Monday, May 8, 2017

TUFUNGUE MAISHA KWA NAMBA ZINGINE




Habari mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel nikimini kwamba u mzima wa afya na unaendelea vizuri na majukumu yako ya kila siku.Makala hii ni kwaajili yako na sio kwaajili ya mtu mwingine mana kuchukua muda wako kuweza kusoma kitu kama hichi inamaana kunathamani flani ambayo unaitafuta au unataka kuiongeza kufika sehemu ingine tofauti na mara ya kwanza.
 Tokeo la picha la quotes about challenges of life

Nikwambie kitu kimoja mpenzi msomaji kwamba hatutaweza kuuondoa umasikini kwa njee ya mtu bila kuhakikisha kwamba  katika akili sehemu ambayo mawazo ya kimasikini yameshikilia tunayatoa na kuweka mbali na akili zetu.  Ni kama ukitaka  kuondoa magugu katika shamba lako sio kuyakata na ukayaacha na mizizi na mashina yake  na ukategemea yasiote, yataota tuu, dawa yake ni kungoa majani yote na kuhakikisha kwamba unachoma moto na sio kuyaacha pembeni mana mengine huota tena.Hapa namaanisha hakikisha kwamba katika akilinyako ukiamua kuondokana na fikra za kimasikini usiache chembe hata kama bado uko katika hali tete jione uko pale unapotaka kuwa hata kama bado hujafika jisemeshe ukwli kwamba haukuumbwa kuridhika na kukubaliana na hali ambayo unayo sasahivi.Unapojiweka karibu na mawazo ya umasikini na hali duni ndivyo kweli utakavyokuwa unajiweka katika mazingira ya kuwa kabisaa masikini,badilisha mawazo yako ipe akilinyako haki yake na lipe kusudi lako nafasi yake, usione kikwazo kama ndo m stand ya kuwa masikini, usione majaribu ya leo kuwa kama sababu za wewe kuendelea kuwa katika sehemu ya maisha ambayo kila siku unaumia na unakosa mambo ambayo unatamani kuwa nayo. Wewe na akilinyako ni kula kitu na kila kitu ambacho unaona unavho au maisha ambayo unaishi ni maamuzi yako ya tafsiri ya kila hali ambayo umepitia katika maisha yako. Hakuna chochote chenye madhara katika maisha yako bila idhini yako na hakuna kitu ambacho kinaweza kuadhiri maisha yako bila ruksa yako ya kwamba kiniathiri au kisiniathiri mfano unachosikia kwa watu bila wewe kukiruhusu kwa tafsiri yake ambayo unaijua hakiwezi kukudhuru ila ukishakiruhusu kuingia katika akili yako kwa tafsiri yake basi uwe tayari kupata madhara ya maana ya hilo au hayo maneno.

Imekuwa ni mara nyingi sana nikiweka msisitizo wa hili swala mana najua kwa asilimia kubwa huwa linatutokea kwa kukabidhi maisha yetu kwa watu wengine ambao  wao mambo ambao ni kipao mbele kutafsiri kwa haraka ni mambo ambayo yanamchango mbaya kwa binadamu au kwawenzao hawastahili kabisa, kwanini nasema hivi? Kuna watu katika maisha yako hawapo kwaajili ya kukujenga ila kwaajili ya kuhakikisha kwamba unakuwa chini ikiwezekana hata zaidi ya uafadhali ambao wanao wao. Na hawa watu huwa na tabia ya kutafuta  tafsiri ya maneno ambayo ni hasi bila hata kutafakari kama ni muhimu au sio muhimu kujua maana yake na madhara ya maana yake kama mtu atakuwa nayo.Naomba nikukumbushe kitu kwamba kila mmoja anaweza kuwa jamaa yako lakini sio kila mmoja anaweza kuwa rafiki yako, kwanini nakwambia hivi? Ni kwasababu sio kila mmoja atataka kukuona kwa tafsiri nzuri ya kutaka kukuona mbali lakini kunawengine wanakuona kwa tafsiri ya kutaka kukuona kuwa mbali sana kwa nyuma yaani uwe chini zaidi ya kawaida.

Hali hii ya maisha hauwezi kuiondoa kwa kuwaambia watu sikutaki au sitaki mambo ambayo unanifanyia, lakini kumbuka ni lazima ujue na wewe tafsiri ya maisha yako ni nini kama tafsiri ya maisha yako ni mafanikio kusaidia watu, au ni mafanikio ya kubadilisha maisha ya watu wengine inabidi sasa uishi katika tafsiri hiyo lakini ijengee misimano ya kusimama na kuonesha kwanba hakuna ambaye anaweza kukutoa njee ya mstari, hii itakusaidia kuvuta watu ambao ni sahihi katika maisha yako na wale ambao sio sahihi  na misimano yako wataondoka wenyewe bila hata kuambiwa. Naimani mimi na wewe ni tafsiri ya mafanikio tena haswa mafanikio ambayo yanazalisha mafanikio kwa watu wengine. Kumbuka hizi ni salamu zangu kwako na najua kunawatu ambao unajua wakipata salamu hizi utakuwa umewaokoa,sasa naomba ushare nao ujumbe huu ili uweze kuwafikia salama.

SOMA;KWANINI UNATAKIWA KUSOMA KITABU CHA NGUZO 3 ZA MAISHA

Ulikuwa nami ;

LAZARO SAMWEL mtunzi na mwandishi wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA.
CONTACTS : 0753616584 / 0653386586
EMAIL        ;  lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment