Monday, May 8, 2017

MAARIFA KUHUSU WAZO LA BIASHARA


Tokeo la picha la quotes about having business ideas
Habari mpenzi msomaji wa makala hizin za Lazaro Samwel nikiwa na iamn kwamba unaendelea vizuri na majukumu lakini pia ukiwa katika sala za kuombea wadogo zetu waliopoteza maisha katika ajali iliyotokea maeneo ya Arusha wiki iliyopita.Licha ya hayo pia najua uko katika harakati za kuendelea kujenga taifa lako kwamba unahakikisha kwamba unajenga msingi imara wa maono yako katika kusudi lako. Kwa yaliyotokea ni funzo tosha kwamba uwepo wako hapa kwa upendeleo wa Mungu ni kwamba kunajambo ambalo unatakiwa kulitimiza na sio kukaa na kuwa mtu wa kulalamika kila siku bila kuamka na kujaribu kila njia kuhakikisha kwamba unajiweka katika sehemu ambayo itakufanya kufikia kusudi lako.Acha kulalamika na anza kuangalia unawezaje kusonga mbele na sio utaendeleaje kulalamika mana hiyo haitakuwa suluhisho la tatizo ambalo unalo lakini utakuwa unaongeza uzito wa kitu ambacho unalalamikia wakati hata haujajaribu chochote.

Leo hii nimeweza kuja kukueleza kuhusu wazo la biashara, ikae akilini mwako ni kwamba nataka kukufanya kuweza kuwa na wazo na sio kukupa wazo la biashara mana nachoamini ni kwamba ukitaka kmsaidia mtu usimpe samaki na usimfundishe jinsi ya kuvua samaki tuu laini hakikisha kwamba unamfundisha jinsi ya kumiliki bwawa au ziwa la samaki ili kila siku awe na uhuru wa kuvua samaki kwa kiwango ambacho anataka na kufanya mambo mengine akiwa na uhakika wa kuwa na samaki wakati wowote.Navyo sema kumfundisha kuwa na bwawa la samaki ni kumfundisha jinsi ya kutumia akili yake kuona biashara na pia ajue jinsi ya kufikirisha akili yake kuona mambo kitofauti zaidi.
Wewe kukosa wazo la biashara inaweza kuwa kwasababu unawaza kwamba wazo la biashara lazima liendane na watu wengine lakini kumbe hapana,Naomba nikwambie kwamba wazo la biashara linaanza kwa kuangaali changamoto za watu ambao wanakuzunguka kabla hata ya kutengeneza wazo lenyewe,namaanisha kwamba kabla ya kuona changamoto za watu kwanza hauwezi kuona biashara ambayo unataka kufanya kabisaa.Wewe ukiona unakosa wazo la biashara jaribu kujiuliza ni mara ngapi ulikaa na ukaanza kujiuliza kuhusu changamoto ambazo zinawakumba watu ambao wanakuzunguka au watu wa sehemu flani? ukiona kwamba hakuna muda ambao ulishawahi kutenga kujiuliza haya mambo jua kwamba ndicho chanzo haswa ambacho kinakufanya wewe mpaka leo unakosa  wazo la biashara.Kwasababu wazo lolote la biashara limelenga kuongeza thamani kwa watu na sio wewe kupata sifa kwamba unabiashara na wakati huo biashara imelenga matakwa yako tu na furaha ya marafiki zako.Usitafute watu kwaajili ya wazo la biashara yako lakini tafuta wazo la biashara kwaajili ya watu na hautakuja kulalamika kabisa kwamba biashara hailipi au biashara mbovu,(nyongeza) nakumbuka kipindi nimemaliza form 4 nikiwa nyumbani katika biashara ya duka ya wazazi wangu kitu ambacho nilikuwa nikisaidia wazazi wangu ilikuwa ni kuandika bidhaa ambazo watu wengi wameulizia na wakaikosa alafu sasa ndo inakuwa oda ya mzigo mpya katika biashara ya duka,hii kwanza inakusaidia bidhaa haitakaa kwa muda dukani na pia utapata faida mapema,lakini kama ingekuwa kwamba unaleta tuu mzigo kwa mawazo yako tuu na kuongeza kwenye duka unawez kila baada ya mwezi ni kutoa vumbi kwenye bidhaa.
Kwa nyongeze ingine pia unaweza kupata wazo la biashara kupitia changamoto ambazo wafanyabiashara wengine wanapitia yani unazalisha wazo la biashara kupitia biashara za watu wengine kwamba unatumia changamoto zao katika biashara zao za kuweza kuleta utatuzi kwa baadhi ya changamoto na wewe ndo unazichukua na kutengenza kitu.

Ukishafanya hivi sasa kumbuka kwamba kunakupata wazo la biashara na kuchukua hatua kwa wazo lako la biashara  kuweza kukamilika.Wazo la biashara sio wazo mpaka ulichukulie hatua kwanza hapo ndipo tunaweza kusema kwamba hili ndilo wao la biashara. Yani kunakitu kama hichi;

1.ANGALIA CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA YAKO.
Tokeo la picha la quotes about seen challanges as business ideas
Hapa ndipo unaweza kupata wazo la biashara kwahiyo usikimbilie kutafuta wazo kwa watu alafu unaacha pia kuangalia sehemu ambayo unaishi kwanza,utakimbia sana alafu kumbe wazo unaweza kulipata hapohapo unapoishi tuu.Mfano maeneo ambayo unaishi kuna watu ambao wanakosa watu wa kufanya usafi majumbani mwao,sasa hapo angalia naweza ikawa fursa pia kwako,inaweza ikawa kwamba sehemu ambayo unaishi wanashida na mashine ya kusagia hiyo inaweza kuwa wazo la biashara,unaweza kukuta kwamba unapoishi kuna shule ambazo wazazi wanalalamika kwamba walimu hawafundishi vizuri na wewe ni mwanafunzi kutoka chuo hauna ajira hilo pia ni wazo la biashara,unaweza kukuta pia sehemu ambayo unaishi watu wanashida ya vitafunwa hii ni fursa, n.k

2.WEKA MIPANGO KUTENGENEZA WAZO LAKO.
Tokeo la picha la quotes about having plans business ideas
Hapa sasa baada ya kuona tatizo flani unaweza anaza kujiuliza unafanya nini,ukiona kama peke yako mambo yanaweza yasiende angalia watu ambao unawaamini au kama ni marafiki unaweza kuungana nao na mkajiuliza tunafanya nini fursa hapa ipo na ni hii hapa?  sasa huku ndipo mnaweza kuweka mipango kama ni kutumia hela yenu kidogo mfukoni kuanza,kuomba mchango kwa watu ambao ni waelewa au hata kuandika pendekezo benki kuomba mkopo kama kikundi pia.Kumbuka angalia na marafiki ambao unachagua kuwashirikisha wazo lako la biashara mana kuna wengine unaweza kuwashirikisha na wakaona hela na sio kulifanyia kazi wazo liwe na matokeo mazuri ndipo mpate hela.

3.KUANZA KUCHUKUA HATUA.
Tokeo la picha la quotes about having business ideas
Hapa sasa ni baada ya hatua ya kwanza na ya pili inahitaji kujitoa na kuhakikisha kwamba wazo ambalo mnalo linaleta matokeo mazuri na kumbuka mwanzo utakuwa mgumu ndio maana nimekwambia ni lazima kuangalia watu ambao sahihi na hawangalii kupata hela mwanzoni mana mkianza kufanyia kazi wazo lenu la biashara na msione matokeo mazuri kifedha wanaweza kuwakimbia kabisaa lakini ukipata watu ambao wanaona pesa baada ya matokeo mazuri lazima maisha yenu yatabadilika tuu baada ya muda.

Huu ujumbe sio wako peke yako share na wengine pia waweze kufunguka.

SOMA;KWANINI UNATAKIWA KUSOMA KITABU CHA NGUZO 3 ZA MAISHA

Naomba kuishia hapa lakini kama utakuwa na maswali au unataka kubadilishana mawazo nami naomba tuwasiliane kupitia namba hizi;

LAZARO SAMWEL 
CONTACTS ; 0753616584 / 0653386586
EMAIL         ; lazarosamweli42@gmail.com

0 comments:

Post a Comment