Thursday, April 20, 2017

HAUWEZI KUTOA BILA KUPOKEA


Tokeo la picha la quotes receiving

Habari mpenzi msomaji wa makala za Lazaro Samwel.Naimani uwepo wako ndio ambao unafanya blog hii kuendelea kuwepo lakini pia uhitaji wenu wa maarifa ndio ambao unatupa chachu ya kuzidi kuinua vipawa vyetu kwa kuwainua nyie kwanza kwa maarifa ambayo tunayo na maarifa ambayo tunaizidi kuyatafuta kuhakikisha kwamba kila mmoja anabadilika na anakuwa na maisha ambayo anayataka katika maisha yake.Makala za Lazaro Samwel ni makala za kila mtanzania na sio watanzania baadhi.Karibu Sana na twende pamoja.Ila nakukumbusha  ukikutana na Rafiki Zako Waambie Lazaro Samwel Anawasalimu kwa Nia ya kuwaona Mnakuwa na Upendo wa  mafanikio kwa kila mmoja ambaye mnakutana nae pia.

Najua baada ya kuona msemo huu wa kwamba MAFANIKIO YANAANZA KWA KUPOKEA utakuwa umejiuliza vipi kwamba tunaambiwa kwamba KUISHI NI KUTOA au Ukitaka kupata unachotaka lazima usaidie wengine wanachotaka? Haya ndo maswali ambayo najua cha kwanza yatakuwa yamekuja akilini mwako na ukaanza kuona kama hauelewi.Lakini cha kwanza kabisa kabla ya chochote hauwezi kutoa kitu chochote bila kukipokea na kuwa nacho ndipo ujiandae kukitoa kwa mtu mwingine.Huwezi kusema kwamba nataka kuwasaidia watu bila kwanza kujisaidia mwenyewe ndipo uweze kuwasaidia wengine.Hauwezi kusema kwamba nataka kusaidia watu kuwa na furaha kabla wewe mwenyewe hujapokea hiyo furaha ndo uanza kutoa kwa wengine,unapoambiwa kwamba kuishi ni kutoa kumbuka katika kutoa kwanza lazima kunakitu uwe umepokea ili na wewe uweze kutoa hata kama ni kidogo namna gani.Mungu siku zote anachokifanya kwako ni kwamba huwa anakupa kitu flani nawe unakipokea kuweza kutatua jambo fani mfano Unasema kwamba nina shida ya hela na ukamlilia Mungu kweli,sikiliza nikwambie kitu kimoja Mungu hatakupa hela moja kwa moja kwanza kabisa kinachofanyika ni kwamba anakupa maarifa na wewe unapokea alafu sasa hayo maarifa ukiyatoa ndani yako na kuweza kuyatumia ndo unapata kitu ambacho unataka,lakini kilichoanza kwanza kabisa ni kupokea kwanza.Tatizo ambalo inakuja kwa asilimia kubwa ya watu wanajiandaa kutoa tuu wanasahau kuwa aina yao ya kutoa inategemeana na jinsi ulivyopokea chanzo cha kile kilichokupa unachokitoa.Ukiwa na upokea m'bovu utakuta hata unachotoa kitakuwa ni kibovu pia.
Kuna mambo ambayo ukimwomba Mungu anakupa lakini sisi ndio ambao tunakosea kupokea na hata tunapopokea sio kama tulivyoomba.Hauwezi kusema kwamba nataka kuwa kocha wa maisha ya watu ikiwa bado hujapokea hiyo talanta ya kuwa kocha wa maisha ya kwako mwenyewe kabla ya kuwa kocha wa maisha ya watu wengine,hauwezi kusema kwamba nataka kuwa mhamasishaji kabla hujapokea talanta ya kujihamasisha mwenyewe alafu sasa uhamasishe wengine, na jinsi ulivyoipokea hiyo talanta yako ndivyo utakavyotengeneza watu wa namna jinsi ambayo ulifanya maandalizi ya kuipokea.Ukipokea kwa shauku ya kutaka kutimiza matakwa yako tuu hata uhamasishaji wako hautakuwa wa kufuungua watu kweli lakini kuwadidimiza mana utakuwa unafanya uhamasishaji kwa ubinafsi,hauwezi kusema nataka kuwa mwalimu kama ndani yako hujapokea talanta ya kuwa mwalimu na ndo ufundishe wengine,nikwambie kitu kuhusu baadhi ya walimu unaona kwamba wanalalamikiwa kutokuwa walimu wazuri mashuleni lakini kumbe unakuta kwamba wengi walipokea talanta ya ualimu kwa maslahi na ndo maana hata wanachokitoa sio kama kilivyokuwa kinategemewa,hata katika sekta zingine utakuta hivihivi na ukiipokea kwa moyo wote yani kwa upendo utaitendea haki talanta yako.Mimi nawe kunamambo ambayo tumeyapokea na inawezekana ni mengi sana zaidi ya haya ambayo nimakutajia lakini ninaimani kunamoja ambalo unalo na ndilo ambalo umelikamata,licha ya hivyi bado unaona mambo hayaendi kama unavyohitaji usilitupe lakini rudi na jiulize ulilipokeaji hili jambo lako na rekebisha.Mungu wetu ni wa huruma na siku zote yupo kwaajili ya kutusikiliza na kuturudisha katika mstari imara na mzuri wa kuweza kutimiza kusudi letu.

Napenda Kukushukuru Sana Kwa Muda Wako Na Naimani SALAMU zangu katika ujumbe huu utashirikisha na wengine lakini pia unaweza acha ujumbe chini kutokana na ulichojifunza.

Kama Bado hujapata kitabu changu cha NGUZI 3 ZA MAISHA au kwa Kubadilishana mawazo naomba tuwasiliane kwa namba hizi;
Contacts; 0753616584 / 0653386586
Email    ; lazarosamweli41@gmail.com

0 comments:

Post a Comment