Tuesday, April 25, 2017

KWANINI UNATAKIWA KUSOMA KITABU CHA NGUZO 3 ZA MAISHA

Kwa mara ya kwanza napata wazo la kuandika kitabu hiki cha NGUZO 3 ZA MAISHA i
ulikuwa ni wakati najiuliza maswali mengi sana baada ya kusoma vitabu vingi vya watu tofauti duniani,hii ilikuwa kama tabia yangu kila mwezi lazima niwe na kitabu kipya cha kusoma  baada ya kumaliza kingine.Lakini pia kulikuwa na maswali mengi ambayo yanakuja akilini kwamba nitaandika kitabu lakini sasa nitamuuzia nani kitabu hiki ambacho nataka kuandika ikiwa kila siku nasikia habari za watanzania wengi hawapendi kusoma vitabu? Hili lilikuwa ni moja kati ya maswali ambayo nilikuwa nikijiuliza mwenyewe kila nikiwa nawaza jinsi ya kuanza kuandika kitabu hiki cha NGUZO 3 ZA MAISHA,japo baada ya uchunguzi binafsi nikajikuta nasema mwenyewe  kwamba watanzania wapo wengi ambao wanahitaji kujua mambo mengi na mimi nitawafikishia tu.Pia kuna mambo ambayo ya msingi niliweza kujinenea mwenyewe baada ya kuona kwamba watanzania wapo ambao wanahitaji kusoma vitabu vizuri na inabidi nianze kuandika kitabu hichi,hayo maneno ni kama ifuatavyo, Lazaro kitabu hiki usiandike kwaajili ya kupata hela tuu,Lazaro kitabu hiki usiandike kwaajili ya wakristo tu,Lazaro kitabu hiki usiandike kuonesha u msomi,Lazaro kitabu hiki usiandike kwaajili ya watu maarufu tu,Lazaro kitabu hiki usiandike kwaajili ya wasomi tuu na watu wenye maisha mazuri tayari,Lazaro kitabu hiki usiandike kujitafutia umaarufu usio weza kubadilisha maisha ya watu n.k baada ya kusema maneno hayo na kuyawazia kwa uweza wa MUNGU ndipo nilipoanza kupata sasa nguvu ya kuandika kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA ambacho cha kwanza kabisa kinalenga  kumwinua mtu wa chini na kumweka katika usawa wa kuweza kuheshimiwa na mtu ambaye anajiona yuko juu (Yani kuleta usawa wa fikra kuona wote ni bora na kila mmoja anaweza kufanya jambo flani kama atasaidiwa) maana ilikuwa kiu yangu kubwa sana kwa kila mmoja ambaye anapata kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA,lakini pia hata wale ambao tayari wanajiona wako vizuri kimaisha wakikipata kitabu wajue kwamba walipofika ni kwasababu ya wale ambao wako chini yao na inabidi wawaheshimu na kuwasaidia na wao pia waweze kutumia walivyokuwa navyo,isiishie hapo ila pia kuwawazia wenzao  mema na kumweshimu katika nyanja ambazo mtu amaeamua kuwa.Kuna watu ambao wanaweza kuuliza kwanini ulikiita kitabu NGUZO 3 ZA MAISHA? Jibu ni kwamba katika maisha ambayo tunaishi niliweza kuona maeneo matatu muhimu sana ambayo kila mmoja anapaswa kuyaelewa katika maisha yake ili aweze kuishi vizuri nayo ni MAENDELEO BINAFSI,MAHUSIANO NA NDOA na UJASIRIAMALI NA BIASHARA.Na ndo maana kiu yangu  ilikuwa kuchanganya maarifa kutoka sehemu tofauti bila kujali kabila,dini na kabila ili kila mmoja aweze kupata tatuzi za changamoto ambazo mtu anakutana nazo katika NGUZO HIZI 3 hapo juu.Kwa kifupi kwenye kitabu NGUZO 3 hizi zimejikita katika mambo yafuatayo;

1.    NGUZO YA KWANZA

Maendeleo Binafsi: Katika nguzo hii nimeweza kulenga katika kubadilisha fikra zako kama mawazo yako yamejengeka kwa kujishusha thamani na kuona kwamba huna uwezo wa kuweza kutimiza mambo makubwa duniani. Katika kipengele hiki utajifunza jinsi thamani yako ilivyokubwa na namna unavyoweza kufanya mambo kwa uwezo ulioko ndani yako. Lakini pia, baada ya kumaliza kipengele hiki, utaweza kujibu maswali muhimu ambayo yamekuwa yakiwasumbua watu wengi, maswali hayo ni pamoja na wewe ni nani? Kusudi lako ni lipi? Kwanini unaishi? Nini maana ya Kujitambua na mafanikio yako? Nini Thamani Ya Kushukuru? na mengine mengi.


2.      NGUZO YA PILI

Mahusiano: Katika nguzo ya pili, ambayo inahusu mahusiano, utajifunza nafasi ya mahusino katika maisha na maendeleo yako. Hivyo kipengele hiki kinagusia kwa vijana na watu wazima katika ndoa zao. Ndani yake utapata maana ya upendo halisi na namna ya kupata mwenzi wa maisha yako. Pia utajifunza namna mahusiano na watu wengine yanavyoweza kukusaidia kuendelea au kukupoteza katika maisha yako ya mafanikio. Na mengine mengi ambayo naamini kwamba hauwezi kutoka kapa.



3.      NGUZO YA TATU

Ujasiriamali na Biashara: Nguzo ya tatu inahusu ujasiriamali na biashara kama shughuli muhimu ambazo watu wengi wanazitegemea katika kuendesha maisha yao. Katika kipengele hiki utajifunza mambo mengi yakiwemo; kuelewa ujasiriamali na biashara, kujua tofauti kati ya hizo shughuli mbili,kujua ni kwanini watu wengi hawafanikiwi katika biashara au ujasiriamali? Na mengineyo, ambayo ukisoma utaweza kufungua akili yako vizuri.

SHUHUDA ZA WATU WACHACHE WALIOSOMA KITABU CHA NGUZO 3 ZA MAISHA

1. " Kwakweli Mungu mwema nakushukuru sana kwa mambo mazuri ambayo yamo kwenye kitabu chako Mungu akubari sana akuongezee hekima na busara! Ufanye zaidi ya hapo🙏     Najifunza mengi sana!!Mr Kayanda kutoka  Ruvuma

2. "Ahsante sana mkuu nilivo kupokea tu nimesha pokea upako wa nguvu,Mwalimu i hope safari yangu ni salama salimini" Mr Irrynine kutoka  Songwe

3. "Nzuri kabisa. Kitabu Chako ni nondo. MTU akijengea nyumba inabaki imara kweli2.  Nimekipenda na Mungu akutie  nguvu na azidi  kukupa mafunuo ya kubadilisha maishà ya watu kutoka  kwenye mtazamo duni kuelekea mtazamo mpana".   Mr Fennias Mannaseh kutoka Arusha                     
4."Mambo vipi kiongoz kile kitabu Mwl wezangu wamekipenda na wameahidi mwisho wa mwezi watanunua vyakwao" Mwl.Seraphine kutoka Singida

Mpaka hapo naimani kunapicha ambayo imejengeka kuhusu vitu gani haswa ambavyo unaenda kuvipata katika kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA,nakukaribisha sana kuweza kupata nakala zako za kitabu hichi kwa 10,000/= tuu na utapata ofa ya kitabu kingine cha Soft Copy kama zawadi ambacho unaweza kikisoma hata ukiwa kwenye sehemu ambayo huwezi kutoa kitabu cha Hard Copy Cha NGUZO 3 ZA MAISHA.Kwa Mawasiliano zaidi juu ya upatikanaji wa kitabu maeneno yoyote Tanzania tuwasiliane kama ifuatavyo;

Sms/calls ; 0753616584 / 0653386586
Whatsapp; 0653386586
Email       ; lazarosamweli41@gmail.com

KARIBU SANA.

0 comments:

Post a Comment