Tuesday, January 24, 2017

MWENZAKO AKINYOLEWA ZAKO TIA MAJI KWELI

Tokeo la picha la success quotes after learning from what someone didnt do and die
www.lazarosamwel.com
Karibu mpenzi msomaji wa makala hii ya Lazaro Samwel  kwa kuendelea kuwa moja katika ya watu ambao ni wafuatiliaji wazuri wa masomo haya katika mtandao.Inawezekana isiwe kusudi lako lakini ni kwamba kunakitu Amabacho Mungu anazaidi kukuonesha kuweza kufanya jambo ambalo amekuleta duniani kulitimiza.Napenda kukwambia kwamba uko sehemu sahihi na Twende Pamoja sasa.


Huu msemo ambao leo nimependa kuuweka kama kichwa cha makala hii ni msemo ambao naimani umeanza kuusikia kwa muda mrefu sana na inawezekana kwamba bado unaendelea kuusikia vizuri .Nimependa kuutumia mana ni msemo ambao unalenga maisha yetu kwa asilimia kubwa  sana kwasababu ni  msemo ambao kwa Upande mwingine unakukumbusha kuhusu wajibu wako hapa duniani kama umeshasahau.Huu msemo kwa lugha ingine ni sawa na mtu kukwambia kwamba Ukiona jambo flani kwa mwenzako limetokea kama changamoto za maisha sasa  na wewe inabidi kujiandaa kwa kuona tatizo ambalo mwenzako amelipata kama la kwako. Ukiona mwenzako alikuwa na malengo makubwa na alishawahi kukwambia kuhusu malengo yake lakini hakuweza kutimiza ,inabidi ujifunze kutoka kwa huyo mwenzako,kaa chini fanya mambo yako kama kesho haitakuwepo,weka mipango na mikakati kama kesho hauatakuwepo duniani mana kunawengi ambao Mungu amekupa chansi ya kusikiliza siku zao lakini mwisho wa siku wao wameshindwa kuzitimiza.Inabidi ujiulize kwanini Mungu mimi tu ameniacha kusikiliza hizi ndoto za watu ambao leo hii hawapo duniani? Nikwambie kitu kimoja kusikiliza kwako mambo ambayo wengine wameacha hapa duniani bila hata kutimiza sio tuu taarifa ambayo inatakiwa kukufikia, ni taarifa ambayo inatakiwa kukutoa katika usingizi ambao unao wa kusema kwamba kesho nitaanza kufanyia kazi maono yangu au kesho ndo nitaanza kutumia muda wangu vizuri.
Jiulize maswali mawili matatu kwamba ulisikia mangapi kwa rafiki yetu Malumbo Sambala Mtumishi wa Mungu na Muhamasishaji ambayo yalikuwa makubwa sana zaidi hata ya jinsi ulivokuwa unadhani na leo hii Mungu kampemnda zaidi? Umejiuliza pia ni mangapi Steve Jobs alikuwa anatamani kuyafanya lakini leo hii yale maono aliyokuwa nayo ameondoka nayo? Jiulize pia ulisikia marafiki zako wangangapi ambao walikuwa na maono makubwa lakini hawajayafikia lakini na wewe Hutaki kutia zako maji?
Nikwambie kitu mpenzi msomaji wa makala hii ya Lazaro Samwel ,haujawahi kujiuliza kwamba kunawakati unapita sehemu na unamawazo ya kitu flani lakini ghafla unakuata watu wanaongea ,lakini ghafla ukasikia neno moja ambalo ndilo linakuwa kama suluhisho katika mawazo yako,au ndo linakuwa kama jibu la kitu ambacho ulikuwa ukiwaza?  Huwa naamini Mungu hufanya mambo kwa makusudi makubwa sana.Anapokuacha usikilize matatizo ya wengine au anapokuacha uone mahangaiko ya watu wengine sio kwamba anakupenda sana kuliko Yule ambaye unamwona ila inawezekana anampa Yule mtu funzo kwa kutokumsikiliza  zamani na kukupa wewe mwenyewe funzo kwa unapoelekea.Ndo maana  nakwambia kwamba MWENZAKO AKINYOLEWA ZAKO TIA MAJI, kunavitu katika maisha havipingiki ila ndo maana tunasema kwamba TIA MAJI.Kama umeshagundua kipaji chako kitumie sana sasahivi hakuna muda wa kusema kesho mana kesho inaweza isiwe kesho yako.Siongei  na vijana tuu,hata na kwa watu wazima bado una chansi kubwa sana ya kufanya makubwa sana na wewe TIA MAJI hata kama ukimwona mtu mdogo yeye kanyolewa. Miaka Ni Namba tuu na akili hauwezi kuisema kwamba imezeka sana kiasi kwamba hauwezi kufanya mambo makubwa.

Nashukuru Sana Kwa Muda Wako Na Ubarikiwe Sana.Kama hujapata kitabu Changu Cha NGUZO 3 ZA MAISHA tunaweza wasiliana nami au kubadilishana mawazo kupitia;

Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational  Speaker
Author      ; NGUZO 3 ZA MAISHA
Email        ; Lazaro Samwel
Contacts  ; 0753616584 – 0653386586

0 comments:

Post a Comment