Biashara ni kujiheshimu katika matumizi ya muda wko na wateja -Lazaro Samwel
Habari mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel,leo hii nimeguswa na kuhakikisha kwamba nakufungua uelewe ni jinsi gani wewe mwenyewe unaweza kuwa biashara kabla ya biashara yako ambayo unayo.TWENDE PAMOJA
Unapogundua kwamba mteja hanunui bidhaa tuu bali ananunua tabia moja wapo kutoka kwako kuweza kurudi tena hapo utakuwa umeweka biashara yako sehemu nzuri.Na sio kutengeneza bidhaa nzuri alafu mteja anapokuja kuichukua anaondoka mtupo na kitu cha kurudi tena kuchukua huduma kwako. Ukiachana na mambo mengine ambayo unayajua katika biashara yako kitu muhimu ni kujua aina ya wateja wako ambao huwa wanakuja kuchukua huduma kwako na tabia zao ni za namna gani? Usipoweze kulitilia hili maanani utaweza kuhamisha wateja sehemu zingine ambazo wanawafanya wateja kama mfalme.
Kitu kimoja ambacho nimejifunza kutokana na makosa ya wafanyabiashara wengi wenye kampuni au biashara yoyote wanakiu ya pesa kuliko kiu ya huduma, wengi wanaharibu biashara zao hapa, au unakuta wengine maneno yao hayaendani na metendo katika utoaji wa huduma zao. Kuna wakati nadhani tusiwe na kinyongo mtu mwingine kufungua biashara kama yako karibu yako au katika maeneo ambayo umeweka biashara yako kwasababu makosa yako ambayo huwa unayapuuzia inawezekana wengine wameyaona na wakaona ni bora kuyafanyia kazi. Uzembe wako katika kutengeneza biahara yako ndani haswa katika utoaji wa huduma unaweza kupoteza uwepo wa huduma yako. Nikwambie kitu kimoja biashara yoyote ambayo unaifanya kwa matakwa yako upate kitu flani kweli unaweza kupata unachokitaka kwa muda flani lakini Mungu huangalia Roho za watu ambao unawapa huduma ile kama kila mmoja au watu wengi wanalalamika kuhusu huduma yako na kusononeka kwa huduma yako au kuhusu bidhaa yako ambayo unawapa hataona haja ya kuweza kukubariki kazi yako ikue kwa vizuri ila Mungu atakuacha kwanza urekebishe makosa ambayo unayafanya kwa makusudi au sio kwa makusudi, na usipoweza kuchukua hatua kurekebisha utalea tuu biashara yako au itakufa kabisaa baada ya muda. Mteja anaposema Mungu Mbariki mtu flani kwa huduma yake ndivyo na wewe kila unachokigusa dunia nzima itasikia kuhusu kazi yako lakini kama mteja anaondoka na kusema huyu mtu hafai utaendelea kulea biashara yako bila hata kukua.
Nimejifunza kitu kimoja kuhusu biashara, kwamba Biashara yako ni maneno ya rohoni ya wateja wako unavyowapa huduma nzuri na wakaipenda kutoka mioyoni mwao hata biashara yako nayo itafika mbali lakini kama utaifanya kwa matakwa ya kupata hela na wateja kuwachukulia wa kawaida tuu unawakati m'baya sana unapoelekea katika biashara yako. Pia biashara ni watu na sio pesa kwanza, weka hili akilini mwako, unapoheshimu kazi ya wateja wako bila ubaguzi wowote ndivyo utakavyobadilisha biashara yako, lakini ukifanya biashara kwa ubaguzi utasonga mbele lakini mwisho utakuwa mbaya mana hata wale ambao utawapendelea sio kila siku ndio ambao unawahudimia.Heshimu Wateja wako Kwanza Ndipo hela Zitakuja tuu.
Asante Kwa Muda wako.
Karibu kupata kitabu chako cha NGUZO 3 ZA MAISHA kwa 10,000/= ndani yake ;
♻NGUZO 1 ; MAENDELEO BINAFSI.
♻NGUZO 2 ; MAHUSIANO.
♻NGUZO 3 ; UJASIRIAMALI NA BIASHARA.
Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
Facebook Page ; Lazaro Samwel
Youtube ; Lazaro Samwel
0 comments:
Post a Comment