
Kunausemi mmoja unasema kwamba mbegu huota pale unapozipanda, huu msemo rafiki yangu Nicholous alishawahi kuniambia nikawaza sana. Lakini baadhi ya mawazo machache yalikuja akili mwangu. Kwamba hii mbegu tunaweza kuichukulia kama mambo yetu ambayo tunayafanya na kuota sehemu ambayo imepandwa ni jinsi tunavyoweka mambo yetu sehemu flani tukitegemea kwamba yataleta matunda mazuri. Mbegu haiwezi kuota katika udongo ambao hauna rutuba bila kusahau na unyevuunyevu yani udongo wenye majimaji kama kusaidia uhai wa mbegu.
Mambo mengi ambayo tunayafanya lakini hatuoni matunda mazuri ni kwasababu yemekosa mambo yafuatayo;
1. Kutokuwa na chaguzi Sahihi.
Nikudokeze kitu kimoja kwamba katika maisha kunakuwa na chaguzi na chaguzi ambayo unafanya zinachangakia kayika jambo lako kufanikiwa. Unapokuwa na chaguzi sahihi kazima utakuwa na juhudi binafsi kubwa sana lakini ukakose kuwa na chaguzi katika maisha yako hauwezi kufanya kiti kwa moyo wako. Mfano ushwahi kukutana na mtu ambaye anafanya kazi ambayo hapendi au ambayo alikosea kufanya chaguzi zamani? Naimani unajua wanavyokuwa, kwanza hawawezi kufanya kazi kwa ustadi mzuri yani ni kulipualipua kwao. Chaguzi sahihi zinazalisha juhudi sahihi sehemu sahihi.
Hata katika mbegu ziko za aina nyingi na watu huchagua kutokana na mazingira yao pia wakiwa na imani kwamba zitaleta kitu wanachokiwaza baada ya kupanda. Ndivo chaguzi za maisha yetu zilivyo.
2. Kukosa lengo Chanya
Sifa mojawapo ya mtu kutokukaa sehemu moja na akaifanya kwa usahihi ni kukosa lengo ya kuwa sehemu ile na kukosa lengo sikuzote ni kukosa msimamo wa kufanya jambo flani kwa usahihi.Yani mtu hakai sehemu moja na akaifanyia kweli,,utakuta leo yuko hapa kesho kule.Lakini huyohuyo anategemea mabadiliko katika maisha yake. Mabadiliko hayako kwa kubadilisha mambo ya kufanya kila siku mabadiliko yanakuja kwa kuwa na mtizamo tena chanya katika mambo machache au jambo flani. Hii huwatokea watu ambao mara nyingi wamevania jambo flani bila kuwa na msimamo na kujua kwamba wanataka nini. Nikwambie kitu usiishi kwa maneno ya watu haswa wafanya biashara mara nyingi wanakosa Malengo ya biashara zao, leo unaweza kumkuta hapa kesho unamkuta katika biashara ingine pia, sasa hapa ndugu yangu unategemea ufaulu kweli?? Mana kitu ambacho unakigusa kinakuwa na kanuni zake za kufanikiwa na zinamaarifa yake pia. Unapofanya kitu flani kwa moyo wako wote na kwaakili zako zote tunasema kwamba huwezi kushindwa kufanikiwa mana huko ndiko lengo lenyewe lilipo na umejidhatiti kwa kila jambo.
3. Kukosa maarifa.
Tunasema kwamba mbegu inahitaji udongo wenye rutuba, na hii rutuba ambayo nakwambia ni maarifa. Ila hili limekuwa tatizo mana watu maarifa wanadhani ni kufanya kitu kwa jinsi unavosikia kwa wengine, wanasahau maarifa ni kutoka sehemu ulipo hidhuria semina za kitu ambacho unakifanya, kuwa ba mentor wa kukuongoza kitu ambacho unakifanya( hapa kumbuka mentor mzuri ni yule amabye anafanya au ameshawahi kufanya jambo ambalo unataka kufanya au ambaye analijua jambo hilo vizuri), kusoma vitabu sana japo hapa wengi wanakuwa wavivu sana kuthubutu na ndomaana mambo mengi yamefichwa sana kwenye vitabu na ni wachache sana ambao wanatambua kuhusu hili.
Ziko nyingi sana lakini Naomba hizi tatu kwa leo zikufungue na TWENDE PAMOJA-@2017
Lengo langu mwaka huu 2017 nisikuache ndio maana nimekuja na Mfumo wa TWENDE PAMOJA-@2017 ambao mtu akipata kitabu changu cha NGUZO 3 ZA MAISHA kwa 10,000/= utapata soft copy ya kitabu cha MY VIBE ATTRACTS MY VIBE pamoja na SEMINA ambayo nitafanya katika Group la TWENDE PAMOJA-@2017 kwa wewe ambae utakuwa umenunua kitabu kwa 10,000/= hizi zote utapata.KARIBU SANA.
LAZARO SAMWEL
MOTIVATIONAL AND INSPIRATIONAL SPEAKER
AUTHOR; NGUZO 3 ZA MAISHA Email ; lazarosamweli41@gmail.com
sms/call ; 0753616584 - 0653386586
0 comments:
Post a Comment