Thursday, March 16, 2017

WAACHA WAKUCHEKE ILI BAADAE WAAIBIKE


Picha inayohusiana

 Karibu Mpenzi msomaji wa mtandao huu wa Lazaro Samwel katika kuhakikisha kwamba unaenda kupata maarifa ambayo yatakusaidia kubadilisha maisha yako pamoja na jamii yako kwa ujumla.

USIOGOPE KUCHEKWA KWA KUTETEA KIPAJI CHAKO KUKUPELEKA KATIKA KUSUDI LAKO - Lazaro Samwel            
Katika kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA niliweza kuweka kipengele cha tofauti kati Ya KUSUDI NA KIPAJI. Nikasema kwamba Kipaji ni Kama Alama za barabarani Kukufikisha salama sehemu ambayo unataka. Usikose kusoma hiyo sehemu kama Bado jitahidi kupata kitabu.
Lakini  nikwambia kitu katika safari hii ya kuweza kuhakikisha kwamba unatembea ndani ya kusudi lako sio rahisi. Na nakusihii ujue hili wala usihofie kutambua hili. Ukiweza kujua hili safari itakuwa nyepesi kwa kiwango flani zaidi ya kutokujua. Utapingwa sana pindi unapoamua kuanza,utakatishwa tamaa sana mana kusimama katika kusudi lako kitakuwa kitu kipya sana mbele ya macho na akili za watu. Kusud lako inapoanza kulifanyia kazi wengi hawawezi kuona unachokifanya mana ufunguo wewe ndiye ambao unao na picha ya mwisho wake Mungu atakuwa amekuonesha.
Kipaji ndugu ni kitu cha kujifunza na ukiwa nacho pia kishikilie sana unaweza kuanza kukitumia ukashangaa unaambiwa unafanya kazi bure au unapoteza muda,cha msingi endelea kujifunza. Kipaji huanza kwa  udogo sana ila unapoongeza juhudi ndipo na chenyewe pia kinazidi kuwa kikubwa na bora zaidi.
Nikupe mfano wa Tiger Wood alianza kucheza Golf akiwa na miaka 3 lakini alianza kuwa maarufu na kutengeneza utajiri akiwa na miaka 20 inamaana Tiger Wood ilimchukua miaka 17 kuweza kutengeneza kitu ambacho kimemfanya kuwa Moja kati ya wanamichezo ambao wanalipwa hela nzuri zaidi.  Hapa unajifunza nini? Funzo ni kwamba haichukui muda kidogo kupata mambo makubwa lakini itachukua muda mkubwa kupata kitu kikubwa na sahihi katika maisha yako. Ndo maana wazungu wasema ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA.Cha msingi ni kuendelea kupigana tu.Kipaji chako kinaweza kuwa katika mapishi na ndo umeanza my friend kama hapo ndipo roho, akili na nafsi yako ipo jifunze zaidi alafu songa mbele matokeo hayaji haraka taratibu utakuja kuyaona, kama ni mwandishi andika sana hata kama huna hela ya kutoa kitabu kunasiku utakuja kuona umuhimu wake  usisahau kuongeza maarifa ya kuandika kitu cha tofauti zaidi na ambacho kitakuwa historia na kuacha alama katika akili za watu, kama wewe ni muhamasishaji isihofu kwanini hujawa na mafanikio au huonekani kwenye runinga ila endelea kukuza kipaji chako na fanya kwa usahihi kunasiku utaitwa na wewe kutengeneza kipindi chako na watakulipa, kama wewe ni mkulima inaweza ikawa ndo usafiri wa kukufikisha katika kusudi lako  kama hiyo sehemu ndipo akili,nafsi na mwili wako imedhamiria kufanya usiofie unapopata changamoto mana hapo ndipo mafanikio yanapoanza kuonekana.

Jua ulimwengu unamengi hata kama ukiamua kufanya jema. Cha msingi jaza ubongo wako kwa vitu sahihi kukufikisha katika kusudi lako.Naamini safari ya kusudi lako lazima mkono wa Mungu utakuwepo tuu kuweza kukuongoza mana ndipo alipokuweka wewe hapo na sio pengine. Kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA niliandika sehemu kuhusu KUSUDI kwamba Mungu Hawezi kukubariki Sehemu Ambayo hajakuumba  uwepo  Hii ni ikiwa unaishi ndani ya KUSUDI la watu wengine. Acha uteseke kwa kuchekwa, kusemwa, kusengenywa kwa kutaka  mafanikio kupitia kusudi lako hata kwa miaka 10 ili uje ufurahi kwa miaka ambayo imebaki ya maisha yako hapa duniani.

Lengo Langu Ni kuhakikisha Mimi na wewe Mwaka Huu Tunatengeneza Historia Na Watu Watambue Uwepo Wetu. Isiwe Tu kila Mwaka Tunawasifia na kupigia makofi Wengine  kwa vitu ambavyo tunaweza kuwa navyo na tukaonesha Uwezo wetu Thabiti. TWENDE PAMOJA


@Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational Speaker
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
contacts ; 0753616584 /0653386586

0 comments:

Post a Comment