Sunday, January 15, 2017

KUWA HALISI NA MAMBO YAKO YAWE HALISI


Tokeo la picha la QUOTES CONCERN BE NATURAL

Kila mmoja anakitu ambacho akiweza kujitambua tuu itakuwa sio yeye  tu ambaye ataona uthamani wake na kujiheshimu.Hata jamii  pia lazima itatupia jicho lakee ambalo huanza kukuangalia  wewe kama tunu kwa woote wanaomzunguka. Nikwambie kitu kimoja kwamba hauitaji kuwa sawa na wengine ili uwe kama unavotaka kuwa na kama watu wengi wanavohitaji uwe. Pia hauitaji kuwa kama wengi walivyo ili jamii na watu ambao upo nao karibu yako wakuheshimu. Inakuchukua Kuishi kiuhalisia kuweza kupata heshima halisia  na sio heshima kwasababu wewe ni mbabe, Mwizi, mwonevu, mwongeaji, msengenyaji sana n.k Ni mambo ya ajabu sana kuona kwamba unatumia vigezo hii kuheshimu na kuweza kukuza mafanikio yake.  Siri Ingine ya mafanikio iko katika kuheshimika kwa Kujitambua kwako (Hili Somo Liko Kwenye Kitabu Changu Cha NGUZO 3 ZA MAISHA)

Mafanikio Mengi ambayo wengi huwa wanayakosa ni kwasababu ya kutokutaka kuwa wao bali kuwa Wale ambao sio wao kwamba unaiga mtu ambaye yeye mwenyewe anaiga kwa mwingine. Mafanikio ni kama nafsi halisia ambayo inatafuata mtu halisi na sio mtu ambaye leo yuko hivi kesho yuko vile utapoteza mwelekeo.Nakumbuka zamani nilikuwa napenda sana kuja kuwa mwalimu kwasababu Tuu Ya kuona wazazi wangu kuwa Walimu pia lakini kumbe nilikua nikilazimisha fani ambayo haikuwa mimi ndani yangu, na hii nimeingundua baada ya kuingia chuo na kuanza kusoma vitabu vingi na kujitambua zaidi. Hata heshima ambayo sasahivi ambayo ninayo sio kwaajili ya kuishi maisha ya wengine ila ni kujiangalia mwenyewe ndani na kuona kwamba kumbe Mimi sio wazazi wangu, rafiki zangu, ndugu zangu,ila mimi ni mimi na ninakitu tofauti na wazazi wangu, ndugu au jamaa.Licha ya hivo sikufuata marafiki wala ndugu kuwa kama wao, hapana lengo nilikuwa nataka kuwa mimi na nichukue nafasi ya kuwa Mimi. Hata mafanikio yanakuhitaji wewe kuchukua nafasi ya kuwa wewe na Kujitambua Zaidi sio  kuwa Mtu mwingine. Watu wengi ambao wanaweka juhudi za kuwa kama mtu flani kwa asilimia kubwa huishiwa kuwa sio kitu kwasababu unajaribu kuchukua nafasi ambayo ishachukuliwa na mwingine.Ni ujinga kuacha Nafasi yako ambayo hakuna mtu anaweza kuichukua katika maisha yako na kukimbilia ile ambayo imeshachukuliwa na sio yako.

Nisingependa nikuache hivihivi ila ningependa kukushauri kwamba Kama mwaka Ambao umepita manbo yako yalikaa hayaensi vizuri na hayakuleta matunda hebu kaa tulia angalia kama ni biashara je ni kwelij unafanya biashara ambayo ni ni wewe ndani yako au unafanya biashara ambayo ukiangalia pembeni ni rafiki yako?? kama ni tabia yako angalia jee unavyovifanya ni kweli tabia yako au ni rafiki zako pia?? Ukiona majibu mengi ambayo unapata ni sio wewe kunauhitaji mkubwa sana wa Kuweza kubadilika na kuchukua Nafasi yako ya maisha ili Uweze kupata mafanikio ambayo unayataka.

Hauwezi kutengeneza Kufuli Bila Ufunguo. Hivo ni sawa na kusema kwamba Hauwezi kuwa na mafanikio Bila Kuwa na Maarifa ya Kubadili Fikra Zako Na Kuweza Kuyatendea Kazi.

Tukutane Tena Muda Na wakati Mwingine Kuweza Kufungua Akili zetu.

Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational Speaker

Author    : Nguzo 3 Za Maisha
Email      : lazarosamweli41@gmail.com
Contacts : 0753386586-0653386586

0 comments:

Post a Comment