Habari mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel,naimani uko vizuri na unaendelea vizuri na majukumu yako ya kila siku.Mtandao huu wa Lazaro unakulenga wewe leo hii ambaye unasoma makala hii kuwa kama chanzo cha kukufanya kuamka pale ulipo na kusonga mbele bila kuangalia nyuma bali kuchukua mafunzo ya kwanini ulianguka na uyatumie kama njia ya mambo mengine kwenda vizuri zaidi.Lakini pia ningependa kukwambia watu matajiri na ambao wanapigania kubadilisha maisha yao siku zote hawapumziki kupata changamoto katika maisha yao,tena kadri wanavyozidi kupigana ndivyo hata ukubwa wa changaoto unazidi kuongezeka.Kwahiyo wewe leo hata kama hujapata vitu ambavyo unavitaka katika maisha yako licha ya kuwa na biashara kubwa au ndogo zenye changamoto kubwa haimaanishi kwamba hauwezi kufanikiwa.Ndugu yangu kama hata kuuza mandazi/vitumbua,kuuza karanga,kuuza barafu,kuuza barafu,kuuza ubuyu,kuuza nguo na biashara zingine ambazo wenzako wanaona hazifai ZIKAMATE KWA MOYO WOTE NA KWA USAHIHI SANA na KWAMBA KILA SIKU USICGOKE KUANGALIAJE UNAWEZAJE KUBORESHA BIASHARA.Tatizo ambalo sisi watanzania wengi huwa tunakosea ni kwamba tunadhani kwamba biashara ndogo haziitaji maarifa ila ni kubwa tu ambazo zinahitaji maarifa,acha hii tabia na wala usidharau biashara wakati unaweza kuifanya ikawa kubwa zaidi.Chukua muda wako jifunze zaidi jinsi ya kufanya jambo ambalo unalifanya ukiona kama haitoshi jitahidi kutafuta ushauri kwa washauri wa biashara na masoko.
Kitu ambacho utakose katika kubadili maisha yako ni kujiona hauna cha kuongeza zaidi juu ya mambo ambayo unafanya,Kumbuka kila wazo ambalo unaliwazia jambo lako litaleta matokeo sawa na mawazo yako,yani ukisema kwamba nitafanya biashara kama wengine wanavyofanya utaishia kuwa na maisha sawa na wale ambao unawaiga.Ukitaka maisha ya utofauti lazima uanze kuwa wa tofauti na wewe ulivyo kimazoea lakini bila kusahau kuwa tofauti na wengine,au kwa upande mwingine ukitaka kuleta kitu cha tofauti lazima uhakikishe unafanya kitu cha tofauti na wengine.Kila mmoja anajambo a tofauti katika kufanya jambo flani na mafanikio yako usitake yafanane kama ya wengine,ukiweka juhudi ya kutaka kufanikiwa kuwa kama mtu flani jua utakapoishia ni kuwa mtumwa wa huyo mtu ambae unamuiga au kuishia katika umasikini wa kujitakia.Anza kujijengea tabia ya kuwa kama unavyotaka kuwa katika maisha yako,usiwe na haraka ya kusema kwamba nataka kesho niwe nimeshafanikiwa bila hata kuchukua hatua thabiti na kwa hatua nzuri na bora,mafanikio ni jumla ya mafunzo madogomadogo ambayo mtu alipata na anaendelea kupata kupitia makosa ambayo alishawahi kuyafanya katika kujifunza na kujaribu.
Kumbuka kuwa utayari wa kushinda mechi hautakufanya wewe kushinda mechi ambayo unayo lakini maandalizi ya ushindi mapema kabla ya mechi ambayo unayo ndiyo yatakufanya ushinde.Yani kuwa na kiu ya mafanikio katika biashara yako au kitu chochote cha kukubadilisha maisha yako haitatosha kukufanya kufanikiwa katika biashara zako lakini kujiandaa kufanikiwa katika biashara zako au shughuli yoyote ambayo unayo au jambo ambalo umetambua kwamba litakusaidia kuweza kufanikiwa katika maisha yako na utayari yako ndicho chanzo kikubwa cha wewe kuweza kufanikiwa.Kujiandaa huku ni kuhakikisha kwanza unakuwa na nidhani na malengo yako lakini pia unajenga tabia ambayo itaenda kukufanya wewe kufanyia haki kusudi lako,
Ulikuwa nami Lazaro Samwel mtunzi na mwandishi wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA .Kwa ushauri au kubadilishana mawazo tunaweza wasiliana;
Contacts ; 0753616584 /0653386586
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment