Habari mpenzi msomaji wa mtandao wa Lazaro Samwel nazidi kukupongeza kuwa pamoja nami katika kuhakikisha kwamba tunabadilisha historia ya maisha yetu sio mimi tu ambaye nataka kubadili maisha yako hata wewe leo ambaye umeamua kuchukua maamuzi ya kusoma makala hii naamini uko katika sehemu sahihi ya kuweza kubadili maisha ya wengine kupitia na wewe kutoka sehemu moja ya maisha kuelekea sehemu ingine ambayo ni nzuri zaidi.
| www.lazarosamwel.com |
Kabla ya kwenda mbali ningependa kuwashirikisha msemo mmoja wa Manya Biashara mmoja mkubwa sana duniani anaitwa Richard Branson mwanzilishi wa kampuni Ya VIRGIN ambayo inamiliki ndege,inastudio ya kurekodi n.k alisema hivi nanukuhu Biashara ni wazo la kufanya watu wengine maisha mazuri. Wazo la biashara ni kitu ambacho watu wengi sana wamekuwa wakisaka na kuweza kuamua kujifunza lakini wamefika mahali bado mambo hayajaenda vizuri.Watu wengi sana husubiri kuwa na kiwango kizuri sana cha pesa ndipo wanaweka malengo au ndipo wanapoanza kutafuta wazo la biashara, naomba kukwambia kitu kimoja, makala hii sio kwaajili ya kukupa wazo la biashara lakini itakusaidia kukuonesha jinsi unavoweza kuliweka wazo lako la biashara hata kabla ya kupata pesa.Ila kama wewe utakuwa ni mzembe wa kuweza kufanyia kazi haya mambo ambayo nitaenda kuyaorodhesha ni bora uache hapa na kuendelea na mambo mengine mana utakuwa unajidanganya lakini kama uko tayari kufanyia kazi mambo ambayo nitaenda kuyataja hivi punde naamini kwamba nitakuwa naongea na mtu mwingine wa tofauti kwa kwa miaka inayokuja.Cha msingi fungua akili yako na tumia ubongo wako katika vitu ambavyo naenda kukushirikisha.Wazo la biashara sio gumu kupatikana lakini ugumu wake huanza pale mtu anapochukulia kweli ni ngumu sana kupata wazo la biashara,au wengine kwa kuwa na mawazo kamba wazo la biashara lazima liwe kubwa sana ndo liwe wazo la biashara,hapana, wazo ni kitu kimoja ambacho kinaanza kwa udogo sana lakini wazo hilohilo kama utaweza kulifanyia kazi utakuwa mtu wa tofauti sana katika maisha yako.Wazo la biashara ni wazo kama utalifanyia kazi ila usipolifanyia kazi litabaki kuwa wazo kichwani mwako.
Ni mswali gani muhimu ambayo mtu anatakiwa kuyazingatia anapotengeneza wazo la biashara?
1. Lazima Uhakikishe kwamba Unakuwa na mipango thabiti, na utambue yafuatayo
a.Kwanini anataka kuwa na wazo la biashara au kusudi la wazo lako la biashara ni lipi?
b. Unataaka kulifanyia wapi kazi au mazingira gani ambayo unaona wazo lako linaweza kufanya kazi vizuri?
c.Unategemea nini katika biashara yako? Jua pande zote kwamba upande wa hasara unakuaje na upande wa faida unakuaje pia.
d. Utalifanya kwa Muda gani na faida unataka iweje?
VITU MUHIMU KUZINGATIA KATIKA WAZO LAKO LA BIASHARA
1. Kuwa Mboreshaji.
Katika karne ya 21 mambo mengi sana ambayo utakuwa unawaza na kuyapata ni mambo ambayo yakujirudia kwa asilimia kubwa ila tatizo ambalo linakuja ni mtu kukosa ubunifu wa kitu flani unachokifanya na kufanya biashara vilevile kama wengine wanavofanya ili na wewe uweze kujikwamua kiuchumia.Hiyo ni ngumu kwasababu kama unafanya biashara ile ile ambayo unaona watu wengine wanafanya tena kwa muundo uleule jua utaishia kuwa kama walewale unavowaona walivyo na kama haitakuwa hivo basi utawapita kidogo sana kutokana na utofauti wa juhudi zako na zao.Navosema kuboresha ni kwamba kama umepata wazo la kuuza matunda lakini sehemu ambayo unataka kuazisha hiyo biashara kunamtu anafanya hizo boresha kwa kubadilisha na kutengeneza juice au hata unasweza kukata matunda na kuweka sehemu nzuri ukaanza kutafuta oda za watu sehemu tofauti.
2.Liwe Wazo La Kipekee.
Ninapoosema kwamba wazo kuwa la kitofauti ni kwamba mtu akiona biashara yako akuone wewe na sio mtu mwingine.Yani kama tunavozungumzia kuhusu JUICE ZA AZAM tunajua pale ni BAKHRESA na Tunapozungumzia kuhusu ITV,STAR TV na vipindi vyake tumwone kweli DR.REGINALD MENGI au ukienda kwa ulaya unapozungumzia Kampuni Ya APPLE Tunamwona Hapo STEVE JOBS ,Ukiona mtandao wa FACEBOOK unamwona MARK ZUKERBERG,Unapoingia ALIBABA.COM unamwona JACK MA. Nachomaanisha ni kwamba uwe na biashara ambayo hata usikuwepo watu wajue kwamba huyu ni flani kafanya hiki sio mtiu anaona biashara yako anaanza kusema kwamba huyu sio flani au flani?
Hapa hakikisha kwamba biashara yako inakuwa au unaitengenezea jina katika soko tofauti na watu wengine ambao wanaotaka kufanya kitu kama chako.
3.Hakikisha wazo lako la biashara linawaza kulenga kutatua matatizo ya watu ambayo yanawakumba kwa silimia kubwa katika jamii au inchi yako.
kama Richard Branson alivoweza kueleza kuhusu biashara kwamba Ni wazo ambalo linaweza kufanya watu wengine kuishi maisha mazuri.Mfano unaona sehemu ambayo unaishai watu wanakosa huduma ya vitafuno vizuri kwaajili ya asubuhi kwaajili ya chai na wewe unaweza kutengenezea,sasa kwanini usifanye hiyo biashara na ukajitengenezea hela au sehemu ambayo unaishi watu wanashida ya mashine ya kusaga unga kwanini usitumie hela yako ukaweka mashine hapo?
4.Kuwa na wazo ambao linaweza kuwa nafaida kwa baadae.
Kuwa na wazo ambalo kwabaadae lazima litakutengenezea kipato kizuri zaidi.
Mawazo mengi sana ambayo watu huwa nayo mara nyingi ni mawazo ambayo yanawaletea faida kwa hapa na pale lakini kuna kitu kimoja kwamba wazo la biashara ambalo ni zuri na linauwanda mpana sana kwa kuangalia mbele siku zote huwa nachangamoto mwanzo sama na inawezekana hata ukaingia hasara kubwa sana katika kuiendesha,lakini ukijua kusudi lake huataweza kukata tamaa katika kuendelea kuifanya..
Naomba Tushie hapo na tukutane Tena katika makala nyingine ya kibiashara ambayo itakuwa inakazia sana kuhusu JINSI YA KUTENGENEZA MPANGO WA BIASHARA.Ulikuwa nami;
Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational Speaker
Author : NGUZO 3 ZA MAISHA
Contacts : 0753386586 - 0653386586
Email : lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment