Nikiwa na imani kwamba leo hii ni siku muhimu sana katika
maisha yako,sina shaka kuona kwamba ndoto zako pia mwaka huu zinaenda kuvuka
mipaka na kuwa zaidi ya hapa unavojiona.Lakini hili litaanza kujionesha kwa
kuondoa kauli ambazo zitakuwa hazina mashiko katika maisha yako kila siku na
hakikisha kwamba Hausemi SIWEZI kwamaana Mungu aliyekuumba
kwa mfano wake aliweza kukuumba wewe na kukupa pumzi ya kuweza kushinda kila jambo
ambalo liko mbele yako.Ukiona kwamba unasema siwezi ni kwasababu unajionea uvivu kufanya unachotaka
kukifanya na ni maamuzi yako pia,lakini licha ya kusema hivyo jua kwamba kauli yako ya kwanza ndiyo
sababu ya wewe kuwa kama unavojiona sasahivi kwamba kweli huwezi kufanya kitu
flani.Kijana mwenzangu ambaye unapenda vitu vizuri,tena ukiona kwenye tamthilia
unasema kwamba na mimi nataka kuwa na gari kama lile au nataka kuwa na nyumba
kama ile.Haikatazwi kufanya hivyo wala kuwa na uhitaji wa mambo mazuri kila mmoja anapenda kuwa na vitu vizuri namna
ile lakini kitu kikubwa ambacho unatakiwa kukielewa ni kutokana na huu msemo wa waswahili wanakwambia
kwamba “UKIONA VINAELEA JUA VIMEUNDWA” yani kunawatu kwanza walianza kuona
kuelea kwa kitu hicho kabla ya hicho kitu kuanza kuelea wakiwa na maana kwamba
kama ni kitu kizuri kunawatu ambao walianza kuona uzuri wa gari,nyumba na
vingine vingi ambavyo unavitamani na wewe kuwa navyo lakini walichokifanya ili kuweza
kupata vitu vile kuna mambo waliamua kufanya na waliamua kujitamkia maneno ya “NAWEZA”,tena
sio kwamba kuweza kifikra na kimaneno tuu lakini ilikuwa ni kuweza
kifikra,kimaneno na kimatendo pia.Hapa inamaana kuna mambo ambayo waliamua
kuyavunja katika ratiba zao tena yale mambo ambayo hayakuwa na umuhimu na
kuamua kuweka haya mambo hata kama haikuwa tabia yao kufikiri na kutenda katika
upande wa kuweza lakini walijitahidi sana kuweza kuwa kama walivyokuwa na kiu
ya vile vitu ambavyo walikuwa wanahitaji katika maisha yao.

Hapa nataka kukwambia kitu gani kijana mwenzangu? Kuwa na
ndoto kubwa ni kitu sahihi sana lakini haitatusaidia kama tutakuwa na wito
mkubwa ndani yetu kuweza kutimiza ndoto zetu hizi kubwa.Kama utakuwa
mfuatiliaji wa makala hizi nilishawahi kusema kwamba sisi kutamani kushinda
katika haya maisha haitatufanya kushinda lakini maandalizi katika kuyashinda
haya maisha ndicho kitu ambacho kitatufanya sisi tuweze kushinda.Jaribu
kujiangalia kwamba wewe unafanya maandalizi gani na ndoto kubwa ambazo unazo,je
unalala sana na kusema kwamba nina ndoto kuwa badala ya kuanza taratibu? Au je
unasubiri umalize chuo ndipo uanze kufanyia kazi kwa kisingizio kwamba hauna
muda wakati kila wiki unapoteza zaidi ya masaa 10 kuangalia mpira na kupiga
soga? Je unaona kwamba hauna mtaji ikiwa simu yako ikaishiwa vocha unaweza
kufanya juhudi yoyote kuweza kupata vocha ya 1000/= kwa siku? Toka njee ya hili
box kama kweli unandoto kubwa na hakikisha kwamba unalichoma mana ukiliacha
unaweza kurudi tena kule ukisema napumzika kumbe ni kurudi moja kwa moja tena.Sisi
vijana hatima yetu ni zaidi ya jinsi tutakavyosuburi ajira na kusema kwamba SIWEZI
kufanya jambo flani.Tunatakiwa kujiona zaidi ya jinsi tunavojiona kwamba tunaweza
kufanya jambo flani katika ofisi ya kampuni flani na sio kwenye kampuni zetu.
“Maisha yako ni zaidi
ya tafsiri ya changamoto ambazo zinakufanya useme SIWEZI.Mapungufu yako yasiwe
kigezo cha wewe kuendelea kusema kwamba SIWEZI” – LAZARO SAMWEL
CONTACTS ; 0753616584 / 0653386586
EMAIL ; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment