
Lengo Langu ni Kukufanya wa tofauti kwa Kidogo Ulichokuwa Nacho,Ikiwezekana Unipite kwa kile ulichojaliwa nacho ukikijua Itakuwa Vizuri Zaidi.
Asilimia kubwa sana ya watu wanakuwa na mawazo makubwa na maono ambayo kweli yana uhai ndani yake lakini unakuta hayo mawazo ambayo wanayo wanashindwa kufika sehemu ambayo wanataka katika maisha yao kwa sababu ya kuwa na Asilimia ndogo ya Utii wa kutaka Kubadilika ndani yao.Ila tukumbuke kitu kimoja kwamba ukiona unatoka katika mawazo Madogo kuelekea Makubwa usipoteze muda wa wewe kuchukua hatua ya kujijenga ndani yako katika tabia ya Kuwaza mambo madogo kuelekea Mambo Makubwa.Mawazo yako muda mwingine yanaweza kukukimbia na yasilete matunda yoyote kwasababu unavoyavuta mawazo mazuri na makubwa unakuta ndani yako bado Unamazingira ya kukaribisha mambo mengine ambayo ni madogo tofauti na Mambo makubwa ambayo ulikuwa unayataka.Lakini pia bado Utii wa Kuweza kujitoa kufanyia kazi mambo makubwa unakuta hakuna, unasahau kwamba mambo makubwa yanahitaji utii mkubwa wa kuweza kuyafanya kuweza kuyatimiza.Nimeshawahi kukutana na watu ambao wanamawazo mazuri sana lakini ndani yao utii wa kutengeza mazingira wa hayo mawazo hakuna wanaishia kuyapoteza kwa wengine.
Huwa na wazo la Namna hii kwamba Kama ilivo ndoto, maono, kusudi, kipaji na vingine vingi ni nafsi ambazo ziko duniani zinazunguka na kuangalia mahali pa kukaa , kwa lugha ingine zinatafuta sehemu ambazo zinaweza kuonesha uhalisia wao ndani kupitia nafsi mbili ulizokuwa nazo ndani yako yani Nafsi Ya Mema na Nafsi Ya Mabaya.Lakini hatuwezi kuziona kwa macho ya kawaida zaidi ya kutengeneza mazingira hayo ndani yetu na sisi ndio ambao tunaweza kuonesha huo uhalisia. Sasa tunawezaje kuviona hivi vitu au mtu anawezaje kuwa na nafsi mojawapo kati ya hizi ambazo nimezitaja Kuendana na nasfi kuu mbili ambazo nimezitaja zilizoko ndani yetu? Twende Pamoja;
1. Lazima kwanza uoneshe utii wa kukubali kubadilisha mazingira ya zamani ndani yako na kuwa mpya.
Nakuahidi sio kwamba ni rahisi ila inachukua uthubutu kufanya hivo ndo maana hapa tunasema utii kwasababu mambo yatakuwa ya kupanda na Kushuka. Lakini katika utii hapa tunaweza kujumuisha kuwa na utayari na kuamua kwelii kufanya jambo flani ambalo unalipenda lakini unalishindwa. Angalia Ophrah baada ya kuambiwa kwamba hana Mwonekano mzuri katika runinga alifanya nini mpaka leo ana Tv Show kubwa Duniani, Angalia wakina Les Brown ambaye aliambiwa anamatatizo ya akili lakini akawa Muhamasishaji mkubwa duniani ambaye kwa masaa matatu anaingiza zaidi $5000. Wewe unatukanwa tuu unaacha kujitengenezea mazingira yako mazuri ya kitu unachokipenda.Inakuchukua utii kuweza kuacha kusikiliza maneno ya watu na kusonga mbele katika ramani ya mafaniko yako.
2.Kuishi maisha yako ya Uhalisia.
Nafsi za namna hii haziitaji mbwembwe zaidi ni halisi na zinahitaji mtu ambaye anaishi katika uhalisia. Hapa namaanisha nini?? Namaanisha kujikubali, kujiona na kusema kwamba kwamba nilivoumbwa sijakosewa na kujua kwamba uuambaji wa Mungu kunileta hapa duniani namna hii ni ili uweze kuendana na Baraka ambazo alishakuandalia hapa duniani. Na ndo maana wengi ambao hawajikubali jinsi walivyo mara nyingi wanaishia kutokuishi maisha ya raha au maisha ya ndoto zao kwasababu wanapishana na nafsi ya kuwa wanavyotaka kuwa. Wewe unaweza kuumbwa na pungufu flani lakini kumbe Mungu kashaweka nafsi ambayo kwa pungufu lako utaelimisha wengine na utakuwa tajiri.Lakini unakuta mtu anajibadilisha, leo anaweka hichi kesho kile mwilini mwake, unakuta kwamba anapishana na baraka zake. Hapa mfano mzuri ni kutoka kwa Muhamasishaji Nick Vujic ambaye hana mikono wala Miguu lakini leo hii ni mfano wa kuigwa, hajamwambia Mungu kwamba Ni bora asingemwumba. Leo wewe kidogo tuu umesemwa kwa kukosa kitu flani unakata tamaa na bado unamiguu na mikono vizuri. Badilika sasa angalia kutengeneza nafsi za mambo ambayo unataka kuwa nayo duniania.
Lazaro Samwel
Motivational And Inpirational Speaker
Author : Nguzo 3 Za Maisha
Contacts : 0753616584/0653386586
Email : lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment