
SALAMU ZANGU KWAKO KWA KIFUPI
Ukijua thamani ya UPENDO utajua umuhimu wa kufanikiwa lakini ukijiweka kujua uzuri wa CHUKI utajua na kupata hasara zake Mana mbegu huota ulipoipanda na haiwezi kuota tofauti na ulipoipanda hata siku moja.Ukiwaza na ukaamua kutenda jambo flani ambalo ni jema jua hata kama utapata changamoto namna gani na ukataka kukata tamaa jua kwamba utaishi pazuri tuu lakini Ukiwaza na kuanza kutenda jambo baya jua utaishia kupata mabaya tuu siku zote katika maisha yako labda ubadilike na uaze kifanya mazuri.Napenda kukupa moyo kwamba jema lako litazalisha mazuri yako ambayo unayataka cha msingi ongeza juhudi na usiangalie nyuma wale ambao hawajathubutu kama wewe ulivyoamua.Usijilinganishe na wengine mana hata jua na mwezi vyote vinaangaza lakini kila kimoja kinamuda wake,tabia zake na hata sifa zake pia.
Hizi ni salamu zangu kwako mana unamaana kubwa sana katika maisha yangu na bado natazama kuinuka nawe kwa kukubadilisha kifikra zaidi. Msalimie na mwenzako mwambie mbegu ambayo tunaipanda ni ya kuleta mabadiliko ya kifikra katika maisha yetu.
Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
Facebook Page ; Lazaro Samwel
Youtube ; Lazaro Samwel
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
Facebook Page ; Lazaro Samwel
Youtube ; Lazaro Samwel
0 comments:
Post a Comment