Wednesday, May 17, 2017

TASWIRA MPYA YA MAONO


Tokeo la picha la inspirational quotes about having a vision

Habari mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel.Karibu sana katika kuhakikisha kwamba maisha yako yanabadilika na kukuondoa katika hali ya kawaida na kwenda kuishi maisha zaidi ya jinsi unavojiona siku hii ya leo.
"Usipojijenga jua hata kilichopo ndani yako hakiwezi kujijenga" - LAZARO SAMWEL

Katika moja ya misemo yangu ambayo huwa napenda kutumia nilishawahi kusema kwamba Huwezi kula ujana kama bado ni kijana lakini unaweza kutumia ujana kutengeneza uzee wa kula ujana,nikiwa namaanisha kwamba ujana hauliwi ukiwa kijana lakini ujana utanifaika nao ukiwa tayari hauna tena nguvu za ujana nikimaanisha unakula matokeo ya ujana wako. Sasa jiulize wewe unakula ujana au unakula uzee mana sisi vijana tunakula uzee na uzeeni bado tunakula uzee pia yani kuna mambo ambayo kijana unatakiwa kuyafanya wakati wa ujana lakini anafanya mambo ya uzee na uzeeni anafanya mambo ambayo alikuwa anatakiwa kufanya ujanani lakini muda anakuwa hana tena.

Hii ni kwetu sote vijana, inabidi tukumbuke kwamba  maisha mazuri hatuwezi kuyatengeneza kwa kuchezea muda katika mambo ambayo hayana maana katika maisha yetu, kaa ukijitafakari katika mambo ambayo unayafanya kuanzia kwenye simu yako ambako ndo ambako vijana wengi tupo, jiulize je simu yako inazidi kukufanya wewe kuwa liability yani kukupunguzia thamani? Ukiona ndio inabidi uchukue hatua mapema sana,lakini ukumbuke kwamba kijana ambaye anasifika kuwa na nguvu anatakiwa kutumia nguvu zake kujenga akili yake vizuri na tena sio kwa uvivu. Hauwezi kuhitaji Range Rover, BMW ikiwa kila siku hauwezi kukaa na kuwaza jambo jipya au kuwa na ratiba ambayo itakusaidia kuweza kubadili mitazamo yako. Unatakiwa wewe kuwa ASSET yani uwe mtu ambaye kila siku unajiongezea thamani kidogokidogo bila kujali kwamba  ni kidogo.

Hakuna ubaya wowote wa vijana kuwa na ndoto kubwa lakini je sisi vijana tuna nini haswa cha kuweza kusaidia Picha kubwa iliyopo ndani ya akilini zetu kutimia? Mana ukubwa wa ndoto zetu lazima uendane na Wingi wa maarifa  ambao unatumika kila sehemu sahihi katika ndoto zetu kubwa bila kupelea. Kosa kubwa ambalo tunalifanya ni kuwa na ndoto kubwa ambazo hatuzitafutii maarifa yoyote mfano tunaweza anzisha biashara lakini tukaifanya kimazoea bila maarifa na hapohapo bado tunakuwa na ndoto kubwa kutimizwa na hiyo biashara kwanini usiitafutie maarifa biashara yako toka mwanzo alafu uanze kuifanye vizuri kuliko kuifanya alafu hujui jinsi ya kuifanya huku unaona akilini mwako unandoto kubwa? Chukua muda wako na jifunze kwamba unatakiwa kufanya nini katika biashara yako ambayo unataka kuianza au unaweza kuanza kufanya biashara lakini pia ukawa na kasi nzuri ya kujifunza jinsi ya kuifanya kiumakini.

Naomba nikuachie salamu hii kwamba Tofali kiumbo unaweza kuliangalia kiubaya sana ukaona kwamba haliwezi kufanya chochote lakini ukiyachukua mengi na ukayajengea utajua thamani ya tofali iko wapi, utashangaa unapoona magorofa imara yamejengwa, nyumba nzuri zimejenga pia, lakini ukiangalia licha msingi ila muunganiko wa matofali mengine ndiyo ambayo yamefisha mapungufu yao.Hata wewe leo hii unapoona maarifa kama haya na kupuuzia ni sawa na kuona tofali moja kila siku ukalidharau kumbe kama utaamua kuchukua hatua na kila siku ukajitahidi kusoma makala hizi utaweza kuanza kujenga msingi mzuri wa maisha yako na maarifa haya ambayo yako kama tofali yatakusimamisha.

WEKA ODA YAKO YA KITABU CHA NGUZO 3 ZA MAISHA.

Ulikuwa Nami

LAZARO SAMWEL
0753616584 / 0653386586

SUBSCRIBE Youtube: LAZARO SAMWEL

0 comments:

Post a Comment