Thursday, March 16, 2017

SABABU AMBAZO ZINAFANYA BIASHARA NDOGO KUFA MAPEMA


Tokeo la picha la motivation picture concern the rule for growing small businesss

Habari mpenzi msomaji wa mtandao wa Lazaro Samwel,natumaini u mzima wa afya na unaendelea vizuri na majukumu yako ya kila siku.Najua wewe ni mjasiriamali au mfanyabiashara kwa namna moja ama nyingine na makala hii ya leo ni kwaajii ya kukufanya wewe kuwa mpya katika biashara yako ambayo unaifanya,twende pamoja.
Kutoka na utafiti uliofanywa na shirika binafsi linaloitwa Bloombery ambalo linamilikiwa na mtu mmoja anaitwa Michael Bloombery kutoka marekani kuhusu Biashara Ndogondogo  lilipata majibu yafutayo; 80% ya biashara ndogo hufa ndani ya mwaka mmoja zinapoanzishwa yani kwamba katika biashara ndogondogo 10  ambazo huanzishwa 8 hufa mapema ndani ya mwaka mmoja na 2 huendelea vizuri. Hata Tanzania watu wengi sana wanapenda biashara na wanapenda kuanzisha biashara zao nje ya ajira lakini kunamambo ambayo hawayajui ndio maana wengi utakuta hawafanikiwi katika hizi biashara. Katika kitabu  hiki ningependa kukufungua kuweza kuelewa ni mambo gani ambayo unayakosa  ili biashara yako kusonga mbele zaidi na kukuletea matokeo mazuri. 

Zifuatazo ni sababu ambazo zinafanya biashara ndogo kufa mapema pale mtu anapoamua kuianzisha.

1. Mtu kuwa na uwoga wa kushindwa.
Hili ni swala ambalo kila mfanyabiashara anakuwa nalo na ndo maana wengi hawafiki mbali kwasababu biashara anaiwekea mawazo ambayo ni butu. Tukumbuke  kwamba kama utakiwazia kitu kwa ubaya lazima kunasiku kitageuka na kuwa kama jinsi ulivyokuwa ukikiwazia.Ni sawa na biashara yako kwamba uliamua mwenyewe kwa uzuri kuifanya lakini bado moyoni mwako unaiwazia kuishindwa kumbuka hiyo tabia ambayo unakuwa nayo ya kuiwazia kwamba utaishindwa itakufanya kwanza ufanye biashara yako vibaya na utaanza kujipa maneno ya uongo kwamba ulijua itakuwa hivyo, hapana wewe ndiye ambae umesababisha mpaka ikawa hivo. Kwa kukushauri ukiona kitu kama hichi kinakuja katika kufanya biashara yako, ikatae kabisa na usiipe nafasi katika kuiwazia kabisaa katika akili yako mana unanguvu zaidi ya kushindwa katika biashara yako. Na ukiona kunakisababishi cha kukufanya wewe kuona kama utanguka katika biashara yako kaa nacho mbali hata kama ni ndugu au rafiki yako.

Mark Twain aliwahi kusema kwamba “Jiweke mbali na watu ambao wanajaribu kudogosha malengo yako/Ndoto zako.Watu wadogo hufanya hivyo,lakini wale wakubwa watakufanya kuona kweli na wewe unaweza kuwa mkubwa”

2. Kukosa maono katika biashara yako.
Picha ambayo unaijenga kuhusu biashara yako ni kama nguvu ambayo unajitengenezea kuhakikisha kwamba unafika. Ila kumbuka kwamba maono mazuri ni yale ambayo yanaambatana na Mikakati na malengo ya jinsi ya kuweza kuhakikisha kwamba kweli kitu kinaonekana. Yogi Berra aliwahi kusema kwamba “kama huweki malengo, usilaumu kwanini huyafikii”.
Hakuna kitu ambacho kinaweza kumfanya mtu kufanya biashara yake kwa juhudi kama picha ambayo ameijenga kwa baadae jinsi biashara yake itakavokuwa.Ukiwa maono makubwa lazima utaweka juhudi kubwa na ukiwa na Maono madogo lazima utakuwa na juhudu ndogo mana haikutishi kuyatimiza ila utakuwa unaona kwamba hata kesho utaweza kuyatimiza.

3.Kuwa na kiu ya pesa badala ya kuwa na kiu ya kuongeza thamani katika biashara yako kwanza.
Huwa napenda sana kusema kwamba hakuna kitu kizuri tukiwa tunaanzisha biashara zetu hakuna kitu muhimu kama kuondoa kiu ya shidah zetu kwanza katika pesa na kuangalia kuitengeneza biaahara zetu vizuri zaidi. Mana biashara ndiyo ambayo itakupatia hela ambayo itakusaidia kutatua matatizo yako na kuweza kukuhakikishia inakusaidia katika mambo mengine muhimu. Wengi huwa tunasahau biashara tukishapata faida kidogo kwenye biashara.Naimani umeshawai kuona watu wakifungua sehemu ya kula mwanzoni huanza kupika chakula kizuri, kadri siku zinavyozidi kwenda na kupata faida kwa wateja kuongezeka wanaanza kupika chakula kibovu na hawajali tena wateja kama mwanzo.Mwishi wa siku atasema kwamba biashara yake imelogwa ila sio kwamba biashara imelogwa ila yeye ndo mchawi wa kusababisha mpaka biashara yake kufa.

4.Kukosa Maarifa
Biashara hufa mapema ukikosa maarifa.Na biaahara kuwa ngumu ni kukosa maarifa. Tafuta maarifa juu ya biashara yako kuondoa giza ambalo liko ndani ya biashara yako. Tafuta maarifa juu ya kutengeneza masoko sio Tanzania tuu dunia nzime,kujua jinsi ya kutengeneza wateja wa kudumu katika biashara yako, pia jitahidi sana kutafuta maarifa kujua jinsi unavyoweza kuleta mabadiliko ya biashara  yako ikaendana na mabadiliko ya kiteknolojia.
Hapa pia naweza kuongeza mtu kukosa maarifa ya kujua jinsi ya kutumia pesa za biashara yake,kutokujua wapi ni sehemu muhimu ya kutumia pesa na wapi sio sehemu muhimu. Hili ni jambo la msingi sana kulitambua mana usipoangalia utabaki kutumia mtaji wote na mwisho wa siku biashara kufa. Kitu kingine katika matumizi ya pesa usichanganye na matumizi yako binafsi. Lakini pia nilishawahi kugusia kuhusu vitu ambavyo unatakiwa kutia maanani ili biashara yako isife mapema unapopata hela katika biashara yako

a. Tenga Malipo Yako

b. Hela ya dharura.

C.Weka Pembeni Kiwango cha Mtaji wa Biashara Yako.

Hakuna biashara ambayo ni mbaya ila ukikosa maarifa kwasababu unataka kuonekana na wewe unafanya biashara lazima biashara utaiona mbaya.Mtu wa kwanza ambaye ni mbaya katika kuinua biashara yake ni yule ambaye anamiliki biashara na sio biashara yenyewe.

Kusoma makala hizi inaweza isitoshe sana naomba uwasiliane nami uweze kujipatia kitabu changu NGUZO 3 ZA MAISHA sehemu yoyote ulipo kwa 10,000/= na utapata ofa ya kusafirishiwa bure.Kitabu hichi kimeshabadilisha fikra za watu wengi sana ambao napokea shuhuda kutoka kwao na wewe inawezekana huu mwaka kupitia kitabu hiki tukaongea kutengeneza historia ingine.

Ulikuwa nami ;

@Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational Speaker
Email ; lazarosamweli41@gmail.com
Contacts ; 0753616584 / 0653386586




0 comments:

Post a Comment