
Habari mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel nikiwa na imani lengo lako kwa mwaka huu ni kuweza kuhakikisha kwamba unabadilisha maisha yako ya mwaka huu tofauti na miaka mingine ambayo imepita katika maisha yako,na naamini kwamba uko sehemu sahihi katika kuhakikisha kwamba unabadilisha fikra zako kutokana na sehemu ambayo upo kuhakikisha kwamba unatoka sehemu moja kufika ingine ambayo ulidhani kwamba hauwezi kufika.TWENDE PAMOJA
Kunadhana ambazo watu wengi walio katika ajira wamekuwa wakiwa nayo na wanadhani kwamba hayo mawazo ni kweli mfano hauwezi kufanikiwa ukiwa umeajiriwa,mshahara hauwezi kukutosha kufanya mambo mengi ukiwa umeajiriwa, napenda kukwambia kitu kimoja leo na ambacho naamini kwamba hawa ambao kila siku wamekuwa wanakwambia kwamba hauwezi kufanikiwa hawajawahi kukwambia,mojawapo ni kwamba hawajawahi kukwambia kwamba UNAWEZAJE KUFANIKIWA KWA KIWANGO KIDOGO CHA PESA AMBACHO UNAKIPATA au hawajakwambia NAFASI AMBAYO UNAYO KATIKA AJIRA UNAWEZAJE KUITUMIA KUFANIKIWA? Licha ya kukwambia hili lakini pia napenda kukwambia kwamba hata mimi nimetoka katika familia ambayo wazazi wangu walikuwa katika dimbwi la ajira na nimeona maisha ambayo walikuwa wanaishi na nimeona pia ni kwasababu gani kwa kipindi kile hawakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kujitoa kiurahisi kujiajiri na kuweza kubadilisha maisha yao tofauti na kusubiri hela ya pensheni baada ya kustafu.
.Sasa katika kukutoa katika visingizio vya kuwa katika ajira nitapenda kukushirikisha mambo ambayo kama utazingatia au kuweza kuviondoa katika akili yako wewe kama muajiri unaweza kusogea sehemu flani katika maisha yako;
1.Acha na tabia ya kuchukia ajira na kupenda mshahara tuu.
Nilishawahi kusema kwamba ukitaka kutoka katika kazi ambazo unaichukia sio kuchukia kazi ambayo unaifanya mana hautaweza kupata njia sahihi ya kutoka zaidi utazidi kujifunga ndani ya hiyo kazi.Ni sawa na waajiriwa kamba ukitaka kufanikiwa kwa kupitia ajira yao ipende kwanza kazi ambayo unaifanya lakini licha ya kuipenda sio lazima iwe ya kwanza lakini weka kitu unachokipenda zaidi kiwe juu a ajira yako alafu hakikisha kwamba kupitia ajira yako kipato ambacho utakuwa unakipata unasaidia kukuza kitu ambacho unakipenda njee ya ajira,Najua utakuwa na wazo kwa muda gani nitakuwa naweka kuweza kulifanyia kazi hilo jambo la kwanza? Endelea kuwa nami.
2.Baada ya kutoka kazini hakikisha kwamba unakuwa na muda wa ziada katika jambo lako la kwanza kulifanyia kazi.
Najua ukiwa umetoka kazini na umekuwa umechoka na unakuwa kama huwezi kufanya kazi lakini kwa kuwa unataka vitu vizuri na unapenda siku moja uwe huru hii ndo inaitwa kulipa gharama kuhakikisha kwamba kitu ambacho unakipenda kinafanikiwa.Unaweza kupumzika kwa muda mchache ukiamka unafanya shughuli zako muhimu kama ni familia pia unahakikisha kwamba unafanya yale mambo mihimu kwanza alafu ukimaliza hakikisa kwamba unakuwa na muda ambao utautumia bila makosa kufabya lile jambo lako kuzidi kulisogeza mbele zaidi na zaidi.
3.Tafuta maarifa na sio kusema kwamba huna muda.
Waajiriwa wengi huwa na visingizio vya kusema kwamba sina muda wa kusoma vitabu lakini ukiangalia katika ratiba za kazini kunakuwa na muda wa ziada kupumzika mfano mwalimu au mfanyakazi yoyote sidhani kama hauna muda wa kupumzika kama huna hebu jaribu kujiuliza ni muda gani ambao unatumia na wenzako ofisini kuongea vitu ambavyo haviwahusu au kujadili siasa au kujadilia maisha ya watu wengine ambayo hayawahusu? najua utakuta kwamba kunamuda mwingi sana ambao unapoteza lakini kumbe ungeweza kuwa unatembea na kitabu chako kwenye mkoba wako wa kazini au kuwa na kitabu katika begi lako la kazini ili kwa muda ambao ulikuwa unafanya mambo ambayo sio ya muhimu ofisini unakisoma,usiogope wafanyakazi wenzako kukucheka kwasababu wewe ndiye ambaye unajua maisha yako yanatakiwa kuwa wapi zaidi ya kuwa ofisini.Maarifa yataweza kukusaidia kuweza kujua kuhusu matumizi ya kipato chako mfano katika kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA niliweza kuonesha jinsi mtu mwenye mshahara wa 400,000/= anaweza kuweka mpangilio wake wa pesa,sasa wewe muajiriwa kama haujaweza kukisoma unawezaje kujua haya mambo? Kuna mambo ya ASSET NA LIABILITY kama huwezi kuyajua kwaninio usione mshahara wako unapotea sehemu ambayo sio muhimu? kuna mambo kama ya GHARAMA na MATUMIZI kama huwezi kusoma vitabu utajuaje kuhusu matumizi muhimu na ambayo sio muhimu? utajuaje gharama za lazima na ambazo sio lazima? ni lazima ubadilike na uache kuwa sawa na marafiki zako kwasababu unaogopa kuchekwa au unaogopa kusemwa.
4.Jua ajira yako sio kila kitu.
Kuna watu ambao wako kwenye ajira lakini wameridhika na kuwa katika ajira hata kuweka akili zao kuwaza kuwa zaidi ya hapo inakuwa ni shida na wala hawataki kubadilika au kubadilisha maisha yao.Hapa unakuta kwamba huwezi kuweka akiba au kuwa na malengo mazuri kwamba hata kuja kufungua ajira.Muda mwingi hawa ambao unakuta wanaridhika na kuajiriwa pindi wanapokuja kustafu wanashindwa hata kujua jinsi ya kutumia hela yao ya kustafu mana sasa ukiridhika na kazi ambayo unayo hutataka kujua jinsi ya kutafuta maarifa au kutaka kuweka chanzo kingine cha kipato,ndo maana sasa mtu anakuwa na pressure na kupanic mana anakuwa na mawazo kwamba sasahivi sitakuwa napokea pesa sawa na nilivyokuwa nimeajiriwa lakini unakuta kwamba anakuwa na mawazo nitafanya nini na kiwango cha pesa nilichokuwa nacho maana hajawahi kukamata pesa kama zile toka azaliwe.Ukijua kwamba ajira sio kila kitu lazima utatafuta shughuli zingine za kufanya kupitia kipato cha mshahara wako ulivyokuwa kwenye ajira na ukatengeneza pesa nzuri,licha ya hivyo pia utaweza kuwa na maarifa ya jinsi ya kutumia pesa na kujiongoza mwenyewe mana lazima utaanza kutafuta maarifa ya mambo mengine pia.
Naomba kuishia hapa wewe unadhani ni mawazo gani ambayo muajiriwa anapaswa kuyaondoa ili aweze kufanikiwa zaidi ya ajira aliyokuwa nayo? comment chini tuweze kujifunza.
Ulikuwa nami;
LAZARO SAMWEL mtunzi na mwandishi wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA
CONTACTS ;0753616584 / 0653386586
EMAIL ; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment