Wednesday, May 17, 2017

MAENDELAO YAKO/MAFANIKIO YAKO


Hongera kwa kuwa mfuatiliaji mzuri wa makala hizi za Lazaro Samwel naamini kunamambo ambayo umeyapata n aunaendelea kuyapata na leo hii unajiona  mtu mwingine na hivyo ndivyo tunavyotaka na sio tofauti. Mwanamafanikio leo hii nilikuwa niandike kitu kingine lakini nikawa nimeguswa kukwambia kuhusu hii mada ya MAENDELEO YAKO AU MAFANIKIO YAKO, naomba uwe makini sana kwa ninachoenda kuongea.

Mpendwa Mafanikio yako hayaji kwa kuendelea kulipia hela kununua vitabu au kuhudhuria semina bila kuamua kufanya mabadiliko katika kila jambo ambalo unajifunza lasi hivyo utakuwa ni mtu wa kusema kwanini sifanikiwi. Ndio,haufanikiwi kwasababu kunatabia za zamani ambazo umezishikilia mpaka leo na hautaki kuziachia kila siku, wengine toka zamani wamekuwa wakijupa matumaini kwamba nitabadilika lakini kesho yake anarudi na tabia zilezile za mwanzoni. Nikwambie neno moja usiseme umri umeenda ngoja niachie vijana na wewe kijana usiseme kwamba bado kijana ngoja nile ujana, ujana utakuja kuujutia ukiwa mzee na wewe ambaye umri unasema umeenda utakuja kukumbuka siku umefunguka lakini ukasema kwamba umri umeenda badala ya kuchukua hatua. Angalia katika Biblia wakina Abraham na mke wake Sara walipata mtoto wakati Abrahamu akiwa na miaka 99, wewe nani leo unamiaka 30, 35, 40 au 45 unasema umri umeenda amka acha kujidhoofisha kwa maneno yako, na wewe kijana wa miaka 20 ,25, 27 kwasababu hauna familia unasema unakula ujana angalia maisha hayakusubiri na wala ujana hautakupa PAUSE ule ujana,wakina Daudi na udogo wake wote alikuwa mfalme na aliongoza Israel, wakina Uziah katika umri wa miaka 16 alikuwa Mfalme na aliongoza Judah. Wewe unasema umri umeenda alafu kesho yake unaamka kuwahi vigengeni kupiga soga, kesho yake unakuwa makini kujua ratiba ya mpira, kubeti na kuweka kiwango cha hela kwenda kutazama leo hii unaona uvivu kuweka akiba au kujipangia malengo yako??  Tuamke sasa.

Mafanikio Yako hayaji kwa kuendeleza tabia hizo cha msingi ondo hizi tabia mapema;

1. Acha visingizio mapema sana na ikiwezekana ukiona unaanza kuwa na visingizo fanya hilohilo jambo ambalo unawekea visingizio.

2. Acha Kujiona wewe ni kamili mana utakuwa kama jiwe ambalo halinadiliko.Kubali kukosolewa panapohitajika kukosolewa, kuwa msikilizaji sio tu mwongeaji, jifunze kwa juhudi zote yani kama wewe ni kijana au hata mtu mzima na hauna hata kitabu kimoja kwako ila magazeti ambayo umekusanya na yenye thamani ya 100,000/= inabidi ujitafakari watoto wako mwishoni watajifunza nini kutoka kwako au wewe kijana watoto wako watajifunza nini kutoka kwako?

3. Ondoa Uoga kabisaa.
Ukijenga  uwoga utabomoa maisha yako kuanzia kwenye akili na mwili wako. Uwoga ukizidi utajenga hali flani katika akili yako na utaathirika hata kimwili na ndoto zako zitabaki tuu kusema lyti ningejua!

4. Kaa mbali na watu ambao hawakutakii mema tunasema hawa ni watu ambao sumu katika maisha yako, wenyewe wako kuhakikisha kwamba unashuka na sio kupanda katika maisha yako. Hawa watafanya uwe unasikia tuu watu flani wamefanikiwa badala ya wewe pia kufanikiwa.

5. Kuwa na majibu mawili katika maisha yako na yatumie sehemu sahihi pia kuhakikisha kwamba mafanikio yako unayapata namaanisha kwamba tumia NDIO sehemu ya kusema NDIO na sema HAPANA sehemu ya kusema HAPANA usikwepeshe maneno hapo jiamini.

Naomba kuishia hapa, naimani kunamambo ambayo umeyapata kupitia makala hii na kunamengi ambayo unaendelea kufunguka zaidi.Ulikuwa nami Lazaro Samwel  mtunzi na mwandishi wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA, kiu yangu ni kukuona unakuwa zaidi ya hapa na zaidi ya wengine ambao unatamani kuwa kama wao mana wewe ni zaidi ya mimi na wao.

Tunaweza wasiliana kwa namba hizi
Contacts ; 0753616584 / 0653386586
Email     ; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment