Habari mpenzi msomaji wa makala za Lazaro Samweli nikiwa na
imani kwamba Unaendelea vizuri na harakati za kuinua kusudi lako.Leo hii
nimependa kukuandalia makala hii fupi nikiwa na imani itaenda kuongeza kitu
flani katika maisha yako na utasogea mbele zaidi ya pale ambapo upo sasahivi.
Tunajua katika maisha kunamsemo mmoja ambao tunausikia sana
na huwa tukiusema mara nyingi ukisema kwamba “Maisha bila ufanisi humaliza
ujuzi wake” kwamba maisha bila kuonesha utofauti sio kitu na ni sawa na
kuwa msindikizaji wa maisha ya wengine na hapo ndipo tunaposema kwamba mtu
anaanza kujiona kama hastahili mambo mazuri bali ni mabaya tuu.Ila kumbe wewe
ambae unajiona hivyo kuna mambo ambayo
unakosa uvumilivu kuyafanya uweza kujitambua na kuweka ufanisi wa kutembea
katika kusudi litakalokupa maisha ambayo unayataka .Nikwambie kitu usiwe na
haraka kupata vitu vizuri ikiwa hata chembe ya kusudi lako haujalitambua ni
bora utumie muda mwingi kuweza kutambua ni wapi roho yako inakutuma kuelekea
bila kusahau kusali sana katika harakati za namna hiyo.Najua ulidhani sitaweka
kitu kwamba ni lazima usali ila nakusii bila Sala bado itakuwa ni ngumu sana
kujitambua unapaswa kuwa wapi zaidi, utakuwa ni mtu wa kutangatanga huku na kule
bila kuwa na sehemu husika ya kuweza kutulia.
Tunaposema kuwa na uvumilivu namaanisha nini? Kwanza kabisa
naomba nianze na huu msemo mmoja ambao naimani utakuja kunielewa vizuri kwamba “Maisha
ni lazima yawe na changamoto mana bila changamoto hakuna mafanikio” ndomaana
tunatakiwa kuwa na uvumilivu katika mambo yetu ambayo huwa tunayafanya ili
tuweze kufikia malengo yetu yenye mafanikio bila hivyo tutakuwa ni watu wa
kukata tamaa kila kukicha na tusione matokeo yoyote mazuri.Kwahiyo kwenye
maisha lazima tukubaliane na jambo moja kwamba katika mipango yetu yote ambayo
tumejiwekea lazima tukianza kuchukua hatua cha kwanza kabisa ambacho tutakutana
nacho ni changamoto ambazo ziko kwa lengo la kutupima na kama hatutakuwa na
uvumilivu mafanikio tutayaona kwa mbali kuanzia pale tunapokata tamaa katika
changamoto ambazo tunakutana nazo. Nimekuchorea mchoro wa pyramid kuonesha
kwamba tunapoweka malengo mwazo kabisa na tukaona kama ni madogo lakini sasa tukianza
kushuka chini kupata mafanikio yatu tutakutana na changamoto lakini pia
ukimalizana na changamoto utakutana na mafanikio ambayo ulianza kuyapangia
mipango toka muda na ukaona kama ni madogo.
Piramidi
Ya Mafanikio Ni Lazima unze na;
1.
Mipango ; kwamba unataka
nini,kwasababu gani unakihitaji,utakipataje,sehemu gani unaweza kukipata,na kwa muda gani
unatakiwa kukipata.
2.
Changamoto; Hapa ni kwamba unapoanza kufanyia kazi malengo
yako sasa kunakuwa na ufungua huu changamoto ili uweze kukukaribisha katika
mazingira mapya na kukufanya uwe mzoefu na sehemu ambayo itakuwa mpya katika
maisha yako.
3.
Mafanikio ; Ni matokeo ya uvumilivu wako katika changamoto
ambazo umepitia na sio vinginevyo.Hapa sio kila mmoja huwa anafika licha ya
kuweka malengo kwasababu sio kila mmoja ambaye ni mvumilivu.
Kwa Watu wengine pia wameweza kuweka Piramidi ya Mafanikio kama ifuatavyo
1. Unataka kuwa na nini ikiambatana na picha ya kitu ambacho unakitaka katika maisha yako haswa yawe ni maono ya mambo ambayo yako katika kutimiza kusudi lako.Kwamba ujenge picha ya jinsi kitu ambacho unakitaka kitakavyokuwa hii itakusaidia kukuongezea kasi ya kupigana katika maisha yako mfano unataka kuwa na nyumba baada ya muda wa miaka 2 sasa lazima uwe na picha kwamba nyumba yako itakuwaje ndani na njee na ujione kama uko ndani ya hiyo nyumba pia,
2.Unatakiwa kufanya nini ili uweze kusogea karibu na maono yako yani kama ni nyumba ambayo unayo akilini mwako? unachotakiwa kufanya ni hakikisha kwamba kunakuwa na shughuli ambazo unaziweka ili uweze kuhakikisha kwamba baada ya miaka miwili unakuwa na nyumba kweli kama ni kuweka akiba kwa kiwango flani na iwe hivyo pia.
3.Weka sasa malengo kuweza kuhakikisha kwamba unatimiza ile picha na mambo ambayo umepanga kufanya.
4. Kuwa na mikakati ya kuweza kuhakikisha kwamba unatembea katika malengo yako ambayo umeshajiwekea.
Naomba kuishia hapo naimani
kuna kitu ambacho umejifunza nakupongeza sana kwa kuwa pamoja name,lakini
ningependa kukupa ofa ya kitabu cha NGUZO
3 ZA MAISHA kwa bei ya upendeleo kwa kuweza kuwa na ujasiri wa kusoma na
kumaliza makala hii ya POSITIVE MIND
VIBE. Ni kwa watu 10 wa mwanzo tuu ambao wamesoma makala hii ndio ambao
watapata kitabu.
SOMA;KWANINI UNATAKIWA KUSOMA KITABU CHA NGUZO 3 ZA MAISHA
SOMA;KWANINI UNATAKIWA KUSOMA KITABU CHA NGUZO 3 ZA MAISHA
Ulikuwa nami LAZARO
SAMWEL Mtunzi na mwandishi wa kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA.Kwa
mawasiliano zaidi
CONTACTS ; 0753616584 /
0653386586
EMAIL ; lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment