Unapoenda kumwomba Mungu haitaji wewe uende kumwomba akufanye kuwa kama mtu mwingine. Unapoenda kwake anahitaji uede kwa jinsi alivokuumba na uombe akuendeleze zaidi ya pale ulipo. Kosa ni kumwona Mungu hayuko sahihi kwasababu hakukuumba kama mtu mwingine. Mafanikio Mengi ambayo huwa tunayataka kupitia msaada wa Mungu inakuwa ni ngumu sana kuyapata kwasababu pindi tunapoenda kuhitaji msaada kutoka kwake huwa tunaenda na kuomba kutubariki sehemu ambayo sio sisi. Mfano wewe umebarikiwa kuwa na Kipaji cha Kufanya biashara na hicho ndicho ambacho unahitaji kukikuza na kuomba baraka za Mungu ziwe juu yako lakini unapoenda kumwomba Mungu unamwambie akubariki kuwa Mwimbaji.Shida ni kwamba atakusikilizaje kukubariki ikiwa unachoomba kubarikiwa sio ambacho amekupatia. Mana inabidi tuelewe kwamba baraka huja sehemu sahihi na wakati sahihi, lakini sisi ndio ambao huwa tubapishanisha hizi baraka kwa kutaka vitu ambavyo Mungu hataki sisi tuvifanye.
Kunamsemo mmoja unasema kwamba Kuwaza ni kitu kigumu na ndo maana sio woote ambao wanajishughulisha kuwaza na wengi ambao hawataki kuwaza ndio ambao hushangaa vitu vya watu wanaowaza na kuweza kupata Baraka kwa Mungu.
SOMA : MAFANIKIO YANAHITAJI UTII
Nachotaka kukwambia ni kwamba, sio rahisi kuwaza ili uweze kupata kitu ambacho unakipenda kukifanya ili pindi usimamapo kwa Mungu uweze kupata Baraka tele.Kwa upande mwingine inawezekana kama kweli utaamua na kutokukata tamaa katika kuendelea kutafuta kusudi ambalo litakusaidia kupata baraka hizi.Hakuna dini ambayo haijui kwamba Mungu wetu ni Mungu wa Huruma lakini pia hana upendeleo. Hilo lisikufanye uwe na kiburi cha kusema kwamba utafanikiwa, hapana, Mungu anahitaji kumsaidia Mtu ambaye anawaza, anamshirikisha Mungu Alichowaza,anatoa sababu na pia kuweka juhudi zilizoambatana na maarifa katika mambo ambayo aliwaza na akamshirikisha Mungu kuweza kumsaidia na kumpa baraka zake.
Nimekutajia hapa ili siku ukiona mambo hayaendi vizuri ni kwamba urudi nyuma na kuangalia kwamba jee ni kweli nashughulisha akili yangu? Je namshirikisha Mungu nachowaza? Huwa ninasababu ya ninachowaza baada ya kunshirikisha Mungu?? Na mwisho jee huwa nachukua hatua?. Ukiona katika maswali haya hapana zinazidi ndio inabidi uchukue hatua ya kuongeza Ndio katika maswali haya. Uzembe ambao nimekuja kuutambua ni kuelewa katika nyakati hizi wengi tumesahau kwamba mafanikio yetu yanamtegemea Mungu, hata ukiangalia wahamasishaji wengi hili swala kulisisitiza ni wachache sana ambao wanafanya hivi, japo unaweza kukuta wenyewe wanasali ila kuandika na kueleza uma wanaona kama watu watawakimbia. Wanasema ukitaka kufanya biashara angalia kitu wateja wako wanachotaka, ila kitu kimoja muhimu katika mafanikio katika sehemu ya kusaidia watu hili swala kuhusu Mungu usiangalie wateja au wasikikizaji wako wanataka nini, fanya kuwaambia na waache wakimbie mana wakienda watarudi tuu. Kila dini mfano Waislamu wanaonesha unuhimu wa sala katika maisha yetu, na wakristo pia hivohivo. Kitu ambacho tunatakiwa kukifanya ili tusiwe kama watu wengine na tukakosa baraka ni kuwaambia watu kwamba wakiachana na uvivu wa kumshirikisha Mungu katika mahitaji yao ya mafanikio hakuna kitakachoshindikana.
Nikuache na Hii misemo ambayo naamini mpenzi msomaji wa mtandao wa Lazaro Samwel itaenda kubadilisha maisha yako,
- Unaposoma Vitabu vingi vya mafanikio bila kuwa na Muunganiko mzuri na Mungu ni kazi bure. Waswahili wanasema kwamba utakuwa unatwanga maji kwenye kinu.
- Ukijilinganisha wewe na wengine kwa mapungufu ambayo unayo utajenga tabia nzuri ya kushindwa katika kila jambo ambalo unataka kufanya.
- Unapoona wengine wanafanikiwa usifikiri kuwa wao na wala usiwe na tamaa na wai ila waza ni namna gani na wewe unaweza kuendeleza ulichokuwa bacho ndani kikawa zaidi ya malengo yako.
Asanteni Sana na Tukutane Tena Katika Makala Ingine na Muda Mwingine. Ulikuwa nami,
Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational Speaker.
Author : Nguzo 3 Za Maisha
Email : lazarosamweli41@gmail.com
Contacts : 0753616584- 0753386586
0 comments:
Post a Comment