Saturday, January 21, 2017

MAISHA NI KUONESHA UTOFAUTI WA FIKRA TOFAUTI


Tokeo la picha la quotes about life being compressive

Habari mpenzi msomaji wa mtandao huu wa Lazaro Samweli.,naimani ufuatiliaji wako wa mtandao huu haukuachi bure kwa ambayo unajifunza.Leo naomba pia niweze kukushirikisha ujumbe huu mfupi ambao naamini kwamba utakubadilisha kifikra na kiakili.TWENDE PAMOJA.

Kunamoja kati ya makala ambayo niliandika kuhusu uwekezaji nilisema kwamba uwekezaji watu wanashindwa kuelewa kwasababu wengi wanawaza uwekezaji katika upande mmoja. Ni sawa na kusema kwamba maisha Tukiyatafsiri kwa upande mmoja vilevile hatutaweza kuyaelewa.Sitaeleza kwa upande huo wa uwekezaji lakini nataka nikulete upande huu ambao utaweza kukuweka karibu na msemo mwingine uliopita. Maisha  yanakuwa magumu kwasababu tunatazama na kuyapeleka katika upande ambao wengi wanasema na kutenda.  Msemo huu nitaunganisha na msemo mwingine uliozoeleka unasema Maisha hayana Fomula. Nakwambia hivo kwasababu wengi wanatazamia maisha kwa kuangalia wengine.Tunasahamu kwamba maisha hayana fomula kwasababu kila mmoja ana njia yake ya kufanya mambo yake vizuri.Bila kusahau kwamba kila kitu mtu alichobarikiwa na Mungu ni vitu tofauti hauwezi kutumia fomula ya maisha ya mtu mwingine ukasema kwamba utafanikiwa au hauwezi kufuata  kanuni za mtu flani na ukafanikiwa katika maisha yako vizuri,hapana, hautaweza kwasababu wewe unakanuni zako za kufanikiwa na pia unakitu ambacho kinaendana na kanuni ulizokuwa nazo ndani yako. Cha msingi usipumzike kujua kitu ambacho unachondani yako kuweza kujengea kanuni za kuweza kufanikiwa.Pia nakukumbuka katika safari ya kugundua haya mambo hakuna kitu kirahisi na hautakiwi kuweka uvivu ndani yake mana unaweza kuanza safari ya kutambua hicho kitu maisha yakakupa mgongo yani majaribu ambayo hujawahi kuyaona katika maisha yako na shetani akaongeza zaidi majaribu ili ukate tamaa. Usisikilize sana haya majaribu na wala usiyatafsiri kwa mawazo chanya.Songa mbele endelea kupambana tena kwa usahihi zaidi,acha uchekwe, uzaraulike, usengenywe, ila jua ulimwengu  ndivyo ulivo ukitaka kwenda mwelekeo sahihi wa maisha yako ambako wengi hawapo na wanapenda kwenda lakini wavivu kujisongesha mbele.

 SOMA: MAFANIKIO YANAHITAJI UTII

Naimani ulishakutana na kundi la marafiki zako ambao wanataka kuwa kama wao na hata kukutenga unapotaka kutofautiana nao. Nikwambie kitu kimoja kwamba Maisha ni mazuri sana ukijijenga katika msingi ambao umeumbiwa kujijenga. Ila ni mabovu sana ukienda kujijenga katika msingi ambao hukupaswa kujijenga. Utakuwa unapoteza Muda.

Wote Tuko Safari Moja Maisha lakini Safari Hii inabidi Tusalimiane na Kushirikishana Ya Mbele Ili Tuweze Kufika salama.

Lengo langu Ni TWENDE PAMOJA-@2017 Nisikuache kama mwaka 2016 ulivokuwa kwako

Kama Bado Hujajiunga Na TWENDE PAMOJA-@2017, nione nikupe Utaratibu Wake.

LAZARO SAMWEL 
MOTIVATIONAL AND INSPIRATIONAL SPEAKER

AUTHOR; NGUZO 3 ZA MAISHA 
Email     ; lazarosamweli41@gmail.com
sms/call ; 0753616584 - 0653386586

0 comments:

Post a Comment