Hizi ni Salamu Zangu Kwako Kwa Ufupi
Mithali 12:1
"Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama"
Mithali 18:1-2
"Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe,Hushindana na kila shauri jema. 2: Mpumbavu hapendezwi na ufahamu;Ila Moyo wake udhihirike tuu".
Kuna mambo ambayo mtu ukitaka kufika mbali lazima uamue kibadilika tena sio kidogo. Kama ni mambo ya uchoyo unatakiwa kuacha kama ni roho ya kujikwaza kwa wengine pia unatakiwa kuacha, ukiwa na roho ya dharau kwa watu unatakiwa kuacha pia mana haya ndiyo ambayo yanaficha mafanikio yako. Wewe unaweza usione lakini kumbe kuna watu ambao wanaona unapoelekea sio sahihi na unachokifanya pia sio sahihi.Hapa unaanza kujishangaa mbona sisogei na wenzangu wanasonga mbele? Tatizo shamba lako ulipanda mambo ambayo unaona leo hayafai na hata ulivoambiwa shamba lako linaota magugu wewe ukasema hayo sio magugu. Hiyo itakuwa ni akili ya kitoto. (Soma 2 Wakorintho 9:6-7)
Lakini pia unaweza pata maarifa zaidi 1 Wakorintho 13 : 11 "Nilipokuwa mtoto mchanga,nilisema kama mtoto mchanga,nalifahamu kama mtoto mchanga,nalifikiri kama mtoto mchanga ; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto" . Kwanini nakupa mstari huu ndugu yangu Mkristo na Muislamu? Katika maisha yetu ili tuweze kusonga mbele na tuweze kufanikiwa lazima kuna mambo tuweze kuyaacha lakini kuyaacha ni lazima uchukue maamuzi kama Mtume Paulo anavotuambia kwamba "......tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto" kuyabatilisha sio kazi ndogo na ndo maana mpaka leo kuna watu wanaumri mkubwa lakini bado wanafanya mambo ya kitoto na wengine unakuta ni vijana wadogo lakini wanafanya mambo ya kiutu uzima na wako mbali. Tofauti ni kwamba kichukua maamuzi ya kuacha mambo ya kitoto na kuacha hayo mambo ya kitoto mojawapo ni kubadilisha fikra zako kufahamu na kutafakari kwanza na sio vinginevyo.Usiseme kuhusu umri, kwamaana unaweza kuwa na miaka mingi lakini ukawa bado una mambo ya kitoto na unaweza kuwa na umri mdogo lakini ukawa na mambo ya kiutu uzima swala ni kwamba fikra zako na ufahamu wako ukoje.Unakuta ni mtu mzima lakini anakuwa na tabia ya kuzira kama mtoto mdogo,kuwa mvivu hata kwenye mambo ambayo hayahitaji uvivu, kutokuwa na hekima ya kuongea mbele za watu kwa kuangalia uzito wa jambo flani, hapa inamaana hakuna ufahamu na kufikiri ndo maana inakuwa hivi.
Inabidi tubadilike ili maisha yetu yaweze kubadilika na kama unaona bado hujabatilisha mambo flani ya kitoto unatakiwa kuacha sasahivi na weka akili yako katika kutafuta maarifa ya kuhama utoto huo kwa kuwa na fikra na ufahamu sahihi wa kiutu uzima.
NAOMBA USALIMIE NA WENGINE KWA KUSHARE NAO UJUMBE HUU.
Karibu kuweka oda ya kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA.
Lazaro Samwel
Contacts ; 0753616584 / 0653386586
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
Facebook page ; Lazaro Samwel
Subscribe In Youtube; Lazaro Samwel
0 comments:
Post a Comment