Wednesday, May 17, 2017

UNAWEZAJE KUWA BIASHARA 1

Tokeo la picha la HOW CAN YOU BE BUSINESS QUOTES
Ukitafuta kisichokutafuta kitakupa kile usichokitaka katika maisha yako na ukitafuta kinachokutafuta kitakupa unachokitafuta katika maisha yako - Lazaro Samwel

Sikujengi ufanye biashara tuu ila nakujenge wewe uwe biashara ambayo itajenga  biashara ya kutumiza malengo yako - Lazaro Samwel

Usifanye biashara kabla ya wewe mwenyewe kuwa biashara. Ukilazimisha kufanya biashara bila kuwa biashara wewe mwenyewe jua utaishia kupoteza kile ulichotumia kuanzisha biashara yako. Namaanisha nini kuhusu haya maneno? Usifanye biashara bila kujijua na kujua ulichokuwa nacho kinawezaje kuleta matokeo chanya kwa watu, usifanya biashara kama huna maarifa ndani yako kuhusu biashara ambayo unataka kuifanya kumbuka kitu kimoja kwamba ukiwa na maarifa ya kutosha kuhusu biashara ya kitu flani huwa kunakuwa na msukumo mkubwa sana kukifanya na kufanikiwa.Ukiona biashara yako inafanya vibaya rudi angalia nyuma jee ulianza kwasababu ya mtu flani? Ukikuta ndio ni bora ukaacha kuifanya kuliko kuendelea kuifanya ili uweze kujipanga upya na kuleta biashara ambayo inamawazo yako na sio mawazo ya watu wengine. Hii inaweza kuwa kazi kwako kwasababu hukuwa umejizoesha lakini nikwambie kitu kwamba ubongo wako kwa muda flani unaweza kuubadilisha katika kuwaza kwa kuhakikisha kwamba kwa muda mwingi unauuliza unaweza kufanya biashara gani na utaifanyaje. Watu wanadhani kuwaza ni lazima uwe umekaa sehemu ambayo imetulia, lakini hapana, kumbe hata ukiwa unatembea huku ukiwaza unaweza kupata wazo zuri la biashara. Kwa kifupi ni akili yako kuizoesha kuwaza kuhusu biashara itakufanya kupata wazo zuri sana la biashara.Usiache kichwa kuwaza mambo ambayo hayana msingi na ambayo ukishamaliza utakuwa hujapata faida yoyote kwa muda huo na baadae.

Nikupe siri ya mambo ambayo  watu wengi inawafanya kutokuwa na biashara nzuri na baadae biashara zao kupotea kabisaa ; 

1. Kutokujua wateja wake wanataka nini lakini anachojua ni yeye anataka nini, ukitanguliza umimi katika biashara jua hauna muda unapotea kabisaa katika biashara. 

2. Kutokujali Muda wa wateja wako. 
Hapa ndo kitu ambacho wengi huwa tunakosea na kushindwa kuelewa zaidi kwamba mteja hata kama hajui kutumia muda lakini anapenda huduma ambayo sio ya kumpotezea muda. Leo unaweza muhudumia mteja wako nyuma na muda akakwambia kwamba huduma nzuri lakini moyoni anasema sirudi tena angalia sana muda na jifunze kusema Samahani lakini isizidi kiasi.

3. Hela ni biashara na biashara ndiyo ambayo inakuletea hela.
Wengi tunavyotambua ni kwamba Biashara ni hela na hela ndiyo inayoleta biashara badilisha mtizamo wako katika hili na biashara yako itakuwa mbali sana. Ukilenga sana kwenye hela jua utapata hela kujenga biashara ambayo haikujengi kabisaa.

4. Biashara ni mimi na mimi ndiye biashara na sio biashara ni biashara na itabaki yenyewe kuwa biashara.
Unaweza kuwa na bidhaa nzuri sana na ofisi nzuri sana lakini kama wewe hauwezi kuanza kuwakilisha bidhaa zako anbazo ndo biashara yako hakuna mtu ambaye atahitaji bidhaa zako. Hapa ni kuanzia katika matumizi ya lugha ya kibiashara na wateja inatakiwa kuwa nzuri.

Naomba kuishia hapo lakini ningependa kukupa taarifa ya kuanzishwa kwa kundi ambalo litakuwa linahusu Wafuatiliaji SERIOUS WA MAKALA za POSITIVE MIND VIBE na AUDIO ZAKE,huko kwa baadae makala zote zitaamishwa na kutakuwa na section ya maswali na majibu kila siku ya jumapili kutokana na ulichojifunza. Kama utahitaji kuunganishwa karibu sana.Kumbuka hii ni kwa watu ambao ni SERIOUS kusoma makala hizi na kusikiliza hizi AUDIO.

Lazaro Samwel (NGUZO 3 ZA MAISHA)
Contacts ; 0753616584 / 0653386686
Email     ; lazarosamweli41@gmail.com

Facebook Page ; Lazaro Samwel

Youtube            ; Lazaro Samwel

0 comments:

Post a Comment