Friday, May 5, 2017

UNAWEZAJE KUTEMBEA NA MAARIFA?


Picha inayohusiana
Habari Mpenzi msomaji wa makala hizi za Lazaro Samwel.Kwa asilimia kubwa sana ukiangalia watu wengi sana imekuwa ni ngumu sana kukaa na simu kutokana na mambo mbalimbali ambayo mtu anafanya kupitia simu yake,lakini pia ukiangalia tunaweza kujiuliza jee ni haki mtu kusema kwamba hana kitu cha kufanya kupitia simu au je mtu anaweza kweli kukosa maarifa kama kweli anasimu ambayo inauwezo mzuri wa kuingia kwenye mtandao? ndio inawezekana kwasababu hatujajua matumizi mengine ya simu ya kusema kuwasiliana tuu.Hii yote ni kwasababu tumekosa maarifa.Kama kama kampuni za simu kama APPLE,NOKIA,SAMSUNG na zingine nyingi zinakutengenezea simu wenyewe wapate hela kwanini na wewe usitumie simu kupata hela? JISEMESHE MWENYEWE na jiulize umekaa na simu yako kwa muda gani na umewatengenezea VODACOM,TIGO,AIRTEL na mitandao mingine shilingi ngapi kwa kuweka vocha na kuingia kwenye mitandao? baada ya hapo njoo jiulize na wewe umetengeneza shiling ngapi kupitia simu yako? Nataka kukupa picha kwamba usifanye kitu kimazoea kama unajua hicho kitu unaenda kukitumia kwa matumizi ambayo yanakuongezea gharama badala ya kukuongezea thamani flani katika maisha yako, Simu inaweza kukubadilisha kifikra kama kweli unaweza itumia vizuri ipasavyo,jiunge na magroup ya whatsapp ambayo unajua yatakuelimisha na kukufungua kifikra zaid na kumbuka sio lazima katika kila group ambalo unapewa link yake ujiunge mengine ni ya kuyatupilia mbali kabisaa kwasababu hayatakupa mwelekeo thabiti wa maisha yako mfano magroup ambayo yanaongelea kuhusu mambo ya mapenzi kila muda,group za siasa kila muda n.k.Unaweza kudownload application za vitabu katika simu yako mfano dropbox na ukaweka vitabu vyako huku ukiona umechoka unasoma,ukiona umepumzika mahala bila kazi muhimu unaingia kusoma.Lakini pia kupitia simu yako unaweza kujiinua na kufanya watu wakujue kutokana na mambo ambayo unafanya kama ni biashara ya chakula unaweza kutangaza mahali ambako unapatikana,kama ni website unaweza tangaza watu waifuatilie zaidi,kama ni biashara ya matunda pia unaweza kuweka wazi na wateja wako wakaju,kama ni biashara ya duka pia unaweza kutuma kwenye magroup ya whatsapp,kama ni kufanya semina pia unaweza kufanya kwenye whatsapp na ukatengeneza hela nzuri tuu ikawa ndo mtaji.

Tokeo la picha la quotes concern how phone can ruin our life
Kijana wenzangu usilalamike kwanini hauna ajira alafu unasimu ya 700,000/= au 350,000/= utachekwa na utaonekana kama hauna akili kumbe uko vizuri sana.Sasa kama umegundua kwamba ulifanya makosa kununua simu ya bei ghali na huna uwezo, bora uuze simu hiyo ujitengenezee msingu mwingine wa kutengeneza hela kwa kufanya biashara au kuwekeza.Kijana mwenzangu kwa umri huu ambao tunao ni umri wa kuatfuta maarifa zaidi na zaidi kabla mambo hayajaanza kuharibika na sio kukaa kivinginevyo,hakikisha hata kwenye begi lako au mkoba wako unakuwa na kitabu kimoja cha maarifa ili muda wako usiwe unapotea kwa kusingizia sikuw na kitu cha kufanya.

Hizi ni salamu zangu kwako kwa ufupi nikiamini makala hii haitaishia kwako tuu bali na wengine pia utawashirikisha ili wapate salamu hizi.

Ulikuwa nami ;

LAZARO SAMWEL Mtunzi na mwandishi wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA.

CONTACTS ; 0753616584 / 0653386586
EMAIL         ; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment