Kila jambo ambalo umeanza kuliwaza kwa mbele unaweza kuona giza nene sana ambalo halikupi hata unafuu wa kujua matokeo yake yatakuwaje, na tena ukizidi kuliboresha zaidi wazo lako na kulifanyia kazi unaona giza linazidi kuongezeka. Nikwambie kitu kwamba kila jambo ambalo unanza kulifanyia kazi huwa linaanza kama giza nene mbele yako,huoni mbele inakuaje lakini unakuwa na imani na matumaini kwamba nitaona mwanga flani katika hili jambo, ndivyo inavyokuwa katika maisha yetu. Lakini kumbuka hata katika Uumbaji wa dunia angalia katika Kitabu cha MWANZO 1:1-5 katika Biblia mstari wa 1: Hapo Mwanzo Mungu aliziumba Mbigu na Nchi. 2: Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena Utupu na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji;........3: Mungu akasema, iwe Nuru ikawa Nuru.
Kwanini nimekupa Mistari hii? Kwasababu maisha yetu pia tunapoanza kuyatengeneza kwenda sehemu nzuri mawazo yetu na nia zetu huwa na ukiwa, utupu na muda mwingi huwa tunaona giza katika kuyatimiza na muda mwingine giza kubwa likawa ni binadamu wenzetu. Mungu mwenyewe alivoanza uumbaji wake kulikuwa na anga lenye giza nene, ukiwa na utupu lakini licha Ya yote kunakitu aliona zaidi ya anga lenye ukiwa, giza na utupu, yani aliona wanyama juu ya ardhi, aliona ndege angani, aliona binadamu (sisi) juu ya ardhi,tunaweza kusema kwamba aliona mambo mema na mazuri zaidi ya utupu, ukiwa na giza katika mbingu na nchi. Hakujali kuhusu Shetani wala adui yoyote yule .Naomba kukwambia kitu kwamba alitupendelea sana na akatuumba kwa mfano wake na neno juu kutoka WAFILIPI 4:13 kwamba "Nayaweza Mambo yote Kwa Yeye anitiaye Nguvu". Leo utaona giza sana na binadamu wenzako wanaweza kuwa ndio giza kubwa zaidi lakini kunasiku atatamka na kusema NA NURU IWEPO KWAKO nawe utajitenga na wale ambao walikuwa ni giza katika maisha yako na mwanga utauona katika kila jambo ambalo inaligusa. Cha msingi mimi na wewe tusikate Tamaa na tujue kwamba kwa Mungu hakuna kukata Tamaa ila kunakusonga mbele zaidi ya giza lililoko mbele yetu mana giza sio kitu ndani ya mwanga ambao tutaupata kwa sala na maombi yetu kwa Mungu.
Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
Facebook Page ; Lazaro Samwel
Youtube ; Lazaro Samwel
0 comments:
Post a Comment