
Tukienda katika biashara ambazo watu wengi wanazifanya, mfano biashara za mtandao, biashara za chakula, biashara za duka, biashara za magari, n.k kuna jambo muhimu ambalo nimekuja kutambua katika biashara zetu ni kwamba, wengi huanzisha biashara kwa kasi nzuri sana na kwa moyo wote kweli wa kusaidia wengine kupitia biashara zao lakini ikifika muda mtu anapata kitu alichokuwa anakitaka biashara huwa mbovu na hata wateja hupungua. Nilishawahi kuongea mwanzo kabisaa kwamba biashara ukianzisha kwa kuangalia hela kwanza bila kuangalia biashara yako inawezaje kuleta mabadiliko kwa watu utapoteza wateja au kwa lugha ingine tunaweza sema kwamba biashara ukiifanya kwa kuipa kipao mbele pesa tuu na sio kutatua matatizo ya wateja wako itakufa mapema tuu. Biashara yenye maono mazuri kwa watu hufuatwa na hela na sio kwamba maono yako yatafuata hela. Watanzania wengi ambao hufanya biashara mara nyingi huanza na mimi nitapata nini wala hata hajali huduma ambayo mwenzake atapata (sio kosa kujua utapata nini lakini ni baada ya kujua utatoa huduma bora namna gani kwa wateja wako) na hii naweza kusema ndo kitu ambacho kinafanya wengi kutokuwa na mafanikio makubwa katika biashara zetu za kawaida. Mfano unafanya biashara ya kuuza chakula kwasababu unahitaji hela unapoenda sokoni kununua mahitaji wewe unaangalia tuu vitu ambavyo kwako hauwezi kuvipeleka na watoto wako wakala ila kwasababu unasema ni biashara unaona haina shida watanunua tuu na watakula tuu,sio hivyo hata kwenye biashara za mtandao walio wengi ambao wanaingia haswa unakuta ni kutatua changamoto ambazo wanazo katika maisha yake haswa huwa ni kipato ndio maana unakuta watu wengine wenyewe wanaingia kwenye biashara ili wapate mapato ya kumwingiza mtu tu lakini baada ya kumwingiza huyo mtu sasa unakuta hata sifa za uongozi anaziweka pembeni kumsaidia mwenzake lakini hajui kwamba sio kila mmoja anaakili sawa na passion ya muda sawa katika kitu anachokifanya na wanahitaji kuhamasishwa ikiwezekana wapewe semina zingine tofauti na biashara ya mtandao ili waweze kujitambua ili waweze kufanya biashara kwa moyo wote.Na kwa uelewa.
Nikupe siri moja mpenzi msomaji wa makala za Lazaro Samwel kila biashara ambayo unaifanya ili uweze kufanikiwa ifanye kama ambavyo wewe ungetaka kufanyiwa, yani kama ni mteja muhudumia kama ambavyo wewe ukienda sehemu flani unataka uhudumiwe, najua hii ni ngumu sana kwa watanzania wengi kwamba kumweka mteja kama mfalme au malkia ni kama kujidhakilisha, ila Tambua kwamba huku ndipo tunapoficha mafanikio yetu katika biashara zetu. Biashara bila upendo ni sawa na baiskeli bila matairi na mnyororo.Badilisha akili yako na anza kuitazama biashara yako kama wateja wako, penda biashara yako kama unavyojipenda mwenyewe, penda huduma yako kama unavyopenda kupokea huduma kutoka kaa wafanyabiashara wengine.
Ulikuwa nami,LAZARO SAMWEL mtunzi na Mwandishi wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA.
Unaonaje kama baada ya muda ukianza kupata makala hizi kwa kudownload katika Application na uwe nayo kwenye simu yako?
Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
Facebook Page ; Lazaro Samwel
Youtube ; Lazaro Samwel
0 comments:
Post a Comment