisha unasalimia wanafamilia au rafiki abao unaishi nao kwa furaha hii pia inasaidia sana.
Naimani kunakitu ambacho umejifunza na umefunguka kuhusu asubuhi yako kuifanya kuwa vizuri zaidi.Ukifanyia kazi utakuwa shuhuda kwa wengine jinsi mambo yanavyobadilika.
Karibu Kujipatia KITABU cha NGUZO 3 ZA MAISHA Kwa 10,000/= na Ofa ya kitabu kingine cha Soft Copy.
Lazaro Samwel
Contact ; 0753616584 / 0653386586
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment