
Lengo langu katika kukuletea makala hii mpenzi msomaji ni kwamba usijutie kubonyeza link hii na kurudi bure kama mara ya kwanza lengo ni kuweza kukubadilisha kuweza kuelewa nini Tofauti Ya Ndoto (Dreams), Mission (Kusudi/Lengo) Na Maono( Vision).
Haya ni maneno ambayo kila mmoja huwa anajiuliza na wengine huchanganya kabisa kuelewa maana Zake , sasa twende Pamoja.
1. Ndoto ni ile hali ya kujenga taswira katika akili yako ukiwa umelala. Kunaaina mbili za ndoto ambazo mtu huwa nazo hapo wengi wanaweza kuweka kiaina nyingine pia,
a. Ndoto za haraka (fast moving dreams)
Hizi ni ambazo mtu inakuwa ngumu kukumbuka kile alichoota.Hizi ni ngumu sana kuweza kuzikumbuka mana unakuta mtu anajua nimeota lakini hakumbuki kitu. Tukumbuke kitu kimoja kwamba hakuna mtu ambaye haoti ila sema wengi huwa tunakuwa katika aina hii kwamba hatukumbuki kitu ambacho tumeota.
b. Ndoto za kubadilika (fast changing)
Hizi hapa mtu anakuwa na uwezo wa kukumbuka japo hata kidogo mana zinakuwa na mabadiliko kwa muda unavozidi kwenda. Illa pia ni ngumu sana kutafsiri ndoto. Mdo maana unakuta ni wachache sana ambao wamepewa uwezo wa kutafsiri ndoto.Kwa zamani ukiangalia ukiangalia katika Biblia Watu kama Joseph ambaye kwa miaka 17 alianza kuwa na ndoto kutoka kwa Mungu alipata kuwa na uwezo wa kuweza kutafsiri Ndoto hasa kwa viongozi wa mfalme Pharaoh na pharaoh wenyewe Mfalme wa Misri (Pharaoh). Licha ya kipindi ndugu zake na baba yake kumwona wa ajabu kwa ndoto alizokuwa akiota haikuwa sababu ya kumtolea hiko kipawa chake( hapa jifunze pia) Mwanzo 40:16-22
2. Tukija katika upande wa pili nitapenda kukuelewesha kuhusu Maono (vision) na kusudi/lengo/Mikakati (Mision). Maono ni Kesho yako Itakuwaje na Kusudi/Lengo/Mikakati ni kwaajili ya leo nifanye nini niweze kuifikia Kesho.
Maono ni taswira ya kitu flani ambayo unaijenga kwa baadae kitakavokuwa, haswa hii sio wakati umelala. Hii mtu anaweza akawa amekaa na akafumba mambo akawaza na kuangalia kwa baadae itakuwa katika maisha yake. Na tunaposema kuhusu Kusudi/Lengo/Mikakati (Mision) hii hasa inaongelea kuhusu wakati uliopo na mara nyingi huwatokea watu ambao wanakuwa na Maono. Ili uweze kufikia maono ambayo unayo lazima uwe na malengo na mikakati ambayo tunasema kwamba ni vitu ambavyo unaweza kuvifanya kwa sasahivi kuweze kutimiza yale maono ambayo unaona kupitia akili yako kwa baadae.
Unapokosa Maono lazima Utakosa Malengo na Mikakati Na Unapokosa Maono ni kama na mtu hajui nini maana ya uwepo wake hapa duniani.Kunamsemo huwa napenda sana kuutumia unasema When you have vision you must have have mission to reach your vision , nikimaanisha kwamba ,Unapokuwa na Maono lazima uwe na Mikakati pia ya kuweza kufikia maono yako.
Lazaro Samwel
Motivational And Inspirational Speaker
Author : Nguzo 3 Za Maisha
Contacts : 0753616584/0653386586
Email : lazarosamweli41@gmail.com
0 comments:
Post a Comment