
1. Nafsi ya kutenda mema
Hii ni nafsi ambayo imebeba mafanikio na kila jambo jema ambalo unalijua. Hii nafsi ni nafsi ambayo inamfanya mtu kufika sehemu ambayo anaitaka katika maisha yake, haswa inakuwa na mtizamo chanya na maisha ya mtu. Kama ni juhudi, kutafuta maarifa na kusaidia wengine hii nasfi inakuwa na sauti ya kipao mbele kuhakikisha kwamba unafanya jambo jema. Nakwambia nafsi ni nafsi nzuri kwasababu Inamuunganiko Mkubwa na Mungu kuliko Nafsi yoyote na jinsi unavozidi kuijenga na kuiwekea mazingira mazuri ndivyo na wewe unavozidi kuona maajabu katika maisha yako.Nafsi ya kutenda Mema ni nafsi ambayo cha kwanza lazima uijenge kwa maarifa na uelewa mkubwa, kumbuka navokwambia hivi usione kama ni rahisi ila inahitaji kujitoa na juhudi binafsi ya kulipa gharama.Huku ndipo mafanikio yalipo,
2. Nafsi Ya Mabaya
Hii nafsi kwa lugha ya kawaida tunasema yenyewe huwa na sauti ya juu kutaka kutawala mtu hata kama yule mtu haiitaji nafsi hii.Ndo maana kunahitaji sana hekima kutoka kwa Mungu kuweza kuhakikisha kwamba unaikataa hii Nafsi pindi unapoona inataka kukupeleka sehemu ambayo sio sahihi katika maisha yako.Hii ni kwasababu nafsi hii imeunganishwa na mambo maovu mengi sana ambayo huwa yanafanya mtu kutokufanikiwa katika maisha yake. Kwa lugha nyepesi ni kwamba inamwunganiko mkubwa sana na shetani na ndo maana ndani yake utakuta kuna chuki, kisirani, dharau, kujiona wa thamani kuliko mtu yoyote,kuwa mtu wa kukatishaa wenzako tamaa,Kuwa msengenyaji mzuri katika mafanikio ya wenzako.Haya ndo matawi ya Nafsi Ya Mabaya.
Nafsi kama hii utaweza kuiondoa, kwanza kuwa mtu wa sala sana na Tambua Mungu anasema nini katika Maisha yako kupitia vitabu vitakatifu kama BIBLIA AU QURAN . Pia usikae na watu ambao ukikaa nao ni washawishi wakubwa wa wewe kuweza kuamsha nasfi mbaya/ Ya Maovu au kuipa nafsi hii uwezo wa kukutawala na wewe kuanza kunena kama wao.
Baada ya kukueleza haya nitaomba nikuelekeze kwanini hatufanikiwi?
Hatufanikiwi kwasababu watu hawajajua ni nafsi gani ambayo wanatakiwa kuilisha chakula sahihi. Nafsi Moja kati ya hizi mbili inaweza kutoka kutokana na Jinsi unavozipa nafasi katika maisha yako.Kama utaipa nafsi ya kutenda maovu inamaana nafsi ingine ya kutenda mema haitakuwa na nafasi katika maisha yako.Ni sawa na msemo mmoja ambao unasema kwamba kama umejaza mawazo potofu katika akili yako inatakiwa watu wasishangae wewe kutokuwa na hekima mana hata akili yako itakuwa imejaa na haina sehemu ya kuweza kuweka hiyo hekima.
Lazaro Samwel
Motivational And Motivational Speaker
Author ; Nguzo 3 Za Maisha
Contacts : 0753386586
Email : lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment