Sunday, January 22, 2017

NI MUHIMU KUJUA UMUHIMU WA KUFANYA KITU UNACHOKIPENDA NA KUTAFUTA PESA.


Kunamtu mmoja anaitwa Vincent Van Gogh aliyezaliwa Netherland mwaka 1853 na kufa 1890 aliwahi kusema Ni bora kufa kwa kitu ninachokipenda kuliko kile ninachokichukia na kama utakuwa mfuatilia Vincent Van  Gogh aliweza kujitoa kufanya kazi ambazo zilikuwa na ustadi wa hali ya juu na hata picha na maneno  ambayo alikuwa akichora na kuandika zilikuwa ni za kufikirika  na kugusa hisia za watu sana. Vincent Van aliweza kuacha historia kubwa sana na bado inaendelea kusomwa na watu wanazidi kuona unahiri huo ambao alikuwa nao.

Tokeo la picha la Vincent Van Gogh success quotes
www.lazarosamwel.com


Nini ambacho nataka Tuende pamoja hapa?? Maisha hayaendi kwa upande wa kujilazimisha kufanya manbo ambayo huyapendi. Na mafanikio hayaji kwa kujilazimisha kufanya kazi kusudi maisha yaweze kusonga mbele. Siri mojawapo ya kuona kwamba unafanya kitu ambacho unakipenda ni kutumia nguvu nyingi alafu mavuno hayakudhi mahitaji yako. Unaweza kuigiza uwongo lakini uhalisia hauwezi kuuigiza mana itajionesha. Angalia kazi inayoifanya ni kweli inayoka moyoni mwako?? Au unafanya kwaajili ya shidah ulizokuwa nazo? (Nitaandika makala ambayo inahusu jinsi ya kunufaika na kazi na usiiache pia)

Kuna mtu mmoja anaitwa Wanda Akyes aliwahi kusema kwamba, if you feel like there is something out there that you are suppose to be doing, if you have a passion for it , then stop wishing and just do it, kwamba kama Kama kunakitu sehemu unaona kwamba unatakiwa kukifanya, na kama unaona unakipenda , acha kuwa na matakwa/matarajio ( wishes), kifanye. Hapa nacho kukwambia ni kwamba hakuna mafanikio sehemu ambayo unajilazimisha lakini mafanikio ambayo unayataka yapo sehemu moyo wako, nafsi yako na akili yako zilipo.Unaweza kufanya kitu na kikakupa hela nzuri sana lakini kama sio kitu ambacho unakipenda hiyo hela sio kitu.

Nikupe siri moja kuhusu hela na kufanya kitu ambacho unachokipenda au kutokukipenda.
Unapofanya kitu ambacho unakipenda hela yako utaituma kununua vitu ambavyo vinathamani lakini unapokuwa unafanya kitu ambacho hukipendi hela yako  utakuwa unaitumia kununua gharama yani naongelea kwamba kauli yako ya matumizi sio kununua uthamani wa kitu ambacho unakitaka.Nikueleweshe kitu kimoja hapa, watu wanaonunua vitu kwa gharama.Hapa wanachukua vitu ambavyo sio vya thamani mana wanachokipata sio cha kutosha. Waingereza wanasema kwamba YOU BUY A PRICE NOT A VALUE  kwamba unanua bei sio thamani.Lakini madhara yake ni kwamba utakuwa unanunua kila siku kilekile kitu mana wew ulinunua gharam na sio thamani, kunamsemo unasema kwamba Cheap is expensive and expensive is cheap, kwamba cha _Urahisi  unahharama kubwa na Cha gharama kinaurahisi_ kama uneamua kununua simu ya 5000/= na mwingine akaenda kununua ya 50,000/= hapa mmoja atakuwa ameangalia ubora wa simu na mwingine kaangalia gharamya ya simu. Huyu ambaye ameangalia bei unaweza kukuta hiyo simu ni nzuri kwa njee lakini ni mbovu, hii itamfanya kurudi tena na tena kununua kama ataendelea kuangalia bei. Lakini huyu mwingine kaona sio shidah akanunua simu yenye ubora kwa 50,000/= huyu atakaa na simu hata kwa mwaka wewe kwa kurudirudi unakuta kwa mwaka umetoa 150,000/= kwa simu za 5000/=. Kuwa Makini.

Ophrah Winfrey pia aliwahi kusema kwamba Passion Is Energy kinyume chake Boredom is not energy, mtu hana nguvu ila anatengeneza nguvu kutokana na hali yake anavoiweka ndani yake katika kufanya kitu flani.Haswa katika kitu unachokipenda mtu huwa na nguvu ya kipekee sana kuweza kuhakikisha kwamba anafanikiwa katika jambo lake. Jiangalie je kitu ambacho haufanikiwi inawezekana umevamia sehemu ambayo sio sahihi.

Napenda kukucha na msemo mmoja wa Ella Fitzgerald alisema kwamba Usikate tamaa kujaribu kufanya kitu ambacho unataka kufanya. Pale penye upendo na hamasa, sidhani kama hautakifanya sahihi.Najua huu mwaka umeanza na inawezekana umeshaanza kukumbana na changamoto katika hatua ambazo unachukua kutimiza malengo yako, napenda kukwambia kwamba usikate tamaa kama kweli unapenda kitu ambacho unakifanya na kinakupa changamoto, jua iko siku kutakupenda pia na kukupa mambo ambayo ni picha tuu katika akili yako kwa sasahivi.

Kama utahitaji kuongea nami au kubadilishana mawazo unaweza kunipata kama;

Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational  Speaker

Author     ; NGUZO 3 ZA MAISHA
Email      ; lazarosamweli41@gmail.com
Contacts ; 0753616584 - 0653386586

USIKOSE COPY YA KITABU CHANGU CHA NGUZO 3 ZA MAISHA.

0 comments:

Post a Comment