Wednesday, May 17, 2017

TANZANIA INATAKIWA KUWA JEMBE NA MPINI NA SIO MPINI WA JEMBE KUPITIA ELIMU


Tokeo la picha la QUOTES ABOUT MISUNDERSTANDING ABOUT SCHOOL EDUCATION
Tatizo Kubwa la Tanzania  ni kutafuta jembe ambalo tumeshikilia mikononi mwetu wenyewe tena mpaka tunafika shambani  na tunasema hatuna shamba - Lazaro Samwel 

Ukitaka kujua taifa la Tanzania linapoendea kufa usitazame walioko kwanza madarakani ila angalie hiki kizazi ambacho kinakuja kuachiwa uongozi na picha ambayo wanayo kuhusu uongozi. Utagundua kwamba Tunapoelekea ni kwamba tutakuwa ni watu wa kukimbia vya kwetu na kuthamini vya wengine na hata tukitaka kuwa na vya kwetu tutahitaji wengine kututengenezea vyetu. Nitaendelea kusema kwelii kuhusu elimu haswa elimu ambayo inamlazimisha mtu kuwaza kuajiriwa na sio kujiajiri kwa asilimia kubwa. Elimu ambayo inamfunga mwanafunzi kutafuta njia mbadala ya kuweza kujikwamua kimaisha kuanzia kwenye fikra yake. Leo hii Elimu inafanya watu ambao hawajasoma kuona kwamba huo ndo mwisho wao wa kuweza kufanikiwa kimaisha kwasababu walishasikia elimu ni ufunguo wa maisha na wakadhani ni elimu ya darani tuu ambayo ndiyo ufunguo wa maisha. Kunakipindi nilikuwa nikisikiliza kwamba serikali inataka kurudisha heshima ya  elimu ya juu yani chuo kikuu lakini nachokiona ni kwamba inazidi kushusha hadhi tena sana elimu ya chuo kikuu, nakwambia hivi mana ukitaka kuthibitisha kutana na mwanafunzi ambaye amemaliza chuo mwaka 2015 na alikuwa ameweka fikra za kuajiriwa lakini hajaajiriwa uone maisha yake yalivyo au pia jaribu kumchukua muweke na mwanafunzi wa inchi zingine kwa kuwalinganisha ndipo utajua naongea nini. Napigwa na butwaa kuona viongozi kushangaa vijana kukosa ajira ikiwa wanajua chuoni wanafunzi wanasomaje au wanafundishwaje. Nikwambie kitu kimoja hata umri wa kuishi vijana unapungua haswa wasomi kwasababu ya msongo wa mawazo na hii inaathiri sana ubongo wao kufanya maamuzi. Viongozi wengi hawajui ladha ya ganda la ndizi la karne hii ya 21 kuelekea karne ya 22 ambako pesa inakuwa na matumizi katika kila kona tofauti na Enzi zao, wanajua ladha ya ndizi yenyewe ila vijana ambao ndio kama watu wao haya maganda wanayala sana na wanaona uchungu wake. Hakuna umuhimu kama kitu unachokisoma na kukilipia kinakuwa baadae hakina maana yani mzazi anasomesha mtoto wake kitu anachokipenda akidhani kwamba kitampunguzia mzigo alafu baadae serikali inachukua kwamba huyu kijana kitu alichokisomea hakina umuhimu sana wacha akae mtaani, this is not serious kwelii kijana akae shuleni miaka 16 mpaka akapata certificate alafu anarudi mtaani tena anakaa miaka 2 au mitatu bila chochote cha kufanya? inabidi serikali kuangali hili kwa ukaribu tena kwa utaratibu sahihi mana tunapoteza rasilimali watu wenye ujuzi wa kutosha.

Ni Tanzania Pekee Mambo Haya Hufanyika.
Tokeo la picha la QUOTES ABOUT MISUNDERSTANDING ABOUT SCHOOL EDUCATION

♻Elimu ni ufunguo wa maisha na ufunguo wa maisha  unasemekana upo kwenye kuajiriwa kwa asilimia kubwa lakini watu hawajawekwa wazi jinsi mawanda ya elimu yalivyo na sio darasani tuu na kuajiriwa ambako Ufunguo wa maisha hupatikana.Na kijana anaamua kuacha kipaji chake kupigania ajira ambayo mwisho wa siku anakosa vyote.

♻Mwanafunzi anafurahi kumaliza form six kwenda chuo lakini anapokaribia kumaliza chuo anakuwa na msongo wa mawazo atapata wapi ajira japo huyu kijana akili yake ndiyo ajira.

♻Watu wanatafuta kutengenza jina la kwamba  Anakisomo  flani japo anajua kwamba kisomo hicho hakitambadilisha maisha yake mana alitegemea ajira tuu. 

♻Kijana anakaa mtaani akisubiri ahadi za serikali kuajiriwa kwa miaka 3 au hata 5 na serikali inaona hakuna shida. 

♻Ni Tanzania pekee inasema tunataka serikali ya viwanda ikiwa kuna vijana zaidi ya 30,000 mtaani wenye visomo vizuri na wanaakili changa ambazo zingetumiwa kuleta hivyo viwanda lakini wenyewe ndo wanaambiwa wasubiri serikali iwape ajira.

I WONDER WHY?? -(Am Just Saying)


Ila Pia Ewe Kijana Mpenda Mafanikio pata Kitabu chako cha NGUZO 3 ZA MAISHA kwa 10,000/= tuu na pia jitahidi kujiunga na group la ASK LAZARO SAMWEL kuweza kupata msaada wa maswali ambayo unayo. 

azaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email     ; lazarosamweli41@gmail.com

Facebook Page ; Lazaro Samwel

Youtube            ; Lazaro Samwel






1 comment: