Friday, January 27, 2017

UNAWEZAJE KUIONA FURSA NA KUITENDEA KAZI??


Tokeo la picha la quotes concern opportunities risk to make money

Fursa ni pungufu lolote ambalo unaliona katika jamii yako  au kwa mtu yoyote na kuweza kulipatia  suluhisho. Hapa ndipo fursa inapoanza kuonekana. Mfano watu mtaani kwako wanashida ya vitafuno hiyo ni fursa pale unapochukua hatua ya kuwapikia mandazi, ukiona jamii yako inahangaika katika kupata huduma ya mpesa hiyo ni fursa pale unapoamua kufungua kibanda chako cha mpesa. Na vingine vingi.

Nikwambie kitu kimoja kwamba fursa zinaanza katika akili yako hakuna sehemu ingine, mtu asikudanganye kwamba atakuonesha fursa, naimani kama atakuonesha itakuwa ni ile ambayo kwake ni fursa. Utayari wako katika ubongo wako ni fursa tosha lakini umejiandaaje kuziona hizo fursa ndo kazi inapoanzia ndo maana wengi tunapenda kufanya mambo ambayo yanafanywa na wengine bila uboreshaji wowote (innovation).

Fursa hauwezi kuiangalia katika macho ya kawaida na ubongo ukawa haujajishughulisha ukasema ni fursa.Ukiona hivo jua kwamba unarudia jambo la mwingine na ikiwezekana kama unandoto kubwa kwa baadae acha kwanza jitafakari.

Kwanini nasea hivi?

Fursa thabiti ni fursa ambayo inaendana na mtu mwenyewe ndani  yake. Hii naongelea fursa ambayo inambadilisha mtu maisha yake kabisaa ndani na njee.

Unadhani  kwanini vijana wengi hatuzioni fursa??

Hizo ndizo sababu za kutokuona fursa

1. Tunaona fursa na hatutaki kuangalia fursa.

Hapa namaanisha kwamba vijana wengi tunapenda kuwa wazee vijana. Yani hatupendi kushirikisha akili zetu kabisaa. Tena ukiona umeangaisha kichwa kidogo ghafla umechoka au hata unaweza kusema kwamba naumwa (uvivu huu wa kufikiri). Ni wapi fursa ni mteremko tuu akili haitumumiki? Labda iwe ni utapeli ule wa kuambiwa lete 6000/= upate milion 3.

2. Kuwa na mtazamo mbovu kuhusu fursa hata kabla ya kuanza kuifanya.

Hii ndo mbaya sana hawa huwa wanajiita wajuaji japo hawajui chochote yani wao wanapenda maisha mazuri lakini wanapenda fursa rahisi, utabadilishaje maisha yako? Na nani kakwambia maisha marahisi namna hiyo?? Piga kazi fanya uchunguzo wa fursa ambazo unaziona.Hapa hapa, watu wengi wanakuwa na mitizamo ya namna hiyo kwa kuwa wameshasikiliza kwa wengine wanavyosema kuhusu fursa flani tena mfano anasikia mtu anasema fursa flani ni mbaya na yeye moja kwa moja na anaona ni ngumu na hata akiwa anaongea na wenzake pia anasema ni ngumu. Nikuambie kitu watu kama hawa sio vizuri kuwapa asilimia nyingi kukaa nao watakufanya kuwa mwongeaji wa vibarazani ukaacha kuamka hapo na kufanya mambo yako na kukamata fursa ambazo zinajitokeza mbele yako.

Unajua  ukitaka kupatwa na mafua kaa na mtu mwenye mafua ndivyo ilivyo hata kwetu kwamba ukitaka kutokuona fursa kaa na watu ambao wao kila siku ni kupondea fursa yoyote ile ambayo inajitokeza mbele yao, utaleta ushuhuda hapa kama na wewe utaiona hiyo fursa.japo pia hiyo ni fursa kwako? mana unaweza kuandika kitabu juu ya malalamiko yako na ukawaambia kwamba mnaweza kupata suluhisho lenu huku na ukawauzia.

Naomba nikuoneshe jinsi ya kuweza kuzifanya hizi fursa mana huo upande ni mrefu kuuelezea.

Les Brown muhamasishaji ambaye ni kama role modal wangu katika tasnia hii ya uhamasishaji aliwahi kusema kwamba Ni bora kujiandaa na ukakosa fursa utajifunza,kuliko kutokujiandaa na ukapata fursa, hiyo itakuwa kazi bure.
Nakwambia hivi ili tusikimbilie fursa kabla ya kujua fursa mana tusipozijua hazitajua na wala hazitaleta muunganiko katika maono ya maisha ambayo tunayataka.Mtu mwerevu utamkuta anaishi uyeye lakini mtu akikosa hekima asilimia kubwa utamkuta katika makundi, yani yeye maamuzi yake yatakuwa yanategemea na kundi lake linasemaje sio yeye mwenyewe.(kama unahii tabia 2017 jitahidi kuiacha)Kwanini nasema hivi?
Fursa tunaweza kuzifanya kwa kuanda akili zetu kifikra na kimatendo  ili kwelii fursa tuseme na ionekane fursa.
Tukifanya hivo hatutashindwa kuzifanya fursa vizuri. Soma vitabu vya kukusaidia kujua jinsi ya kuendesha fursa kama GUIDE TO INVESTING by ROBERT KIYOSAKI omba ushauri wa fursa ambayo unafikiria kuifanya Kwa watu ambao ni sahihi pia, jaribu kukaa na watu ambao watafanya usonge mbele.Kama unaweza kupata mtu wa kukuongoza katika kuifanya fursa vizuri mkamate mkono uhakikishe kwamba anakufikisha hiyo sehemu ambayo unataka.

Usiogope changamoto ukipata fursa flani.Kuna usemi mmoja unasema Kwamba fursa ni ngumu lakini Ugumu ni fursa.Hauwezi kupata kitu kizuri bila kuwa na changamoto, na changamoto hauwezi kuzipata kama haujaribu sehemu sahihi. Changamoto huja sehemu mbili kuu ambazo  mwanzo na unapofikia mwisho, ndo maana wahenga wakasema mwanzo mgumu. Lakini kumbuka na unapokaribia mwisho wa safari yako majaribu au changamoto huongezeka mana jua shetani hapendi ufanikiwe na wala hapendi kuona kwamba ulimshinda kule pa mwanzo mgumu.

SOMA ;KWANINI USIACHE AJIRA YAKO

Lakini tukumbuke katika kuzifanya hizi fursa Unaweza ukawa na maarifa na nguvu lakini ukikosa ithubutu hivi vyote havina maana pia.Ukishanoa akili yako kwaajili ya fursa kingine ambacho huwa kinafwata ni uthubutu (willingness) kufanya hiyo fursa kiusahihi.

Lengo langu Mwaka 2017 TUENDE PAMOJA nisikuacha.

Kama bado hujachukua copy ya kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA  Kwa 10,000/= karibu sana kujipatia. Sehemu  yoyote utakipata.

Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational Speaker

Author    : NGUZO 3 ZA MAISHA
Contacts : 0753616584 - 0653386586
Email     : lazarosamweli41@ gmail.com

0 comments:

Post a Comment