Tuesday, January 24, 2017

KWANINI USIACHE AJIRA YAKO.



 Tokeo la picha la quote  about why i should not leave my job
Habari mpenzi msomaji wa mtandao huu wa Lazaro Samwel naimani u mzima wa afya na Mungu Anakusaidia katika kupambana na shughuli zako kuhakikisha kwamba mwaka huu unakuwa mwaka wa tofauti na miaka mingine yote.Nakupongeza kwa juhudi hizo ambazo zinaonesha kiu ya mafanikio katika maisha yako.

Najua kichwa cha makala hii kitakuwa kimakupa hamasa sana  ya kujua kwamba kwanini usiacha kazi yako.Najua ushaambiwa mengi kuhusu ajira lakini kwa asilimia kubwa ni kwamba umesikia ubaya wa ajira.Nikwambia kitu kuhusu ajira ambacho nimekuja kugundua kwamba wengi wetu tumeshindwa kuelewa.Ajira ni kama kipaji ambacho kitakusaidia kukufikisha katika kusudi lako kama kweli utaelewa kwamba kipaji kinaweza kupotea muda wote kama hutaweza kukinoa vizuri.Ajira sio mbovu ila sisi wenyewe ndo wabovu katika kupokea taarifa kuhusu ajira na kujisahau kwamba njee ya ajira tunatakiwa kutengeneza maisha ambayo yatasaidia watoto wetu kwa baadae.Ajira huwa na mtindo mmoja ambao naomba nikikumbushe kwamba kama hutaangalia unaweza hata kusahau familia yako na hata watoto wako muda mwingine hata wasijue uthamani wako kama mama au baba katika familia.Hii ndo tunasema kwamba unasahau kuhusu wewe na kukumbuka kuhusu wengine ambao wamekupa ajira kwa masaa 18 na ukirudi nyumbani unawakumbuka watoto wako kwa  lisaa 1 tuu na kusinzia.Najua hakuna mtu ambaye anapenda maisha ya namna hii lakini pia sio makosa ya ajira makosa ni yako kwa kuon ajira kama ndo mwisho wa kufanya mambo yako.Huwa napenda kutumia msemo mmoja kwamba Ukiona sehemu ambayo mtu haridhiki na kile anachokipata jua hiko sio kiyu ambacho kinaweza kumtoa kimaisha.

Kunamambo ambayo unatakiwa kuyafanya kabla ya kuingia kwenye ajira, mana ajira sio kitu pekee cha kukutoa kimaisha lakini inaweza kuwa usafiri wa kukutoa sehemu moja kwenda ingine  kimaisha kama kweli utaelewa mambo yafuatayo;

1.Kuwa na mpango nje ya ajira.
Na hii ukitaka kujuan kwanini watu wengi wanaingia kwenye ajira na hata wanalipwa mshahara mkubwa lakini maisha hayabadiliki ni kwasababu hakuna malengo na mikakati njee ya ajira yake.Hii ina maana hata mshahara ukiingia hajui ataupeleka wapi na atakachokiwaza ni kuhakikisha kwamba hela anaitumia kuonesha ufahari wa njee na kuacha kuweka hela katika mpango thabiti ambao angekuwa ameupangilia ungemfanya kuwa mbali.Huyuhuyu mwajiriwa ndiye ambaye analalamika kuhusu ugumu wa maisha na muda mwingi wa kufanya kazi ambao unawachosha wakati anakipato kikubwa.Ndo maana kwa wenzetu ulaya hata kama uko kwenye ajira lakini mfanyakazi anapewa mafunzo kuhakikisha kwamba kweli ajira ambayo anaifanya inambadilisha kweli. Kunamuda tusiseme kwamba AJIRA mbaya ila sisi ni wabaya sana hata pindi tunapopata ajira, mana hatutendei haki hata kile ambacho tunakipata katika kazi zetu.

Kama unajua kwamba umeajiriwa hakikisha mambo ambayo unayafanya hayatazidi kukutoa mshahara wako au kukutoa hela mfukoni,  wazungu wanasema kwamba DON’T BUY LIABILITIE'S BUY ASSETS AND LET ASSET'S INCREASE YOUR INCOME ,hii niliezea kwenye kitabu Changu Cha NGUZO 3 ZA MAISHA.

 Sababu 1  tuu Kwanini nakwambia kwamba usiache ajira? Ajira hautakiwi kuiacha kwasababu ifuatayo,

1. Ajira usiiache lakini itumie iweze kukufanya wewe mwenyewe kuacha hiyo ajira.Usitumie ajira  ikufanye uendelee kuitumikia. Ila itumie ajira uache kuajiriwa  ili na wewe uajiri wengine ambao hawajui kutumia ajira zao.Tukumbuke kitu kimoja kwamba kwa sasahivi vijana wengi wanakimbilia kuajiriwa hii ni kwasababu hawana Mipango njee na kuajiriwa , na kijana usikimbie ajira kama huna kitu cha kufanya.Chukua muda kwanza kuhusu kuajiriwa na piga mahesabu kwamba wewe malengo yako ni yapi njee na kuajiriwa alafu sasa ingia kazini lakini akilini mwako kuwa na sauti ya kwamba unafanya ajira hiyo kuweza kuhakikisha kwamba unatimiza malengo yako njee na ajira kupitia kipato ambacho utakuwa unakipata,achana na zile tabia za kwamba mshahara hautoshi kwahiyo ngoja nikanywe pombe niumalizie huko,huku unajipeleka pabaya.Tunasema kwamba ukiitumia ajira vizuri automatical itakuhitaji wewe uiache uende kuendelea na kuendeleza malengo yako,ila kama hautaweza kuingia na mipango ajira unaweza kuitumikia mpaka kustafu na maisha yasiwe yamebadilika.

Nini Maoni Yako? Weka Maoni Yako.

Nashukuru Sana Kwa Muda Wako Na Ubarikiwe Sana.Kama hujapata kitabu Changu Cha NGUZO 3 ZA MAISHA tunaweza wasiliana nami au kubadilishana mawazo kupitia
Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational  Speaker
Author      ; NGUZO 3 ZA MAISHA
Email        ; Lazaro Samwel
Contacts  ; 0753616584 – 0653386586

0 comments:

Post a Comment