Friday, May 5, 2017

JENGA BIASHARA YAKO NA WATEJA WAKO



Picha inayohusiana       
 Habari  mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel nazidi kukwambia kwamba ni wewe ni wa pekee sana kwa kuchukua muda huu kuweza kusoma makala hii nikiwa na imani ufuatiliaji wako hautaweza kuondoka bure mwaka huu bila kusimamisha kitu chako chochote na kuja kutoa ushuhuda kwa wengine ulipofika. Kumbuka wewe ni wapekee sana.Katika kuelimisha jamii zetu huwa nakutana na watu wengi sana ambao wananiuliza maswali kutokana na mambo ambayo wanayo ndani yao haswa kutokana na biashara ambazo wanafanya.Swali kubwa ambalo huwa nalipata ni nitapata wapi soko la bidhaa ambao ninayo au kwa huduma ambayo ninayo?katika swali kama hili huwa kunamambo ambayo huwa yanakuwa dalili kwa mtu kukosa soko, cha kwanza kabisa ni kwamba inawezekana huyu mtu ambaye amekosa soko alikosea hatua za mwanzo katika kuanzisha biashara yake lakini pia alikosa maarifa juu ya uendeshaji wa biashara yake pale alipoanza biashara yake mfanonKutokuwa na maarifa juu ya uuzaji wa bidhaa ambayo anayo kwa  kujiwekea malengio na kuanza kuyafanyia kazi.Na wewe jaribu kujitafakari kwamba soko lako ulikosa kwa kitu gani, je ni kwamba ulichukua hatua ambazo sio sahihi katika kuanza biashara yako? au ulikosa maarifa juu ya uendeshaji wa biashara yako mwanzoni?  Nitaanza kuelezea jambo moja muhimu sana ambalo nimelitaja na kama utakuwa makini katika kusoma na kuchukulia hatua naimani hapa baada ya muda tunaweza kuongea mengine.
 KUCHUKUA HATUA AMBAZO SIO SAHIHI KATIKA KUANZA BIASHARA YAKO?

Watu wengi wanadhani kwamba kuanza biashara ni kuwa na kipato tu na kuweza kuanza kitu  ambacho unakitaka na kupata pesa,HAPANA,biashara ni wateja na wateja hauwezi kuwapata kwa siku moja,hili naomba uweke akilini.Lakini pia hatua za mwanzo katika kuanza biashara yako ndiyo ambayo itakufanya kuweza kutengenza wateja wengi kadri unavyotaka.Unaweza kuuliza kivipi sasa? Cha kwanza kabisa katika kutengeneza soko ni lazima ujiulize kwamba unawapelekea watu kitu gani ambacho ulifanya uchunguzi na wakakwambia wanakihitaji au watakihitaji kama kitakuwepo? Yani namaanisha kwa upande mwingine kwamba ulifanya uchunguzi wa muda mrefu au muda mfupi kuweza kujua watu wa eneo flani wanahitaji nini au wanakubali nini?  Hii ni hatua muhimu sana kabla ya kuanza kufanya biashara.Hakikisha kwamba unavodadisi kwa kuwapa  watu maswali tofauti na kukujibu kwa  kuandika au kwa maneno na kutembelea sokoni  na kuongea na watu ambao wanafanya biashara ambayo ni mbadala au ni sawa na biashara unayofanya  unatengeneza nao uhusiano mzuri nao haswa wale watu ambao huwajui kwa kuchukua na namba zao, hata wale ambao wanauza kitu mbadala na chako ambacho unataka kuleta sokoni mana hawa ndio ambao watakusaidia kutengeneza wateja.Jitahidi pia kusoma vitabu na magazeti kujua watu wengine wanasema nini kuhusu biashara ambayo unataka kufanya. Wanateja wanapenda biashara ambayo imejitosheleza ,na kama ulikuwa hujui  ni kwamba wateja wanapenda kujua sana kwamba wewe utawapa nini kabla ya wewe kuhitaji kitu kutoka kwao tofauti na hapo utabaki na bidhaaa zako kama za matumizi nyumbani kwako lakini kumbe sio. Waingereza wanasema kwamba ni YOU MUST DO SOME MARKET RESEARCH TO PUT YOUR BUSINESS IN A GOOD POSITION AGAINST RIVALS.

Katika hatua za mwanzoni katika kuanza biashara kwa mtu yoyote ni lazima uwe na 4  “W ” ?              
1.What to Produce?       Utazalisha Nini?  Jua Kitu ambacho wateja wako wanataka.(Ubora ni kitu cha Muhimu sana kuonesha utofauti wako na wengine)



2.Who To Produce?       Utazalishia Wakina Nani? Jua sifa za wateja wako.(customer Profile)


3.When To Produce?     Ni Muda Gani Wa Kuzalisha? Jua Muda mwafaka ambao unatakiwa kuanza biashara yako.

 4.Where To Produce?    Wapi Pa Kuzalishia? Jua Eneo Sahihi Kufanyia Biashara Yako
Kuwa na bidhaa haiwezi kukufanya wewe kuwa na wateja lakini bidhaa yenye ubora ambao wateja wanataka kutokana na uchunguzi mdogo ulioufanya ndicho chanzo cha wateja katika biashara yako – Lazaro Samwel

Picha inayohusianaMAMBO  3 YAKUJUA KWA MTEJA WAKO ILI KUONGEZA WATEJA WENGINE

Ø  Mteja huwa haji kununua bidhaa yako tuu lakini pia ananunua na tabia yako kuelezea wengine.

Ø  Mteja haumuuzi bidhaa BORA tuu hata Ubora wa tabia yako ikiambatana na huduma yako pia unauza mfano kuwasiliana nae kwa unyenyekevu na kumweshimu hata kama anakauli mbaya au anamaisha ya namna gani.

Ø  Mteja kwako hatarudi kwasababu ya  wewe tuu  kuwa na biashara lakini atarudi kwa ubora wa bidhaa zako,mazingira yako kuwa safi pamoja na huduma  yako nzuri ambayo imeambatana na tabia nzuri ambayo unonesha kwao.

"Jua Mteja MMOJA ambaye anakuja kwako sio kwamba yuko peke yake kweli hapana lakini kunawengine zaidi ya 100 ambao anaonyuma yake na wewe ukiweza kumnasa mmoja jua kunawengine ambao utaongeza katika biashara yako" - Lazaro Samwel

MAMBO MENGINE 4 AMBAYO UNATAKIWA KUJUA ILI UONGEZE WATEJA WAKO (4 P's)

1. Products (Bidhaa) - Angalia kuweka kitu sokoni ambacho kitakuwa kitambulisho chako na ambacho mtu akiona ajue anachukua kitu cha mtu gani pia mfano mzuri angalia kampuni kama APPLE,SUMSANG wanachokifanya wamanembo na bidhaa ambazo zinalenga matakwa ya wateja wao.

2.Place (Mahali)- Angalia mazingira ambayo yatamfanya mteja wako kupata huduma nzuri au sehemu ambvayo mteja wako anaweza kupata bidhaa kwa urahisi zaidi.

3. Promotion (Kujitangaza) - Unawawekaje wateja wako karibu katika kuwajuza huduma au bidhaa ambazoi unazo? unatakiwa uhakikishe kwamba wateja wako wanapata taarifa juu ya huduma ambayio unayo au huduma mpya.Tumia mitandao lakini pia hakikisha muda mwingine i biashara ya kuuza utoke na uzungumze na watu kuhusu unachokifanya.
4.Price (Bei Za Bidhaa) - Hakikisha kwamba unaweka kiwango cha bei ambacho kitalenga wahusika lakini pia kisizidi washindani wako ambao wanabidhaa mbadala na zako yani hakikisha kwamba hauendi kinyume na hali ya maisha ya watu ambao umeenda kuweka biashara yako. Asante Sana kwa kuwa Pamoja nami, ulikuwa nami;

LAZARO SAMWEL mtunzi na mwandishi wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA.
 Kwa Ushauri,Kubadilishana Mawazo Zaidi AU Kupata kitabu changu tuwasiliane kupitia ;        
                                                                                                                              
      CONTACTS ; 0753616584 / 0653386586
     EMAIL          ; lazarosamweli41@gmail.com





0 comments:

Post a Comment