Sunday, January 15, 2017

IJENGE BIASHARA YAKO


Tokeo la picha la quotes concerning building a good business
 Habari Mpenzi Msomaji Wa Mtandao Wa Lazaro Samwel, Naimani uko salama Salmini.kama ilivowadia sipendi kukuacha mwaka Huu uwe vilevile na miaka mingine nataka mwaka huu nikufanya mtu wa tofauti na ndo lengo la mtandao huu kuhakikisha inaposoma post hizi usimame imara katika kujijua na kusonga mbele zaidi.

Leo Hi ningependa kuwashirikisha mambo mazuri ambayo naimani yatakusaidia kama utaamua kuchukulia hatua katika maisha yako.

Ningependa kuongea na wewe mfanyabiashara ambaye unandoto kubwa sana za kuweza kuja kuwa kama wakina McDonald, Warref Buffet, Aliko Dangote, Mo Dewij, Bakhresa, Dr. Reginald Mengi na wengine wengi ambao unawafahamu katika maisha yako. Nikwambie siri moja ya mafanikio katika biashara yako ambao wengi wameshindwa kuelewa na kutokufika mbali katika safari yao ya mafanikio katika biashara zao;

1.  Katika biashara yoyote ambayo unaifanya hakuna kitu kikubwa kama  kuithamini  biashara yako kabla ya kupata pesa.Unapothamini biashara yako zaidi ndipo itakapokupatia pesa unayotaka, lakini unapothamini pesa badala ya biashara yako huatapata kitu ambacho unakitaka katika biashara yako. Hapa napoongelea kuhusu kuithamini biashara yako simaanishi kwamba kuwa unaifanya kama wengine wanavoifanya, hapana, kwamaana kawaida ya watu wengi hufanya biashara na hawafiki mbali kwasababu wanachokifanya ndicho wengine wanachokifanya.

Namaanisha nini naposema kuithamini biashara yako? Ukiangalia watu wengi ambao  wamefanikiwa vizuri katika biashara zao ni watu ambao kwanza wamekuwa na utii katika utendaji wao wa kazi. Utii ni neno pana sana katika biashara. Ninaposema utii kwa upande mwingine ni  kuwa mvumilivu katika biashara zako na pia kujaribu kuleta kitu ambacho wengine inawezekana wanakifanya ila kwa utofauti ambao utakuwakilisha wewe kinamna yake.

Hakuna biashara ambayo utaanza leo na kukupa matunda ambayo unayataka leo hiihii. Angalia watu wengi ambao wameshindwa katika biashara nyingi unakuta ni kwamba hapakuwa na utii katika biashara zao. Walifanya biashara kwa uharaka wa kujijenga wenyewe na sio kuijenga biashara kuwajenga wao kwanza. Nikwambie kitu kingine kwamba kuithamini biashara yako ni uwanja mpana sana, haswa inaanza kwa mmiliki wa baishara yenyeww kujiheshimu ndani na njee. Biashara yako itajiuza kutokana nawewe ulivo. Kunamaswali ambayo inabidi ujiulize kama kweli unathamini biashara yako.

i. Je Unaendana na biashara yako?

Kwamba kwa faida ambayo unaitaka na wewe umejiwekea hadhi hiyo,kuanzia kwenye kuongea na wateja na mazingira ya biashara yako. Hata kama mteja wako awe na hadhi gani hakuna ambaye hataki huduma safi na ya kuheshimika. Angalia hili sana mana unaweza kukuta Unataka faida kubwa lakini bado biashara yako unafanya kama umelazimishwa, wewe mwenyewe sio msafi,mazingira unakuta ni machafu, lugha ya mteja kama anamkaripia, bidhaa ni chafu n.k  sasa unatakaje maisha yako kubadilika ingali wewe mwenyewe hutaki kubadilika ukaendana na biashara yako??

ii. Unataka biashara yako ifike wapi? Umejua kusudi la kuanzisha biashara yako?

Biashara yako lazima iwe na sababu ya kuwepo na hiyo sababu lazima kila muda inawekewa malengo na mikakati ya kuweza kuifikia. Ukiona biashara yako haikuwi nenda sehemu  angalia, uliiwekea malengo kutokana na sababu ya uwepo wake? au ulifanya kwasababu rafiki zako wanafanya? Wengi huwa tunaangukia katika kundi hili na ndo maana pia biashara kwa miaka 5 mpaka 10 iko palepale na maisha yako yanakuwa palepale. Hii sehemu ni muhimu sana mana unapotambua unapotaka kufika na unapotambua kusudi la biashara yako lazima uhakikishe kwamba unaitafutie maarifa ya kuiendeleza zaidi na zaidi, usiseme kwamba hakuna maarifa kwaajili ya kukuza biashara yako. Sasahivi kuna watu wanaandika vitabu vingi sana jinsi ya kukuza biashara yako, angalia kitabu cha kitabu Cha Makirita Biashara Ndani Ya Ajira, kuna mwandishi Mwingine anaitwa Kelvin Kitaso mmiliki wa Kampuni Ya Gracious Printing Ltd Dar-es-Salaam. Ukiona hautendei haki biashara yako, jua inawezekana unajilazimisha kuifanya au hujui unachokifanya ni kwa malengo gani. Amka Hapo ulipo fanya kitu kiwe kizuri zaidi.

Tukutane Tena Muda Mwingine kwa Somo Lingine pia. Ulikuwa Nami;

Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational Speaker

Author     : Nguzo 3 Za Maisha
Email        : lazarosamweli41@gmail.com
Sms/calls : 0753616584/0653386586

0 comments:

Post a Comment