Wednesday, May 17, 2017

SALAMU ZA KUISUBIRI AJIRA KUTOKA SERIKALINI

Tokeo la picha la waiting employment quotes
Imedhaminiwa na kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA 

Nimepata salamu zako Ndugu Yangu kutoka kwa rafiki yako niliyemwambia akusalimu kutokana na jumbe zangu  sijaridhika na jibu lako la kwamba unasubiri Ajira na serikali imebana sana Sijachoka kuendelea kumwambia rafiki yako akikutana nawe akwambie nakusalimu kwa Nia ya kubadili watanzania wenzetu kifikra. 


Nazidi kukusalimu mana nikiacha utasahau kitu kimoja muhimu sana juu ya maisha yako haswa ni kutokana na maswali ambayo ulishajiuliza toka zamani na ukajijibu mwenyewe. Nilisikia siku ukisema na kumwambia rafiki yako kwamba huwezi kufanikiwa kwasababu ya aina ya familia ambayo umetoka? Lakini pia rafiki yako alishaniambia kwamba unasema maisha ni magumu lakini hauwezi kuishi bila kuangalia mpira kwa wiki  na kuweka vocha kila baada ya siku 1 ambako inakuhitaji kuweka kuanzia 7000/= au 10,000/= kwa wiki hapo tumeacha hela yako ya kula kwa wiki kama pia 10,000/= mana nasikia wewe haupendi kujibana kwenye kula vyakula vizuri. Cha mwisho kwa uchache rafiki yako kaniambia kwamba bado unalalamika kwamba huoni ajira japo unakisomo cha stashahada. Naomba nikusalimu kwa kujibu maswali uliyoniuliza kupitia rafiki yako.


Rafiki kama nilivyokuambia tatizo lolote ambalo utakuwa nalo  hicho ni kiashiria cha tatizo lingine kubwa zaidi ya hili unavyoliona na Tatizo lenyewe ni kutokuwa na UELEWA. Kushindwa kuelewa ni sawa na kuchukua mbegu na kuweka juu ya jiwe ukitegemea kwamba itaota na utavuna. Familia yako haiwezi kuwa tatizo la umasikini wako na ukiona unasema hivyo jua unajitakia kuwa hivyo na inawezekana unapenda ile hali ya familia yako kuwa hivyo ili iwe kama kisingizio chako wewe kutokupigania maisha yako pale unapokutana na changamoto.Changamoto za familia zetu tunatakiwa kusichukua kama vichecheo vya sisi kuweza kupigana na kuwa zaidi ya pale tulipo na sio kuchukulia kama pumziko la kupigania maisha yetu kwenda katika level zingine. Lakini pia rafiki nikujulishe hiyo ratiba ya kuangalia mpira kwa wiki na kupoteza kwa mwezi zaidi ya 30,000/= bila kujua, utasemaje hauna ajira au hauna kitu cha kufanya, kwanini usitafute vijana mkaonganika kwapamoja na hizo hela ambazo mlikuwa mnapoteza kwa mambo ambayo hayana msingi mkaangalia kitu cha kubuni hata kama kwa mtaji mdogo?? Inawezekana sio lazima iwe mnaangalia vijana huwa tunasehemu nyingi sana za kupoteza hela bila kujua sasa hizo sehemu ndo mitaji yetu, vijana wengi wa kitanzania wanadhani mtaji ni lazima mpaka upewe na benki au ukopeshwe na kidogo ambacho anakuwa macho anaona sio mtaji, Badilika Kijana. Naomba nikusalimu kwa kukwambia kwamba unamuda mwingi sana lakini ni kawaida yako kusema sina muda wakati unamuda wa kukaa kwenye simu kwa masaa hata 4 kwa siku yenye masaa 24 na bado utasema sina muda wa kusoma vitabu, sina muda qa kupata coaching and mentoring, sasa kwa staili hii kwanini nisiendelee kukusalimu kila siku mana hunielewi? Kunawatu wanatengeneza hela nzuri kaa dakika moja wewe lisaa limoja unakosa hata kuhudhuria semina au kujisomea kitabu unategemea nini? Nitamwambia rafiki akwambie kwamba Tanzania mpya haswa kwa vijana inaanza kwa kubadili fikra zao kujitambua na kujua jinsi gani wanaweza kitumia walichokuwa nacho ili waendane na kusudi lao na sio kutumia wengine ambavyo wameshavitumia, hiyo haitaleta utofauti.



Najua nimekusalimu Leo kama ndugu na najua kunamengi unahitaji kujifunza ili tuanze kuongea kwa lugha moja ya kuwabadilisha marafiki wenzetu wengine. Usisite kuwasiliana nami nikupatie kitabu changu cha NGUZO 3 ZA MAISHA kwa 10,000/= tuu pamoja na ofa yake ya kitabu kingine cha Soft copy. 


Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)

Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email     ; lazarosamweli41@gmail.com

Facebook Page ; Lazaro Samwel

Youtube            ; Lazaro Samwel





0 comments:

Post a Comment