
Katika hali ya kawaida hakuna mtu yoyote ambaye hana wakati mbaya au hali ya huzuni katika maisha yake unaweza kuona mtu anatabasamu, anacheka lakini kumbe moyoni mtu anahuzuni tele. Hata mimi pia huwa ba haki ya huzuni na wewe najua lazima huwa unakuwa na hali ya huzuni unakuwa na mudi mbaya pia. Lakini hata yote tunatakiwa kuweka kitu kimoja akili kwamba vyote vinakuwa na mwisho wake na haviji kukaa milele katika maisha yako, leo unaweza kuwa na hali ya huzuni bila amani lakini kesho unaamka uko na hali ya furaha na amani tele, haya ndo maisha yalivyo kila siku. Sasa inakuaje watu wengie wanaishi maisha ya furaha kama hawajawahi kuwa huzuni katika maisha yao? Haswa wengi na hata mimi huwa siipi huzuni mazingira yoyote hata kama najua kwamba hapa kweli naweza kuwa na huzuni na kitu kingine ambacho huwa napenda kuwaambia watu ni kutokuingixa huzuni katika akili yako ikajenha hisia mbaya ambazo zinaweza kukuletea madhara katika maisha yako haswa kiafya mana itafanya hata kuwa na msongi wa mawazo pia, cha msingi ni kujua kweli huzuni ipo lakini haina makazi kwangu na inatakiwa kuondoka. Ukiamua kuacha huzuni kweli ukitawale italazimisha kutengeneza mazingira ya muda mrefu na hapa unakuta inazalisha hisia ambazo zitakufanya hata jambo dogo likitokea unashangaa unasikitika sana na kuathiri hata utendaji kazi wako wa akili. Kunawengine wandhani kuondoa huzuni ni kunywa pombe lakini nikwambie kitu, hapo ni kama unajisahaukisha kuhusu huzuni lakini huzuni iko pale pale. Pia tukumbuke huzuni haiwezi kuja bila kuitengenezea mazingira ya huzuni na ukitaka kuondokana na huzuni jitahidi kutoka katika mazingira ya huzuni ambayo yako kwako au kama yanayokuzunguka.
Wingi wa huzuni ndani yako ni upotezaji wa Muda wa kuachia huzuni kuondoka ndani yako - Lazaro Samwel
Sasa ni mambo gani ambayo mtu anatakiwa kuyafanya ili aweze kuepukana na huzuni na kuwa na Furaha;
1. Ukiona unahuzuni jitahidi kufanya mazoezi mfano kukimbia, kuruka kamba au mazoezi yoyote ambayo yataweka akili yako sehemu ingine tofauti na akili.
2. Kama Unapenda kusikiliza Muziki sikiliza miziki ambayo sio pia ya kuhuzunisha angalau kwa dakika 15 au 20.
3. Jitahidi kufanya mambo ambayo unayapenda na huwa unatulia kwa kutumia akili kuweza kuyatenda hii itakutoe katika mazingira ya huzuni.
4. Soma vitabu vya hadihi au uhamasishaji hii itakusaidia kuweza kukuweka vizuri hata katika jambo ambalo unalionea huzuni.
5. Jichanganye na watu kubadilishana mawazo angala kwa 30 au 35 minutes hii inakufanya kujenga taswira ingine mana utakavyoongea na watu na kufurahi ndivyo utakavyojijengea mazingira mazuri ya furaha ndani yako kusahau huzuni uliyokuwa nayo.
6. Usikae na watu ambao wanaolalamika na kuhuzunika kuhusu mambo ambayo yanaweza kukusababisha na wewe kuwa na huzuni zaidi. Mfano unahuzuni mpenzi wako amekuacha hautakiwi kwenda kukaa na watu ambao wanaongelea kuhusu mambo hayohayo utazidi kuumia, jaribu kutafuta mambo mengine tofauti na hayo itakusaidia.
Nitaomba kuishia hapo kwa Leo, naomba tukutane muda na wakati mwingine kwaajili ya somo lingine pia.
Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
Facebook Page ; Lazaro Samwel
Youtube ; Lazaro Samwel
0 comments:
Post a Comment