Tuesday, May 16, 2017

TASWIRA MPYA YA MAONO YAKO.


Tokeo la picha la vision quotes inspirational
Habari mwanamabadiliko mwenzangu wa karne ya 21.Lengo langu ni kuhakikisha picha iliyoko akilini mwako katika muonekano wa nega ya picha inakuwa kama picha halisia kabisa.Na hii ndiyo chachu kubwa haswa katika jamii zetu kutafuta mazuri kutengeneza taifa huru kifikra.

Tunaposema kuhusu maono kwa maana kawaida tunasema kwamba ni "uwezo wa kuona/ndoto".Kwa maana ingine tunaweza sema kwamba maono ni picha ambayo mtu anajenga akilini mwake na anataka kuitimiza yani kuitoa kwenye kitu ambacho kiko kwenye hali ya mawazo kwenda katika hali ya kitu ambacho kinaonekana.Kukosa maono kwa watu wengi mara nyingi husababishwa na watu kuishi maisha ya wakati ambao umepita na wenye maono huishi kwa kuangalia kesho yao (future).Maono mazuri ni yale ambayo yamejengwa katika kusudi  kwasababu huku ndiko mtu anapoweza kusonga mbele kuhakikisha kwamba anatimiza kusudi lake.Mfano wewe moja ya kusudi lako ni kwamba unataka kujenga nyumba na akili yako umeshaweka picha halisi ya nyumba yako itakavyokuwa na wengine unakuta kwamba wameweka mpaka picha ya kitu ambacho wanakitaka.Siri mojawapo ya maono ni kwamba lazima uindike kwanza ndipo tunasema kwamba haya ni maono,Sijui kama unanielewa hapa mana hauwezi kuwa na maono alafu ukawa hujaweka mipango ya kuhakikisha kwamba ile picha inatoka katika mawazo na kuwa kitu halisia ndo maana waingereza wansema kwamba “There is no vision without mission”.Kama huna maono kweli hauwezi kufanya chochote zaidi ambacho utakuwa unakifanya zaidi utakuwa na shughuli nyingi zisizokuwa na mpangilio wowote  na zikawa na matokeo ambayo sio mazuri kabisa katika maisha yako.Unajua kunatofauti kati ya mtu kuwa na matofali lakini hajui matofali yanatakiwa kufanyiwa nini na  ukakutana mtu mwenye matofali lakini anakwambia kwamba “bwana mimi nataka kujenga nyumba na ramani yake ni hii” hapa mwenye maono ni Yule ambaye anamatofali lakini anaona kitu flani njee na matofali lakini Yule mwingine ambaye anamatofali na hajui cha kufanya hana maono yoyote pia.

Tabia mojawapo ukianza kuwa na maono ambayo yako kaika kusudi lako huwa yanabadilisha mtu kabisaa mana hayamweki mtu kuwa kaama zamani alivyokuwa,maonon yanamfanya mtu kuishi katika kesho yake (future).Huwezi kusema kwamba unamaono ikiwa bado  ukiiangalia kesho yako unajiona kama ulivyo leo,hayo sio maono na kama kunakitu ambacho unasema kwamba ni maono yako na bado ukitazamia kwa mbali zaidi unajiona kwamba utakuwa palepale hauna budi kuachana na hayo maono mana hayo sio maoni. Siku zote ukitazamia maono yako ambayo unayo lazima utajiona mtu mwingine kabisaa na sio kama ulivyosasahivi,maono kwamba ukishakuwa nayo na ukaona kwa mbele yatavyoweza kukuinua kuna mambo ambayo taratibu unaanza kuacha tena unakuwa na heshima flani kwako mwenyewe na watu wengine pia mfano 

1. Lazima utaanza kuelewa matumizi yako ya pesa yanatakiwan kuwaje na sio kutumia pesa zako kila sehemu tena hata sehemu ambazo hazina umuhimu na wala hazikuongezei thamani yoyote.Utaelewa hela yako inatakiwa izunguke wapi na ikuletee kitu gani maana kwa mbalin kunakitu kizuri ambacho utakuwa unakiona kwaajili yako.

2. Utaanza kuelewa kwamba ni marafiki wa namna gani ambao unatakiwa kuwa nao manamara nyingine maono mtu anaweza kupata kwa kuwa n watu wenye maono lakini ukikaa na watu ambao hawana maono kuna asilimia kubwa sana na wewe kutokuwa na maono katika maisha yako na hatimae miaka itakuwa inapita unaishi maisha yeleyale huku mkifarijiana na wenzako ambao pia hawana maono .Angalia muda mwingine sio kwamba maisha ni magumu,jiulize watu gani ambao umezungukwa nao katika maish yako ya kila siku,utakuta kitu ambacho unalalamika kwa asilimia kubwa ni tabia za marafiki zako ambao unao au ambao unatumia muda mwingi kuwa nao.Jiulize pia inakuaje kwamba unalalamika maisha magumu alafu kunawatu kwa mwaka wanatangazwa kuwa mamilionea au mabilionea na ni umri wako?

3. Utaanza kujua umuhimu wa muda na utaelewa umuhimu wa muda kwenye Maono yako.Hiki ni kitu ambacho watanzania wengi tunacho na tunazani kwamba kuwa na maisha mazuri au kutimiza maono yet ni kutumia nguvu kwa muda ambao unautaka na utafanikiwa.Vijana wa kitanzania muda mwingine hatufanikiwi au hatuwezi kutimiza maono ambayo tunayo kwasababu ya matumizi mabovu ya muda haswa kwenye mitandao na pia kwenye vijiwe,inawezekana kwamba vijana wengi wanadhani kwamba kuwa na maono makubwa lazima uwe na elimu kubwa,hapana sio ukweli mana wewe kwenye faacebook unawezaje kujua lugha ya kingereza na haujui hiyo lugha? Mac Zukerbertg lengo lake ni kuwaleta watu sehemu moja na kuweza kuwasiliana kama uko nae jirani,vipi wewe kwa maono ambayo unayo ya kuwa na ardhi,nyumba,gari na biashara nyingi unadhani utazitimiza kw kupoteza muda sehemu ambazo sio muhimu alafu ukishamaliza ndo unapata akili ya kulalamikia serikali? Hapana kwa hivyo hatuwezi kufika na hata hatutaweza kuwa na maono na kuyatimiza.

4. Ukiwa na maono sio kila jambo utakuwa unafanya kwakuwa umeambiwa kwamba kunahela. Kumbuka kwamba kufanya kia jambo unalokutana nalo katika maisha yako ni ishara ya kujionesha kwamba hauna maono yoyote kuhusu wewe mwenyewe.Unaweza kuuliza kwamba mbona wengine wanakuwa na kazi zaidi ya moja na bado wanaishi na kweli sisi tunachoangalia ni kwamba kuishi maisha ambayo ni zaidi ya kawaida. Ukiwa na maono lazimo utakuwa misimamo ambayo umeweka katika maisha yako kuhakikisha kwamba muda wako ni wewe mwenyewe hautumiwi vibaya lakini unajitumia kuhakikisha kwamba maono yako yanatimia.

Kuna mengi sana ambayo ningependa kusema nawe lakini hizi salamu itakuwa ni kitu tosha ambacho kitakusaidia kuhakikisha kwamba unafungua ukurasa mpya katika maisha yako. Usikose kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA weka oda yako kukipata.Ulikuwa nami;

Lazaro Samwel (Create Youth Mindsets)
Contacts ; 0753616584 / 0653386586
Email     ;  lazarosamweli41@gmail.com




0 comments:

Post a Comment