
Ukishakuwa kwenye ajira cha kwanza jua kwamba kuchukia ajira ambayo upo haitakufanya kuweza kutoka kwenye hiyo ajira na ubadilishe maisha yako kwenda upande mwingine unaoutaka .Haitakuja kutokea kubadilisha maisha yako kama unajua kwamba haupendi kuwa kwenye ajira flani na bado unaichukia,ila tambua kitu kimoja kwamba kuipenda kwanza ajira ambayo unayo ndicho kitu pekee ambacho kitakupatia njia sahihi ya kutoka hapo kwenda sehemu unayoipenda. Nasema hivi kwasababu wengi wameshaweka mawazo mazito kuhusu ubaya wa ajira ambako kumewafanya kuwa hata na matumizi mabovu ya pesa zao ambazo wanazipata katika ajira zao, lakini pia imewasababisha kutengeneza picha mbaya katika jamii kutokana na kutoa huduma mbaya. Hii picha ambayo wanaitengeneza kumbuka imeanza na kuchukia kazi zao na mwisho wa siku hata wanapoanza kufanya mambo yao binafsi hayaendi kwasababu tayari chapa ambayo iko katika jamii yao ni mbovu na mbaya.Na itakuchukua muda kuanza kutengeneza tena sifa zako nzuri ila kama bado upo kwenye kazi ambayo ulikuwa unaichukia unaweza kurekebisha kupitia huduma ile ile ambayo watu wanakuona kwa ubaya. Utendaji wako wowote wa kazi katika ajira ambayo inagusa maisha ya watu ni channel nzuri sana ya kujijengea msingi mzuri wa mambo yako pindi unaposema nataka kuacha ajira sasa na kufanya mambo yangu. Kumbuka hili
POKEA SALAMU ZANGU
Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
Facebook Page ; Lazaro Samwel
Youtube ; Lazaro Samwel
0 comments:
Post a Comment