![]() |
| WWW.LAZAROSAMWEL.COM |
SPONSORED BY NGUZO 3 ZA MAISHA
Habari mpenzi msomaji wa makala hizi la Lazaro Samwel naimani u mzima wa afya na bado tunazidi kukutana kwa mara ingine ukiwa umetenga muda wako kuweza kusoma makala hii ya kukubadilisha maisha yako pamoja kwapamoja na familia au jamii yako.Napenda kukwambia kwamba uko sehemu sahihi na unasoma kitu sahihi kukitumia katika maisha yako.
Ukiishi kwa ukawaida wa macho ya watu hautaweza kuona raha ya kuishi hapa duniani ukiishi kwa kutegemea pesa tuu hautaona thamani ya maisha yako zaidi utaona maisha yako yatakuwa pungufu katika thamani ya pesa na licha ya yote ukiishi kujisifu kwa wingi wa pesa ambazo unazo benki bado haujajua utu wa watu ni nini katika maisha yako,Ukiishi kwa kwa umaarufu na ukaweka mipaka ya kuishi na watu wengine kwa kuhofia umaarufu wako utapotezwa jua bado ndani yako hauna Mungu na wala haujajua nini maana ya maandikio ya Mungu vizuri,kwa wakristo naomba msome YOHANA 15;7 na kwa Waislamu naomba Pia naomba msome MANENO YA DHAHABU (78) moja wapo ya neno ambalo nimeweza kulishika na kulipenda ni USIMDHARAU YEYOTE HATA KAMA AKIWA DHAIFU AU MASIKINI. Tunaishi katika Dunia ambayo mtu akitimiza kusudi lake flani busara inapotea kama alivyokuwa mwanzoni alipokuwa anatafuta kusudi lake na anajiweka mbali na watu ambao wanaweza kuhitajia kusudi lake na wao waweze kutambua kilichopo ndani yao.Kitu kimoja kwa maisha ya namna ambacho kimepotezwa na kinazidi kupotezwa ni FURAHA,kwa maana Furaha ya kweli ambayo haitoki kwenye pesa,magari,nyumba, n.k Furaha ya kweli inatokana na jinsi unavyoweka watu wengine kuwa na Furaha ambayo unayo na unaona kweli inapaswa kuwa hivyo,pesa haiwezi kueleza thamani ya furaha yako ukifa,Gari pia haliwezi kuweka historia ya Furaha yako ilivyokuwa bali ukiweka Furaha usoni pa watu thamani na historia ya Furaha yako itajulikana na itaelezwa na vizazi kwa vizazi na wataiandika kila kona ya miji na hata majumbani kwao watabandika picha yako wakisema huyu ndiye aliyetufundisha maana ya FURAHA katika mji huu.
Kuna watu leo wanaweza kuonekana kama hawana akili na wanaonekana masikini mbele ya macho yetu lakini kiuhalisia hakuna mtu masikini na hili ni kama kufanya kosa kusema kwamba mtu flani ni masikini,sawa najua utakuwa unajiuliza huyu Lazaro Samwel anaongea nini leo? Lakini nataka kukwambia kitu kimoja kwamba hata uumbaji wa dunia haukuumbwa kwa uchoyo na dharau ya kutenganisha mtu mmoja baina ya mwingine,ukiangalia kwa undani ni kwasababu ya kukosa maarifa kwamba kugundua mtu flani kuwa katika hali flani ni wajibu wako wa kuweza kuangalia kwamba unawezaji kumsaidia huyo mtu kutoka katika hali flani ya kimaisha kwenda sehemu ingine nzuri zaidi.Maswali ya KAMA
- Kama kweli tunaamini kwamba kila mmoja ameumbwa na kusudi la kutimiza kitu flani duniani tena kizuri na kikubwa kwanini leo hii unakubali wenzako kuwa masikini kwa kukosa maarifa?
- Kama kweli tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na unaamini kwamba Mungu wetu ni wahuruma na anatupenda kwanini wewe leo unakuwa na chuki na watu flani baada ya kufanikiwa?
- Kama kweli unaamini kwamba hakuna mafanikio ambayo yanakosa muunganiko baina yako na watu wa chini kwanini leo unadharau maisha ya watu ambao wako chini badala na wao kuweza kuwainua?
"Kama hakuna mtu aliyeletwa Duniani kimakosa basi wengine wakishindwa kujua hilo sisi na wengine ndio wa kuweza kuwasaidia kujua kwamba hawapo duniani kimakosa na kuona kwamba watu wengine kufanikiwa sio kwamba hawawezi kufanikiwa,inabidi wajue kwamba kila wanachokiona kwa watu wengine na kuona kwamba hawawezi kukifikia wanaweza kukifikia na kuwa hata zaidi ya hapo" - LAZARO SAMWEL
Peke Yangu siwezi kusalimu watu wote naimani kwa wewe ambae umepata ujumbe huu unaweza kushirikisha na wengine na wao waweze kujiona kama wapya katika maisha yao na kubadilisha jamii zao au familia zao pia.Nia yangu ni kusalimia kila mtanzania kwa nia ya kuwajuza kwamba Upendo ndicho chanzo cha kila kitu katika maisha yetu lakini haswa ni kukusalimia kwa kukubadilisha Fikra kwanza ili Uwezo na Tafsiri nzuri ya Upendo unaoleta Furaha ya kweli.
Ulikuwa nami;
Lazaro Samwel kwa mawasiliano,ushauri au kubadilishana mawazo tunaweza wasiliana kwa namba hizi 0753616584 / 0653386586 au Email ; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:
Post a Comment