Wednesday, May 17, 2017

TATIZO SIO TANZANIA ILA NI FIKRA ZA WATU WALIOKO TANZANIA


Tokeo la picha la THINKINGmindset quotes

Ukimwona na Mwenzako Mwambie Namsalimu Kwa Kuikomboa Tanzania Kifikra -Lazaro Samwel 

Ni jukumu langu na lako kusema kwamba Maisha bila ufanisi huondoa ujuzi kabisa. Na maisha ya maslahi kwanza huondoa Ujenzi bora wa kipaji chako. Nakusalimu Ndugu Yangu mana huu ndio ukwelii ambao kila siku tunauona.

Ni jukumu langu na lako kutambua kwamba hakuna mtu yoyote maskini ila ni tafsiri ya umasikini ndiyo inayotumaliza kila kukicha, tatizo sio kutokuwa na mtaji ila ni uelewa wetu katika mambo ambayo yanatuzunguka haijalishi ni vingapi au ni vya aina gani.  Tatizo sio umasikini lakini umasikini ni alama ya kuwa na tatizo kubwa nyuma yake. Nakusalimu Tuu ndugu Yangu na nataka Tuende pamoja kwamaana Tanzania ni inchi ambayo ina watu ambao wanaitwa masikini lakini ni matajiri wanafunikiwa kujiona ni masikini kwelii badala ya kuwaondoa katika janga moja la umasikini wa fikra na sio kuwaambia masikini. 

Nakusalimu Tuu ndugu yangu mana umasikini ambao Tanzania tunaambiwa tunao sio umasikini wa hela ila ni umasikini wa fikra na Tatizo kubwa ni kutokuelewa kuhusu muda, japo kwa neno moja kubwa ni kwamba tumekosa UELEWA.Na huu uelewa ni kutokujua kwamba sekunde moja ambayo tunaipoteza kunawatu ambao wanatengeneza  hela kubwa,sio hivyo tuu lakini pia kulalamika hatuna cha kufanya lakini wageni kutoka inchi zingine wakija huku wanaona cha kufanya, jee sisi tunaubongo tofauti na wao? Hapana,kila kitu ni sawa lakini jinsi tulivyojenga uelewa katika akili zetu ndivyo ambavyo vinaleta shida kubwa katika maisha yetu. Umasikini wa fikra unaanza kwa kukosa uelewa na kuchangia kuleta umasikini wa kipato.Nikwambie kitu, kwamba uelewa wako haujengwi kwa kufanya vitu ambavyo havina umuhimu lakini unaanza kwa kufanya mambo ambayo yanaumuhimu kwanza na hapa ndo ktu pia ambacho watanzania wengi tunakosa kwamba hatuna vipaombele kwasababu tumekubaliana na umasikini wa fikra kama ndo maisha yetu. 

Japo nakusalimu leo na naomba usalimie wengine nilikuwa na shida ya haya maswali ujiulize mana Tatizo ni asilimia kubwa ni sisi wenyewe kwamba kwanini hutaki kujitoa katika hilo janga la umasikini wa fikra?kwanini hutaki kusoma vitabu? Kwanini unalalamika maisha ni magumu lakini hauyachukulii hatua? kwanini unajiona masikini wakati wewe mwenyewe ni fursa kwa tatizo ambalo unalo? Kwanini useme serikali ndo inabana wakati wewe unatumia masaa   9 kulala 5 kupiga hadithi 4 kuangalia tv na 4 kwenye mtandao 2 kwenye 2 kuzurura sehemu ambazo haizina  umuhimu? 

Nakusalimu Tuu ndungu yangu ukimwona na mwenzako mwambie Namsalimu kwa kubadilisha fikra za Watanzania wenzangu japo sijafika napotaka mana wengi tunatakiwa kuinuana na kwenda pamoja.

Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email     ; lazarosamweli41@gmail.com

Facebook Page ; Lazaro Samwel

Youtube            ; Lazaro Samwel




0 comments:

Post a Comment