Wednesday, April 26, 2017

UNAWEZAJE KUTOKA ULIPOFUNGWA KIAJIRA?


Picha inayohusiana

Habari mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel.Kwanza kabisa napenda kukupongeza kwa kuwa moja ya wafuatiliaji wazuri kabisa wa makala hizi toka zilipoanza mpaka sasa tulipofikia naimani makala hizi hazijakuacha kama zilivyokukuta lakini zimeweza kukutoa katika sehemu moja kwenda sehemu ingine ambayo ulikuwa unatamani na wengine zinazidi kuwasogeza karibu na mambo ambayo wanayataka katika  maisha yao.

Leo nimeanza kwa kukupa swali ambalo litakupa ufikirie lakini kwa kukusaidia zaidi ni kwaajili ya wewe ambaye umeajiriwa na ndani yako unajihisi kuwa sehemu ambayo sio sahihi.Kuna watu wengi sana ambao wamefungwa katika ajira lakini inakuwa ngumu sana kuweza kutoka katika vifungo hivyo kwasababu ya kuwa waoga wa kuweza kujifungua katika sehemu ambayo wanaona kabisa kwamba haiwapi amani na wala haiwapi kweli ya kesho,nakumbuka wakati nafanya field yangu ya mwaka wa pili kuhusu maswala ya manunuzi na ugavi maeneo flani ambayo sitapenda kutaja jina nilikutana na dada mmoja ambaye ni Afisa Ugavi na tulikuwa tukibadilishana mawazo kuhusu ufanyaji wa biashara haswa katika ufugaji wa kuku na akawa akaniambia "Lazaro unajua biashara ya kuku ambayo naifanya inanilipa mara 3 zaidi ya mshahara wangu ambao naupokea?" kwanza nilishangaa,alafu nikamuuliza kwamba "sasa kuku wako nani ambaye anawasimamia" akaniambia kwamba "kunawatu ambao nimewaajiri ndo wanasisimamia" sikuishia hapo nikamuuliza kwenye ufugaji wa kuku wako unatumia masaa mangapi kwa siku akasema "ni mawili tuu tena ninaporudi kutoka kazini" nikamuuliza "na kazini unatumia masaa mangapi kwa siku" akasema kwamba  "masaa 8 na muda mwingine mpaka  hata 10" . Sasa kitu ambacho kilikuja kunishangaza ni pale nilipomwambia kwamba kwanini usifanye ile kazi ambayo unatumia masaa 2 kwa siku na kukupa kipato kizuri zaidi ya unacholipwa lakini bado unakuwa na maamuzi yako binafsi katika uzalishaji na kula jasho lako kuliko ile ambayo unatumia masaa 8-10 lakini bado hausogei mbele na bado unaongozwa katika mfumo ambao lazima uufuate? akanijibu kwa ufupi kwamba "naogopa nitachekwa" yani kwa kifupi kwamba watu watamdharau kwa kutokuwa ofisini na kuonekana msomi kwasababu ameajiriwa.Tokeo la picha la picture of a sad employeeLengo langu ni nini katika kukupa kahadithi haka kafupi? cha kwanza kabisa ni kukujuza kwamba watu wengi huwa wanakuwa na uwoga wa kuweza kutoka sehemu ambayo wanaona kwamba wanapoelekea sio pazuri ikiwa kunasehemu nzuri tayari wameshajitengeneze.Fikiria huyu dada kwa ujana ambao anao na kwa kiwango cha Hela ambacho anasema kwamba anatengeneza licha ya kutumia masaa mawili (2) kutazama mradi wake angeamua sasa kuweka yale masaa yake nane (8) kwenye mradi wake je angetengeneza kiasi gani cha pesa? Ni kiwango kikubwa sana,lakini licha ya hivyo angekuwa na muda gani wa kuweza kutulia na familia yake na watoto wake? kweli angekuwa na muda wa kutosha sana tofauti na tunavyodhani.Kitu ambacho kinamwangamiza  ni kwamba anavumilia kitu ambacho anaona kwamba hakitakiwi kuvumiliwa kwasababu ya macho ya watu.

Nikwambie kitu mpenzi msomaji wa makala za Lazaro Samwel kwamba ajira sio mbaya ila wewe kuendelea kukaa kwenye ajira mpaka kujisahau kwamba na wewe unatakiwa kutengeneza ajira ndio shida,lakini pia kutokana na hali ya kitanzania inatubidi kwanza kuanza na ajira haswa kwa wale watu ambao tumetoka katika familia za chini kidogo ili tuweza kutengeneza mtaji japo ambao unaweza kutumika katika kutengeneza kitu cha kututoa kwenye ajira.Hili wengi huwa wanajisahau na wakipata mapato yao huwa wanadhani ni kwaajili ya kula na kuondoa jasho lakini hiko kiwango cha kwanza ni cha kumshukuru Mungu kwanza na kumwomba kwamba unapoenda kuiwekeza iweze kuleta njia nzuri ya kuweza kukutoa katika kuajiriwa na kujiajiri. Ajira yako inaweza kuwa mkombozi wako wa kuweza kukutoa ulipofungwa japo hapo penyewe umeshafungwa.Chukua hatua na hakikisha kweli unatumia nafasi hiyo nzuri kuweza kutimiza kusudi lako.

Naomba kuishia hapo. lakini kama utakuwa a uhitaji wakitabu changu cha NGUZO 3 ZA MAISHA ambacho naamini kama utakitia mikononi mwako hauwezi kubaki kama ulivyo katika nyanja kuu tatu yani Maendeleo Binafsi.Mahusiani Na Ujasiriamali/Biashara naomba tuwasiliane kupia ;

SMS/CALLS ;0753616584 / 0653386586
WHATSAPP ; 0653386586
EMAIL         ; lazarosamweli41@gmail.com

KARIBUNI SANA...

0 comments:

Post a Comment