Monday, April 16, 2018

MIFANO HII ITAKUFUNGUA KATIKA MAISHA YAKO


Utasikia ooo wewe hiyo biashara haikufai,  ooo wewe huna lolote unaigiza tuu,  ooo wewe bado mdogo kula kwanza bata achana na mambo ya kiutu uzima, ooo hiyo biashara inakudhalilisha, ooo huwezi kuwa mwanamitindo,  ooo wewe huwezi kuwa mwandishi,  a lot of blaaah blaaah utazisikia sana tena hata kwa watu wako wa karibu sana ambao ulikuwa unadhani wangekupa ushauri mzuri.

Wakati Shakira akiwa anajifunza mziki mwalimu wake alimwambia "Shakira unasauti kama ya mbuzi." lakini Shakira hakukata tamaa na naimani kwa sasahivi ukiambiwa kuhusu Shakira na sauti yake unaelewa nachokwambia,  sio tena sauti ya mbuzi kama mwalimu wake alivyokuwa anasema, sio hivyo kama ulitazama kobe la dunia mwaka 2006 lililofanyika Afrika Kusini utakuwa unakumbuka mwimbo wake wa "WAKA WAKA".  Robert Goddard moja ya watu ambao leo hii mawazo yake yamechangia katika urukaji wa roketi kwa mara ya kwanza marafiki zake walimcheka sana kwa mawazo aliyokuwa anawaambia na muda mwingine hata kumzomea, Thomas Edison mvumbuzi wa balbu ya umeme aliambiwa na mwalimu wake kwamba " Ni mjinga kuweza kujifunza chochote." lakini leo hii tunaongea mengine na inawezekana hata uzao wa mwalimu huyo wake wanatumia Balbu zake, mchoraji Vincent Van Gogh wakati wa uhai wake michoro yake iilikuwa inadharauliwa sana na katika uhai wake ni mchoro mkoja tuu ambao akiuza kwa rafiki yake tena kwa bei ya chini sana lakini leo hii mchoro wake unauzwa zaidi ya dola milioni 100 ($100million's)

Nachotaka kukumbusha ni kwamba umeua ndoto zako ngapi kwa maneno ya watu ?  je unajua leo ungekuwa wapi kama ungesonga mbele katika ndoto uliyokuwa nayo ?  Kuna umuhimu gani kumsikiliza mtu anavyokukatisha tamaa ikiwa unajua hajui unachokijua hata kama ukimweleza ?
Nikukumbushe tuu kwamba kuna maneno mengi sana ambayo ukiwa kwenye safari yako ya mafanikio utayasikia na lengo unakuta ni kutaka kukutoa kwenye lengo lako husika haswa kisa wanaokwambia wako pembeni na hawaoni wewe unachokiona kule unapotazamia kwa kile unachokifanya.Unachotakiwa kukifanya ni usikilize tuu ile sauti inayokuita kule unapoangalia na kutaka kufika na hizi za pembeni waambie mpaka nifike ninapopaona lakini nyie hampaoni.

🆕 Utakuwa umefanya la maana sasa kubonyeza link hii kwa chini kudownload Application yako pendwa ya LAZAROSAMWEL kupata masomo mengine mengi ambayo inawezekana kipindi cha nyuma ulikuaa unafuatilia , bonyeza 👇🏾👇🏾👇🏾
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.lazarosamwel.app

Kocha Lazaro Samwel
0753616584
#akiliyaushindi

0 comments:

Post a Comment