Wednesday, May 17, 2017

TABIA KUU YA KUACHANA NAYO


Tokeo la picha la quotes about procrastination
Habari mpenzi mfuatiliaji wa makala hizi za Lazaro Samwel  naimani u mzima wa afya na unazidi kufunguka zaidi kila siku.

Leo hii katika mada  ambayo naenda kuwaelekeza ni kuhusu tabia moja kuu ambayo ningependa kukushauri kuweza kuiacha  mapema mana inaweza kuwa unaiona kila siku lakini unaichukulia kawaida kwasababu ya kukubali kuishi maisha ya kawaida kama watu wengi wanavyoishi. Tabia kuu hii ni ipi ambayo nakwambia licha ya kuwa na tabia nyingi sana ambazo zinampoteza mtu?? Tabia yetu kuu ambayo tunatakiwa kuiacha Ni KUHAIRISHA MAMBO au wazungu wanasema PROCRASTINATION, hii ni tabia ambayo idadi kubwa ya watu tunayo na tunailea kwa kuitetea pindi inapotokea kwetu lakini kumbe kuilea kwetu ndipo kunafanya sisi wenyewe kupoteza mambo ambayo tulikuwa hatutaki kupoteza. Unakuta mtu anatakiwa kufanya kazi flani sasahivi lakini anasema mpaka kesho wakati hata sasahivi inawezekana kufanyika, hii ndo tabia ya KUHAIRISHA.Lakini unatakiwa kukumbuka kwamba hakuna kitu kigumu kama kufanya jambo ambalo ulikuwa unatakiwa kulifanya leo mana kesho sio tu utalifanya hilo jambo lakini utafanya na yale ambayo ulikuwa unatakiwa kuyafanya hiyo siku, unakuta mzigo juu ya mzigo ambao unakufanya kutokufanya mambo yako kwa ufasaha zaidi. Kama ni kazini inamaana wewe unaweza kufukuwa kabisa na mwingine ambaye hana hiyo tabia akachukua nafasi yako. Tunatakiwa kuangalia kwamba kwani kunashida gani au kunagharama gani ambazo unapata kwa kufanya  jambo ambalo litakunufaisha wewe mwenyewe? Kama hakuna acha tabia hiyo na fanya mambo kwa muda sahihi na sehemu sahihi pia.

Ubaya mmoja mkubwa wa kuhairisha mambo yako ni kwamba itakufanya kuweza kupoteza fursa nyingi sana kwasababu unakuta kunakuwa na fursa hapo ulipo lakini na unatakiwa kuzifanya leo lakini unasema kesho.Nakwambia hivi kwasababu pia watu kama wakina John Masom mwandishi wa vitabu aliwahi kuandika na kusema kwamba Kuhairisha ni mboleo ambayo inakuza shida na matatizo, lakini kumbuka pia na waswahili wakasema kwamba Muda ni Mali inamaana wewe leo unavyohairisha mambo yako inamaana kuna muda ambao unaupoteza kwenye hilo jambo bila kufanyia kazi, kwa tabia hii usishangae kwamba kunasiku na wewe unajishangaa kwa kuwa masikini mana huko kuhairisha ambako uliamua kuufanya ulishakupotezea muda ambao ni mali yako.

Kesho huwezi kuijua na hujui itakuwa na mambo gani, kwanini sasa usifanye jambo ambalo unaliona mbele yako na unaona ni wakati wake? Mana kesho itakuwa na mambo yake tofauti ja ya leo.

Naomba kuishia hapo, nashukuru Sana kwa Muda wako ni mimi ;

Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email     ; lazarosamweli41@gmail.com

Facebook Page ; Lazaro Samwel

Youtube            ; Lazaro Samwel


0 comments:

Post a Comment