Tuesday, May 9, 2017

KUNA MWANAUME KUPENDA MWANAMKE MMOJA NA SIO WANAWAKE??


Tokeo la picha la quotes about man having one woman or two

Napenda kukukaribisha katika mtandao huu wa Lazaro Samwel nikiamini kuwa  huku haujafanya makosa na uko sehemu sahihi katika kusoma makala hizi ambazo zinajikita kubadilisha historia ya kila mmoja bila kujadili aina yoyote ya maisha ambayo mtu anaishi au aina ya maisha ambayo mtu anayo.

Leo nitaenda kukushirikisha baadhi ya mambo na maswali ambayo nimeweza kukutana nayo katika mitandao na nikaona kwamba niweze kukumegea ili nawe uweze kupata kitu.Haswa swali ambalo nimeweza kupata ni kutokana na video moja ambayo imesambaa mtu akisema kwamba "hakuna mwanaume ameumbwa kupenda mwanamke mmoja,na ukikuta mwanaume wa namna hiyo jua anamatatizo au hayuko sawa" bila shaka naimani na wewe inawezekana katika pitapita zako umeweza kukutana na video hii,lakini nami nilikuwa na maono kutokana na huu moja ya mstari ambao nimeusikia katika video hiyo.Kwanza kabisa ningependa kusema kwamba hiyo video inaujumbe ambao sio wa kujitosheleza na unatafsiri ambayo sio sahihi kwa mwanaume.Mwanamme ameumbwa kupenda mwanamke mmoja zaidi ya hapo itakuwa ni kutamani ambako sasa wengine ndo tunasema kwamba ni kupenda na hapo ndo unakuata kwamba kunakudanganywa na  watu kuumia kwasababu unadhani mtu alikupenda kumbe alikutamani. Kwa wengine ambao wanasoma Biblia wanaweza kurejea katika kitabu cha Mwanzo katika Biblia na kujiuliza kwanini Mungu alimpa Adam mwanamke mmoja na hakuonesha kumpatia mwanamke mwingine? na hapo ndipo utaanza kupata kwamba mwanaume kamili sio lazima awe na wanawake zaidi ya mmoja,lakini pia kumbuka kwamba kila mwanamke ameumbwa kuwa msaidizi kwetu sisi wanaume na hauwezi kusema kwamba uchukue kila mwanamke hapo hata utaanza kutenegenza chuki baina ya wale wanawake mana lazima kunammoja ambaye unaweza kumwona wa maana kuliko mwingine,lakini pia licha ya hiyo mwanaume pia anatakiwa kuwa na mambo mawili katika akili yake yani MAARIFA (Knowledge) na KUJIONGOZA (Self Control) unapokosa hivi cha kwanza lazima kila unayemwona utaona kwamba unatakiwa kuwa naye haitajalisha kwamba nyuma umeacha wanawake wangapi.Kwanza kabisa unatakiwa kujua kwamba unapokosa kujiongoza(SELF CONTROL) kwanza unakosa umiliki wa roho yako lakini sasa utakuwa unaongozwa na mwili kutimiza matakwa ya hisia zako za kimwili na kushindwa kuwa na maarifa ya kuweza kujua kwamba ni sahihi unachokifanya au laa.Kutokuwa na mwanamke mmoja ni matokeo ya kuongozwa na mwili na sio roho na huko ndiko kuna uzao wa kutamani kitu ambacho sio chako na sio sahihi mana unakosa maarifa na kujiongoza na kuona kwamba tayari ninaye mwingine na huyu mwingine hapaswi kuchukua nafasi ya mwenzake.Ukisoma WARUMI 8;6-9 hii mistari inasema "Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti;bali nia ya roho ni uzima na amani. (7) Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu,wala haiwezi  kuitii. (8)Wale wafuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. (9)Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu,ninyi hamfuati mwili;balimwaifuata roho.Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo,huyo sio wake" pia unaweza soma MITHALI 4;23 "Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima"

Kwa mwanaume kujitambua ni kitu muhimu sana lakini ukijiachia wazi lazima utakuwa katika kundi la kutamani na sio kupenda kama tunavyodhani.Ukiacha nafasi katika mwili kukupeleka au kukuongoza kuna mambo mengi sana ambayo unaweza kufanya na yasifike mbali sana kwa kuwa kunakitu ambacho unakuwa umekosa katia yako na Mungu ambako sasa unatakuwa kuanza upya kuleta muunganiko ambao utakuja kukufanya kuonekana ni kicha katika familia na kuwa mtu wa kuheshimika na jamii yako.

NYONGEZA KWA WANAWAKE

Kwa wanawake Pia wanatakiwa kuhakikisha kwamba wanakuwa karibu sana na Mungu katika kusali  na kuwa na macho ya rohoni kuweza kuzitafakari hatua zao mana hauwezi kuvuta kitu ambacho wewe sio na baadae ukaja kulalamika kwamba wanaume woote wako sawa,sio hivyo itakuwa wewe ndo hauko sawa na ndo maana umevuta mtu ambaye amekuja kukuumiza kama ungeweza kujiweka katika mazingira ya mtu sahihi usingeweza kuumiwa lakini kwakuwa unakaribisha watu ambao ndio wewe ulivyo tegemea kupata matokea kama ambayo unayawazia.Licha ya kusikia kwamba mwanaume ndie anatakiwa kuwa kichwa katika familia, lakini ili uweze na wewe kupata ambaye ni kichwa hakikisha kwamba hauchezi mbali na tabia za mwanaume ambaye ni kichwa.usiseme kwamba Mungu atakusaidia tuu, atakusaidia kivipi kupata mwanaume ambaye unadhani atakuwa kichwa na wewe unajiweka kuwa  kama mkia ukiwa hauna hata chembe ya tabia ambazo zinamuunganiko na mwanaume kichwa ambaye unamuhitaji? Kuna usemi ambao pia unatumika kwamba "wanaume wote wako sawa" lakini kumbuka hili kwamba "kweli wanaume wote wako sawa lakini wanatofautiana kitabia".Badilisha mtizamo wako na kuwa kama unavyotaka kwa mwanaume ambaye unataka uwe nae katika maisha yako uone utavuta wa namna gani.

Tokeo la picha la quotes about man having one woman or two

Ulikuwa nami LAZARO SAMWEL mtunzi na mwandishi wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA.Kwa mawasiliano zaidi

CONTACTS ; 0653386586 /0753616584
EMAIL         ; lazarosamweli41@gmail.com




0 comments:

Post a Comment