Sunday, January 22, 2017

UKUBWA WAKO LAZIMA UTEGEMEE UDOGO WA WENGINE

 Tokeo la picha la quotes concern success doesnt depend on being great
Habari mpenzi msomaji wa Mtandao wa Lazaro Samwel naimani wewe ni mtu mwenye kiu ya mabadiliko katika maisha yako na unahitaji vitu sahihi kuweza kuhakikisha kwamba maisha yako yanakuwa ya tofauti. Twende Pamoja;

Naimani ulishawahi kusikia kuhusu msemo mmoja wa Ndege Tai kwamba ni mfalme wa Anga, lakini bila kusahau ukasikia pia msemo wa Ndege wenye mabawa sawa Huruka pamoja, haijatosha pia wakaenda baharini wakasema kwamba Samaki wakubwa hula samaki  wadogo.  Nisikupeleke mbali naomba tuje kwa upande huu wetu ambako unasikia kwamba ukitaka kifanikiwa lazima ukae na watu ambao wamefanikiwa, kwamba ukikaa na watu wenye mawazo duni lazima na wewe utakuwa duni. Au ukitaka kuwa mtu mkubwa lazima ukae na watu wakubwa.  Nikupe Siri Moja Tai hawezi kuruka na tukamsifia bila kuangalia kitu cha kula Ardhini kwa maana ingine kwa wanyama au ndege wenzake ambao amewazidi ukubwa na nguvu, hawa samaki wakubwa hawawezi kuendelea kuishi kama pia hawa samaki wadogo wasingekuwepo.

Naomba nikwambie kitu kimoja kwamba mafanikio kwa asilimia kubwa inategemeana na  jinsi  inavoishi na watu woote kwa namna flani.  Kunamtu mmoja anaitwa Wallace Wattler aliwahi kusema kwamba mafanikio hayaji kwa kufanya kitu flani lakini mafanikio yanakuja kwa kufanya kitu flani kwa namna flani nachotaka kukwambia ni kwamba kuwa na watu wa hadhi ya chini sio kwamba utakua maskini na kukaa na watu matajiri sio kwamba utakuwa tajiri hata kama watakuonesha mambo ambayo wanafanya.Hakuna mtu yoyote ambaye amefanikiwa kwa kufanya vitu vyake kwa wenzake ambao  wamefanikiwa kama yeye ila kwa watu ambao wako chini au tofauti na hali yake. Ndo maana nilikupa misemo Ambayo inasema kwamba Ukitaka kufanikiwa kaa na watu waliofanikiwa, kuonesha kwamba haya mambo Muda Mwingine inabidi tubadili fikra kuyawazia zaidi.Naomba kukwambia kwamba kama katika asilimia ukitaka kufanikiwa 30% kaa na watu waliofanikiwa na kwa maarifa ambayo watakuwa wanakupa tumia ipasavyo kwa 70% ya watu ambao unaona hawajafanikiwa unapokaa nao.Hapo ndipo mafanikio yanapokuja. Angalia wakina Aliko Dangote wanavofanya unadhani wanawekeza kwa wakina Dewij, angalia Buffett anavyofanya unadhani anawekeza kwa matajiri wenzake? Angalia Dewij, Backhresa, Dr. Reginald Mengi hela zao zipotoka, kumbuka zinatoka kwa watu wa hali ya chini na sio wa juu kama yeye. Kitu ni kwamba hiyo 30% unaitumiaje na 70% unautumiaje ukiwa na watu ambao watu wanasema kwamba hawajafanikiwa??

Kwa lugha nyepesi hauwezi kuruka bila kukanyaga ardhi na hata matajiri hawawezi kuwa matajiri bila kuwa na muunganiko mkubwa na watu wa chini.

Tukutane Kwa Muda na Wakati Mwingine. Ulikuwa nami ;

Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational   Speaker

 Author     ;NGUZO 3 ZA MAISHA 
Email       ; lazarosamweli41@gmail.com
Contacts ; 0753616584 - 0653386586 

0 comments:

Post a Comment